Mgomo na Maandamano Dar, Tarehe 5/01/2016

Kama unaona ni ghali tembea kwa mguu!
Mbona kiongozi wenu mkuu ni rafiki wa walalahoi kama anavyojipambanua ,inakuaje kwa nyie vibaraka kua na kauli hizi ?? Au ni zuga tu machoni pa watu ila moyoni anatekeleza kauli yake ya pigeni mbizi kwani nini bana
 
Hivi hizo barabara hazijajengwa kwa kodi zetu?
Au hao UDART ndo wametoa hela za kujenga kiasi cha kuzimiliki wenyewe?
 
MAANDAMANO SIO SOLUTION ILA NAUNGANA NA WEWE NAULI HIZO NI KUBWA UKIZINGATIA HALI YA KIFEDHA BADO SIO NZURI. HAO WALIOPANGA WAMEZINGATIA NINI HADI KUONGEZA, KWENI KUNA KIPATO CHA MWANANCHI KIMEONGEZEKA?? Hii biashara ina faida wasitake kukomoa wananchi.

Queen Esther

Katika hili ndugu zangu wana Dar es salaama naomba na kukiri kuitwa mchochezi na nitawajibika binafsi. Naomba waliotayari kuniunga mkono wasiogope, mjitokeze.

UDART, waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo Kasi yatakayoanza kutoa huduma hiyo tarehe 10/01/2016 wamepeleka maombi kwa SUMATRA kuomba iidhinishiwe gharama ya usafiri jijini Dar iwe ni Sh. 1,200/- njia kuu (Morogoro Road) ambayo kimsingi ni kutoka Kimara hadi Posta na Sh. 700/- njia za pembeni ambayo ni kutoka hapo ulipo kwenda ama Posta au Kariakoo.

Mwanafunzi ni nusu nauli ya mtu mzima (Yani wanafunzi watalipa Sh.700 kwa njia kuu na Sh.350 njia za pembeni kutoka Sh.200 wanayolipa kwa sasa). Kama ilivyo ada SUMATRA wameitisha mkutano wa wadau tarehe 05/01/2016 katika ukumbi wa Karimjee Hall saa tatu na nusu asubuhi ili kujadili na kupitisha nauli hiyo.

Ndugu zangu tuna uzoefu wa mikutano hii kutumika kama muhuri maana watu hawaihudhurii, na wakiudhuria basi ni wachache sana. Na hapa ndipo jamaa hutumia mwanya huo kupitisha bei wanazotaka wao. Tumekuwa tukiona EWURA wakiitisha vikao vya wadau ili kupitisha bei za umeme na mafuta. Wadau wanaohudhuria ni wachache na mwisho wa siku ukilalamika unajibiwa "imepitishwa kwa kushirikisha wadau, mbona hukuja kutoa maoni yako?"

La pili ni kwamba bei hizi hupangwa kwa mtego. Mfano hapo UDART wanataka Sh. 1,000/- (njia kuu) na Sh. 500/- (njia za pembeni) sasa wakisema 1200 au 700 wanajua mkilalamika sana mtashuka hadi kwenye bei wanazozitaka, na mtakua mmeingia kwenye mtego wao huo.

Tukumbuke kwamba toka awali tuliambiwa ujio wa mabasi hayo utarahisisha gharama za usafiri mbali uharaka wake.

Kwa sasa daladala zetu hizi mtu akiwa na Sh. 1,000/- anaweza kusafiri safari moja (barabara kuu 500/-) na safari nyingine (400) njia ya pembeni akatumia Sh. 100/- kula karanga.

Ombi langu kwenu: (1) Tarehe 05/01/2016 tujitokeze kwa wingi pale Karimjee Hall kiasi cha ukumbi kutapika. Yeyote anayedhani anaguswa na suala la usafiri Dar asibaki nyumbani. Tuifanye siku hii kuwa Bunge Huru la Dar. Wanafunzi Vyuo vikuu, mama Ntilie, wafanyakazi viwandani, machinga, walimu na wadau wote wa usafiri wa umma tunaomba mjitokeze kwa wingi wenu kuja kupaza sauti.

Tukatae gharama hii ni KUBWA mno wala tusiingie mtego huu. Nauli ya 1200 kwa 700 ni kubwa sana na inamuumiza Mtanzania maskini anayetegemea usafiri wa daladala. Hebu fikiria mama anayekaa Kimara anasafiri kila siku kwenda Soko la Samaki Feri kununua Samaki aje akaange auze apate vijisent vya kuendesha maisha yake na wanae.

Kwa nauli ya sasa anatumia Sh.6000 tu kwa wiki nzima (yani 500/= × 2 × 6). Lakini kwa nauli ya mabus yaendayo kasi atalazimika kutumia Sh.14,400 kwa wiki (yani 1200/= × 2 × 6). Ongezeko la Sh.10,800/= sawa na asilimia 140%. Hili ni ongezeko kubwa sana ambalo watanzania maskini wanaotegemea usafiri wa daladala hawawezi kumudu.

Ni lazima gharama hizi zishuke la sivyo watuachie daladala zetu. Tukiungana kwa umoja wetu tutashinda nguvu ya mabepari wanaotaka kutumia umasikini wetu kutajirika maradufu. Mabasi haya ni mapya, barabara ni mpya hakuna sababu ya kupandusha nauli kwa kiasi hicho. Tusitafsiri kauli ya "kusoma namba" kwa kukandamiza maskini. UVCCM, BAVICHA nk mtusaidie kwa hili bila kujali itikadi zenu.

05/01/2015 tukusanyike kwa wingi pale Karimjee Hall kupinga nauli hizi za kinyonyaji.. Siku hiyo ifanyike kuwa BUNGE HURU la Dar.
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana nadhani ndio nchi pekee unaweza kukuta huduma za serikari zinaweza shinda zile za private yaani serikari ikiwekeza mara nyingi ujue lazima waje na tozo za ajabu ajabu wakati hela inayotumika ni ya walipa kodi utadhani serikari ni familia nyingine na raia wake.

Hao Sumatra wakiwakubalia nauli mpya hii mijamaa na private nao si watataka kwani wao pia hawana gharama ambazo zinafanya kupata faida ndogo kutokana na nauli za sasa
 
Kweli tutaisoma namba. Najuta kufanya kazi mikocheni wakati nakaa kimara
 
kwanini nauli zisiwe zilezile kama za daladala? wasituongezee migharama ya maisha bana
 
Naunga mkono hoja kuwa nauli ni kubwa.
Kwa upande mwingine wanaoishi mbezi mwisho wameshazoea hali ya kulipishwa 1000 iwe kutoka mwenge ama posta, mabasi rasmi huyeyuka ikifika saa 1 jioni na hubaki hayo ya 1000.
Naona DART wameona inawezekana, usafiri wa umma wakati wa usiku ni suala la kufatiliwa kwa karibu.
 
Katika hili ndugu zangu wana Dar es salaama naomba na kukiri kuitwa mchochezi na nitawajibika binafsi. Naomba waliotayari kuniunga mkono wasiogope, mjitokeze.

UDART, waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo Kasi yatakayoanza kutoa huduma hiyo tarehe 10/01/2016 wamepeleka maombi kwa SUMATRA kuomba iidhinishiwe gharama ya usafiri jijini Dar iwe ni Sh. 1,200/- njia kuu (Morogoro Road) ambayo kimsingi ni kutoka Kimara hadi Posta na Sh. 700/- njia za pembeni ambayo ni kutoka hapo ulipo kwenda ama Posta au Kariakoo.

Mwanafunzi ni nusu nauli ya mtu mzima (Yani wanafunzi watalipa Sh.700 kwa njia kuu na Sh.350 njia za pembeni kutoka Sh.200 wanayolipa kwa sasa). Kama ilivyo ada SUMATRA wameitisha mkutano wa wadau tarehe 05/01/2016 katika ukumbi wa Karimjee Hall saa tatu na nusu asubuhi ili kujadili na kupitisha nauli hiyo.

Ndugu zangu tuna uzoefu wa mikutano hii kutumika kama muhuri maana watu hawaihudhurii, na wakiudhuria basi ni wachache sana. Na hapa ndipo jamaa hutumia mwanya huo kupitisha bei wanazotaka wao. Tumekuwa tukiona EWURA wakiitisha vikao vya wadau ili kupitisha bei za umeme na mafuta. Wadau wanaohudhuria ni wachache na mwisho wa siku ukilalamika unajibiwa "imepitishwa kwa kushirikisha wadau, mbona hukuja kutoa maoni yako?"

La pili ni kwamba bei hizi hupangwa kwa mtego. Mfano hapo UDART wanataka Sh. 1,000/- (njia kuu) na Sh. 500/- (njia za pembeni) sasa wakisema 1200 au 700 wanajua mkilalamika sana mtashuka hadi kwenye bei wanazozitaka, na mtakua mmeingia kwenye mtego wao huo.

Tukumbuke kwamba toka awali tuliambiwa ujio wa mabasi hayo utarahisisha gharama za usafiri mbali uharaka wake.

Kwa sasa daladala zetu hizi mtu akiwa na Sh. 1,000/- anaweza kusafiri safari moja (barabara kuu 500/-) na safari nyingine (400) njia ya pembeni akatumia Sh. 100/- kula karanga.

Ombi langu kwenu: (1) Tarehe 05/01/2016 tujitokeze kwa wingi pale Karimjee Hall kiasi cha ukumbi kutapika. Yeyote anayedhani anaguswa na suala la usafiri Dar asibaki nyumbani. Tuifanye siku hii kuwa Bunge Huru la Dar. Wanafunzi Vyuo vikuu, mama Ntilie, wafanyakazi viwandani, machinga, walimu na wadau wote wa usafiri wa umma tunaomba mjitokeze kwa wingi wenu kuja kupaza sauti.

Tukatae gharama hii ni KUBWA mno wala tusiingie mtego huu. Nauli ya 1200 kwa 700 ni kubwa sana na inamuumiza Mtanzania maskini anayetegemea usafiri wa daladala. Hebu fikiria mama anayekaa Kimara anasafiri kila siku kwenda Soko la Samaki Feri kununua Samaki aje akaange auze apate vijisent vya kuendesha maisha yake na wanae.

Kwa nauli ya sasa anatumia Sh.6000 tu kwa wiki nzima (yani 500/= × 2 × 6). Lakini kwa nauli ya mabus yaendayo kasi atalazimika kutumia Sh.14,400 kwa wiki (yani 1200/= × 2 × 6). Ongezeko la Sh.10,800/= sawa na asilimia 140%. Hili ni ongezeko kubwa sana ambalo watanzania maskini wanaotegemea usafiri wa daladala hawawezi kumudu.

Ni lazima gharama hizi zishuke la sivyo watuachie daladala zetu. Tukiungana kwa umoja wetu tutashinda nguvu ya mabepari wanaotaka kutumia umasikini wetu kutajirika maradufu. Mabasi haya ni mapya, barabara ni mpya hakuna sababu ya kupandusha nauli kwa kiasi hicho. Tusitafsiri kauli ya "kusoma namba" kwa kukandamiza maskini. UVCCM, BAVICHA nk mtusaidie kwa hili bila kujali itikadi zenu.

05/01/2015 tukusanyike kwa wingi pale Karimjee Hall kupinga nauli hizi za kinyonyaji.. Siku hiyo ifanyike kuwa BUNGE HURU la Dar.

Sawa mkuu umeskika. Toa gambalakobe tutambuane basi
 
Mbona tunazifunga kamba akili zetu..

Kama gharama ni kubwa watu watatafuta namna. ...mbona kuna wapanda baiskeli mjini.

Hao wameona daladala ni ghali pia kuna watembea kwa miguu.

Kwa wafanyabiashara. ..Mfano wakaanga samaki watapandisha bei ya samaki ili kuweza kupata nauli na faida. ..hiyo hofu ya gharama ni illussion
 
Pia ikumbukwe, hii nauli ikipandishwa hivi, na mikoan pia inapanda, kwa hiyo hili linatuhusu sote watanzania, sio wa dar es salaam pekeyao..
 
Tatizo kubwa hapa ni kwamba kunauwezekano mkubwa huu sio mradi wa serikali bali ni kwamba wapigadili. Mtazamo wangu nikwamba huu mradi hautatatua kero yausafiri kwa walio wa serikali kipato cha chini.Pia bado suala lafoleni litakuwa palepale. Serikali wangeweleza kwenye usafiri wa kipato treni inge punguza sana Tatizo la foleni kwani miundo mbinu yake ni rafiki kwa mazingira pia haichukui nafasi kubwa katika ujenzi wake na niwangharama nafuu sana inabeba idadi kubwa ya abiria kwa wakati mmoja . Ubinafsi na ufisadi unafanya kuanzishwa miradi km hii ambbayo haina tija.
 
Mbona kiongozi wenu mkuu ni rafiki wa walalahoi kama anavyojipambanua ,inakuaje kwa nyie vibaraka kua na kauli hizi ?? Au ni zuga tu machoni pa watu ila moyoni anatekeleza kauli yake ya pigeni mbizi kwani nini bana
Asilimia 70 ya watanzania wako vijijini wanatembea kms za kutosha tu kutoka kijiji A kwenda B....bado hawajapata barabara na usafiri wa uhakika.

Nyie wa Dar mliojaziwa miradi lukuki ya mawasiliano mnaleta nyodo....I REPEAT ASIYEWEZA KULIPA NA ATEMBEE KWA MGUU !!
 
Back
Top Bottom