Mgomo na Maandamano Dar, Tarehe 5/01/2016

Mgomo na Maandamano Dar, Tarehe 5/01/2016

Mtowa mada isijiumeze kichwa chako bure waulize wakaazi wa kigomboni kwa huyu baba pombe being ndio hiyo hiyo 1200 tutaisoma nomber
 
Utanichosha bure ,amini unacho amini wacha nibaki na imani /mawazo yangu pia
@Unclebe usichoke...nieleweshe kwa data na facts na sio vilio vya mtaani !

ukisema nauli iwe sh 400 utueleze sababu za hiyo sh 400....kwani bado utakuwa na watu wasioweza kuimudu!
 
Unawaongelea watanzania au wakazi wa Dar?
Usihamishe mada tetea kwa data na facts....jiulize wanaotakiwa kwenda huko posta ni kina nani ?au ni watu wa kipato kipi hasa hasa ukizingatia kuwahi ???
@ Jingalao ccm, Ikiona kkoo imejaa watu usifkir wote ni wakazi wa dar, weng wa nje ya Jiji la dar watayapanda hayo magar
 
Mifano
1. Hospitali
2. Mawasiliano (simu)
3. Vituo vya mafuta
4. Zima moto
5. Ulinzi
6. Mabenki
7. Redio

Sijaongelea uzalishaji kwa upande wa viwanda ambavyo ndio vitahitaji zaidi huduma za saa 24.
Mkuu unamaanisha unatoka Kimara kwenda Posta kufuata huduma ulizotaja?
Kama ni kufuata....basi huduma zote hizo zinapatikana maeneo ya pembezoni.

Na kama unaenda kuzitoa basi ni wazi kipato chako kitastahimili vizuri nauli hizo.
 
Kimsingi nauli ni kubwa, hata ingekuwa 700, bado ni kubwa sana. Inawezekana haya mabasi walengwa .ni maofisa wenye kazi zao huko Posta na hii inaweza kuwa mbinu ya kuhakikisha watu wa hovyo hovyo hawapandi haya mabasi.
Mkuu tangu itoke ile kauli kwamba mwenye hayo mabasi ajitokeze LA sivyo serikali itayachukua, mwenyewe alishapatikana???
 
Ndugu zangu tuna uzoefu wa mikutano hii kutumika kama muhuri maana watu hawaihudhurii, na wakiudhuria basi ni wachache sana. Na hapa ndipo jamaa hutumia mwanya huo kupitisha bei wanazotaka wao. Tumekuwa tukiona EWURA wakiitisha vikao vya wadau ili kupitisha bei za umeme na mafuta. Wadau wanaohudhuria ni wachache na mwisho wa siku ukilalamika unajibiwa "imepitishwa kwa kushirikisha wadau, mbona hukuja kutoa maoni yako?"

.

Hilo halina tofauti na Bunge letu linavyotumika kama Muhuri wa Mipango ya Mafisadi.
Inashangaza kuona wanaweza kuleta bei pendekezwa lakini sioni bei hiyo ifikiwaje?
Kilicho takiwa kujadiliwa ni namna bei ilivyofikiwa na siyo bei yenyewe-na hapo ndipo SUMATRA nao kuwa sehemu ya huu Ufisadi na hii ni Jipu na kama Magufuli kweli yuko kwa kutumbua majipu basi asichelewe kuliona hili.


Biashara ni kuchagua-kama wamenunua Magari yanayotumia gharama kubwa kwenye uendeshaji ni juu yao-maana Mtu mwingine anaweza kufanya maamuzi ya kibiashara kwa njia sahihi na kwa gharama Nafuu.

Waje watueleze kimaandishi walifikiaje gharama hiyo- na hili si kwamba lifanyike tukiwa ndani ya Ukimbi bali mapema 21days kabla ilitufanye utafiti na kuwa na hoja na siyo umbeya-kinyume na hivyo huu ni uhuni na sanaa za kila siku.
 
  • Thanks
Reactions: KXY
Kama ni kweli wamepanga hizo nauli ni kiasi kikubwa serikali inabidi iangalie ili suala kwa umakini mkubwa nchi zote usafiri wa umma unasimamiwa na serikali siyo kikundi cha wafanyabiashara wachache.
Hahahaaaa wewe nawe...
 
Mlikataaa madiliko na mh Lowassa mtajijua, Nyumba zenu mnabomolewa na nauli in a panda Mara tatu, na bei ya vyakula nayo tutaongeza, ataeshindwa ahame nchi
 
Mkuu unamaanisha unatoka Kimara kwenda Posta kufuata huduma ulizotaja?
Kama ni kufuata....basi huduma zote hizo zinapatikana maeneo ya pembezoni.

Na kama unaenda kuzitoa basi ni wazi kipato chako kitastahimili vizuri nauli hizo.
Hoja ya nauli inajadilika si tatizo.
Hoja niliyoiongeza ni usimamizi mzuri wa huduma ya usafiri kwa usiku.
Watu wanaofanya kazi hadi muda wa ziada pia wanahitaji usafiri wakitoka usiku.
Mfano ni waziri wa ardhi alivyotoa tamko kitengo cha huduma kwa wateja wafanye kazi hadi usiku.

Kwa sasa inaweza kuonekana si tatizo lakini miaka michache ijayo kuna matumaini uchumi utakua na mahitaji ya huduma yatakua vilevile.
 
Mkuu nadhani urekebishe headline. Kuhudhuria Karimjee siyo maandamano wala mgomo ni haki yako kama raia. Muhamasishane muendee. Lakini ulivyoandika unataka sasa dola itumie kisingizio izuie huo mkutano Karimjee. Tumia akili kuliko nguvu na siku zote utafanikiwa.
Vinginevyo una hoja nzuri sana na nzito.
 
Mafisadi wamewasilisha hoja la kifisadi mtaisoma namba na bado sana subirini
 
@gambalakobe heshima kwako mkuu. Nimependa timing unayo propose itumike na hamasa uliyoitengeneza.
Hiyo ndiyo namna inayopaswa badala ya kusu iri maamuzi yapitishwe halafu ndiyo watu waanze kuvutana na kulalamikiana.
 
Kiukweli kwa hii style wanachi tuliyowengi tujipange kurudi nyumbani kama affordable ya maisha ndo hii watu awezi ishi more than 45year ok niwakati wenu ccm
 
Kiukweli kwa hii style wanachi tuliyowengi tujipange kurudi nyumbani kama affordable ya maisha ndo hii watu awezi ishi more than 45year ok niwakati wenu ccm
Turudi vijijini tukalime tukuze uchumi!
 
Namkumbuka mwaka 2004 kama nitakuwa nijasahau kidogo, Nilikuwa Mombasa na Nilikuta town bus za serikali (matatu) AU Kenya bus nyingi zikiwa mpya 'mfano' wa hizi UDA ndogo ambazo zilikuwa zikizunguka route zilizopangiwa na kila kituo zilisimama na bahati mbaya hazikuwa na abilia labda mmoja mmoja aliyejilipua.

Baada ya kuuliza mbona hizo gari ni mpya na sioni zikiwa na abilia nikajibiwa na Jamaa yangu aliyekuwa anaishi mwinjaka kuwa kuna mgomo baridi "hizo matatu ziko na nauli ya juu sana, so kenyan we can't afford to pay hizo fair" nikamuuliza zaidi ndipo akatoa sababu kama zilizotolewa na Jamaa yangu @gambalakobe hapo juu.

Mwisho wa siku leo wanazipanda bila kinyongo na wanalipa nauli ile ile na isitoshe kwa sasa ipo juu zaidi, ambapo tofauti ni kuwa wao wanaheshimu zaidi sheria kuliko sie watz.
 
Last edited:
Back
Top Bottom