Mgomo na Maandamano Dar, Tarehe 5/01/2016

gambalakobe

Member
Jul 1, 2015
55
73
Katika hili ndugu zangu wana Dar es salaama naomba na kukiri kuitwa mchochezi na nitawajibika binafsi. Naomba waliotayari kuniunga mkono wasiogope, mjitokeze.

UDART, waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo Kasi yatakayoanza kutoa huduma hiyo tarehe 10/01/2016 wamepeleka maombi kwa SUMATRA kuomba iidhinishiwe gharama ya usafiri jijini Dar iwe ni Sh. 1,200/- njia kuu (Morogoro Road) ambayo kimsingi ni kutoka Kimara hadi Posta na Sh. 700/- njia za pembeni ambayo ni kutoka hapo ulipo kwenda ama Posta au Kariakoo.

Mwanafunzi ni nusu nauli ya mtu mzima (Yani wanafunzi watalipa Sh.700 kwa njia kuu na Sh.350 njia za pembeni kutoka Sh.200 wanayolipa kwa sasa). Kama ilivyo ada SUMATRA wameitisha mkutano wa wadau tarehe 05/01/2016 katika ukumbi wa Karimjee Hall saa tatu na nusu asubuhi ili kujadili na kupitisha nauli hiyo.

Ndugu zangu tuna uzoefu wa mikutano hii kutumika kama muhuri maana watu hawaihudhurii, na wakiudhuria basi ni wachache sana. Na hapa ndipo jamaa hutumia mwanya huo kupitisha bei wanazotaka wao. Tumekuwa tukiona EWURA wakiitisha vikao vya wadau ili kupitisha bei za umeme na mafuta. Wadau wanaohudhuria ni wachache na mwisho wa siku ukilalamika unajibiwa "imepitishwa kwa kushirikisha wadau, mbona hukuja kutoa maoni yako?"

La pili ni kwamba bei hizi hupangwa kwa mtego. Mfano hapo UDART wanataka Sh. 1,000/- (njia kuu) na Sh. 500/- (njia za pembeni) sasa wakisema 1200 au 700 wanajua mkilalamika sana mtashuka hadi kwenye bei wanazozitaka, na mtakua mmeingia kwenye mtego wao huo.

Tukumbuke kwamba toka awali tuliambiwa ujio wa mabasi hayo utarahisisha gharama za usafiri mbali uharaka wake.

Kwa sasa daladala zetu hizi mtu akiwa na Sh. 1,000/- anaweza kusafiri safari moja (barabara kuu 500/-) na safari nyingine (400) njia ya pembeni akatumia Sh. 100/- kula karanga.

Ombi langu kwenu: (1) Tarehe 05/01/2016 tujitokeze kwa wingi pale Karimjee Hall kiasi cha ukumbi kutapika. Yeyote anayedhani anaguswa na suala la usafiri Dar asibaki nyumbani. Tuifanye siku hii kuwa Bunge Huru la Dar. Wanafunzi Vyuo vikuu, mama Ntilie, wafanyakazi viwandani, machinga, walimu na wadau wote wa usafiri wa umma tunaomba mjitokeze kwa wingi wenu kuja kupaza sauti.

Tukatae gharama hii ni KUBWA mno wala tusiingie mtego huu. Nauli ya 1200 kwa 700 ni kubwa sana na inamuumiza Mtanzania maskini anayetegemea usafiri wa daladala. Hebu fikiria mama anayekaa Kimara anasafiri kila siku kwenda Soko la Samaki Feri kununua Samaki aje akaange auze apate vijisent vya kuendesha maisha yake na wanae.

Kwa nauli ya sasa anatumia Sh.6000 tu kwa wiki nzima (yani 500/= × 2 × 6). Lakini kwa nauli ya mabus yaendayo kasi atalazimika kutumia Sh.14,400 kwa wiki (yani 1200/= × 2 × 6). Ongezeko la Sh.10,800/= sawa na asilimia 140%. Hili ni ongezeko kubwa sana ambalo watanzania maskini wanaotegemea usafiri wa daladala hawawezi kumudu.

Ni lazima gharama hizi zishuke la sivyo watuachie daladala zetu. Tukiungana kwa umoja wetu tutashinda nguvu ya mabepari wanaotaka kutumia umasikini wetu kutajirika maradufu. Mabasi haya ni mapya, barabara ni mpya hakuna sababu ya kupandusha nauli kwa kiasi hicho. Tusitafsiri kauli ya "kusoma namba" kwa kukandamiza maskini. UVCCM, BAVICHA nk mtusaidie kwa hili bila kujali itikadi zenu.

05/01/2015 tukusanyike kwa wingi pale Karimjee Hall kupinga nauli hizi za kinyonyaji.. Siku hiyo ifanyike kuwa BUNGE HURU la Dar.
 
Hivyo viwango havikubaliki.........kwa namna yeyote haviwezi kukubaliwa....
 
Ccm mliichagua wenyewe,mliipenda mnaipenda."hapa kazi tu"
 

Attachments

  • 1451816397638.jpg
    1451816397638.jpg
    88.5 KB · Views: 41
Mleta mada ni muoga,dhaifu na mchochezi.
Sumatra huwa hawakurupuki kupandisha nauli,na kunakuwa na vikao si chini ya vitatu hadi nauli ipande.na watu wanajulishwa kwanza ili wajitayarishe.
Sioni hekima kwa mtoa mada kushawishi watu wafanye vurugu badala ya kushawishi wadau wajitokeze kuja kupinga nauli kwa data.je kikao kikihamia sehemu nyingine na wakapitisha nauli itakuaje?
Huu ni wakati wa kazi kwa juhudi maarifa na kufuata sheria sio kila jambo ni maandamano
 
Kama ni kweli wamepanga hizo nauli ni kiasi kikubwa serikali inabidi iangalie ili suala kwa umakini mkubwa nchi zote usafiri wa umma unasimamiwa na serikali siyo kikundi cha wafanyabiashara wachache.
Huwa nakufuatilia sana...! Mbona uwapongezi vijibwa wenzio..?
 
Back
Top Bottom