Mgomo na Maandamano Dar, Tarehe 5/01/2016

Mgomo na Maandamano Dar, Tarehe 5/01/2016

Kujadiliwa...
Hivi umejitoa ufahamu ama unafanya maigizo?
Umesema hivi:

"Huu ni uongo hakuna kitu kama hicho..."
"Huyo jamaa ni muongo wa kupitiliza ni mchochezi ....soon utaona"

Sasa mimi nikaweka taarifa rasmi kama ilivyoripotiwa na Mwananchi, kwamba ni kweli hizo ndizo bei pendekezwa. Sasa mleta mada ametoa wito wa wanadarisalama kukutana ili kuweka nguvu katika mjadala na kuweka mapendekezo yao juu ya nauli za mabasi hayo.

Uongo na uchochezi wake ni upi sasa?
 
Katika hili ndugu zangu wana Dar es salaama naomba na kukiri kuitwa mchochezi na nitawajibika binafsi. Naomba waliotayari kuniunga mkono wasiogope, mjitokeze.

UDART, waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo Kasi yatakayoanza kutoa huduma hiyo tarehe 10/01/2016 wamepeleka maombi kwa SUMATRA kuomba iidhinishiwe gharama ya usafiri jijini Dar iwe ni Sh. 1,200/- njia kuu (Morogoro Road) ambayo kimsingi ni kutoka Kimara hadi Posta na Sh. 700/- njia za pembeni ambayo ni kutoka hapo ulipo kwenda ama Posta au Kariakoo.

Mwanafunzi ni nusu nauli ya mtu mzima (Yani wanafunzi watalipa Sh.700 kwa njia kuu na Sh.350 njia za pembeni kutoka Sh.200 wanayolipa kwa sasa). Kama ilivyo ada SUMATRA wameitisha mkutano wa wadau tarehe 05/01/2016 katika ukumbi wa Karimjee Hall saa tatu na nusu asubuhi ili kujadili na kupitisha nauli hiyo.

Ndugu zangu tuna uzoefu wa mikutano hii kutumika kama muhuri maana watu hawaihudhurii, na wakiudhuria basi ni wachache sana. Na hapa ndipo jamaa hutumia mwanya huo kupitisha bei wanazotaka wao. Tumekuwa tukiona EWURA wakiitisha vikao vya wadau ili kupitisha bei za umeme na mafuta. Wadau wanaohudhuria ni wachache na mwisho wa siku ukilalamika unajibiwa "imepitishwa kwa kushirikisha wadau, mbona hukuja kutoa maoni yako?"

La pili ni kwamba bei hizi hupangwa kwa mtego. Mfano hapo UDART wanataka Sh. 1,000/- (njia kuu) na Sh. 500/- (njia za pembeni) sasa wakisema 1200 au 700 wanajua mkilalamika sana mtashuka hadi kwenye bei wanazozitaka, na mtakua mmeingia kwenye mtego wao huo.

Tukumbuke kwamba toka awali tuliambiwa ujio wa mabasi hayo utarahisisha gharama za usafiri mbali uharaka wake.

Kwa sasa daladala zetu hizi mtu akiwa na Sh. 1,000/- anaweza kusafiri safari moja (barabara kuu 500/-) na safari nyingine (400) njia ya pembeni akatumia Sh. 100/- kula karanga.

Ombi langu kwenu: (1) Tarehe 05/01/2016 tujitokeze kwa wingi pale Karimjee Hall kiasi cha ukumbi kutapika. Yeyote anayedhani anaguswa na suala la usafiri Dar asibaki nyumbani. Tuifanye siku hii kuwa Bunge Huru la Dar. Wanafunzi Vyuo vikuu, mama Ntilie, wafanyakazi viwandani, machinga, walimu na wadau wote wa usafiri wa umma tunaomba mjitokeze kwa wingi wenu kuja kupaza sauti.

Tukatae gharama hii ni KUBWA mno wala tusiingie mtego huu. Nauli ya 1200 kwa 700 ni kubwa sana na inamuumiza Mtanzania maskini anayetegemea usafiri wa daladala. Hebu fikiria mama anayekaa Kimara anasafiri kila siku kwenda Soko la Samaki Feri kununua Samaki aje akaange auze apate vijisent vya kuendesha maisha yake na wanae.

Kwa nauli ya sasa anatumia Sh.6000 tu kwa wiki nzima (yani 500/= × 2 × 6). Lakini kwa nauli ya mabus yaendayo kasi atalazimika kutumia Sh.14,400 kwa wiki (yani 1200/= × 2 × 6). Ongezeko la Sh.10,800/= sawa na asilimia 140%. Hili ni ongezeko kubwa sana ambalo watanzania maskini wanaotegemea usafiri wa daladala hawawezi kumudu.

Ni lazima gharama hizi zishuke la sivyo watuachie daladala zetu. Tukiungana kwa umoja wetu tutashinda nguvu ya mabepari wanaotaka kutumia umasikini wetu kutajirika maradufu. Mabasi haya ni mapya, barabara ni mpya hakuna sababu ya kupandusha nauli kwa kiasi hicho. Tusitafsiri kauli ya "kusoma namba" kwa kukandamiza maskini. UVCCM, BAVICHA nk mtusaidie kwa hili bila kujali itikadi zenu.

05/01/2015 tukusanyike kwa wingi pale Karimjee Hall kupinga nauli hizi za kinyonyaji.. Siku hiyo ifanyike kuwa BUNGE HURU la Dar.
Hiyo tarehe si ndio nyumba zianza kuvunjwa au
 
haya bana ila wewe na dingi yako hakikishen mnalipia kodi makontena yote mliyoingiza nchini miaka kumi yote iliyopita. Kenge nyinyi!
Naona unatafuta baasha kwa nguvu mimi siyo zangu hizo dogo jaribu kwa wengine.

Punguani wahed.
 
[QUOTujugalao, post: 15013219, member: 56995"]Kwa nini unaiona sh 700 -1400 ni luxury?kwa vigezo vipi hasa?

Kmimi sijawahi kupanda ndege kwa kuwa uwezo wangu ni wa basi....haimaanishi ndege ni anasa!!
Utakuta asilimia zaidi ya 50 wanaoelekea posta hawana shughuli ya maana zaidi ya kwenda kukwapua tu....kama maisha ya bongo yatawashinda acha warudi kimanzichana,kwa msisi na mamseri!![/QUOTE]
Acha ujinga jinga lao hiyo nauli ni kubwa sana Dada zetu vibarua kwa waindi wnaolipwa mishara midogo wachuuzi wa samaki wa feri mama zetu watapata nini kama mtaji wa elfu kumi utoe hiyo nauli ya hayo mabasi yenu makada wa ccm kwani huu mradi si wa serikali kwa nini serikali isitoe bei ya nauli elekezi yenye maslai kwa wananchi
 
Hiyo mbona ndogo,kwani boda boda unalipa shs. ngapi tena unapigwa na jua,vumbi ama mvua. ipande tu maana hata shs/dollar bado majanga tusije funga biashara bure
Mbona 1200 ni chini hata ya dola moja, watanzania tunataka nn?
 
Wakati mlipokuwa mnakatika viuno huku mkiimba mtaisoma namba mlifikiri ni lowassa na mbowe ndio wangeisoma namba? Pambafu! Kama hela huna panda farasi. Wakati wa kampeni mijinga inakata viuno kama misenge halafu ccm wakifanya yao yanaanza kubwabwaja. Hatuji karimjee ng'o! Mbona tuliwaita kwenye maandamano ya kupinga wizi wa kura hamkutokea.
 
Jana nilileta mada humu juu ya hili suala la nauli sijui iliishia wapi. Ama ilifutwa au haikupata wachangiaji lakini nauli hizi mpya hatazitakuwa na unafuu hata kidogo.

Tiba
 
Tusubiri kulipia tukipita kwenye flyovers wanazotaka kuzijenga
 
Jamani wewe ni jingalao nani huwa anakuruhusu kuchangia mada? Kichwa chako huwa kimejaa makamasi!
Huo ni ukweli binti yangu...iliwahi kuimbwa kama unaona elimu ni ghali jaribu ujinga!
 
Jana nilileta mada humu juu ya hili suala la nauli sijui iliishia wapi. Ama ilifutwa au haikupata wachangiaji lakini nauli hizi mpya hatazitakuwa na unafuu hata kidogo.

Tiba
Mkuu unafuu unaotaka ni upi?unataka ufike kazini kwa kuchelewa?
 
Mkuu unafuu unaotaka ni upi?unataka ufike kazini kwa kuchelewa?
Kwani sasa hivi nafikaje kazini? Hoja yangu hizo nauli Mpya au ziwe saws Na za sasa au zipungue Zaidi, sio kuwa juu ya Zaidi ya hizi zilizopo.

Tiba
 
Kama unaona ni ghali tembea kwa mguu!
Like father like son.
Kauli inafanana na ya 'father' wako ambaye aliwahi kutamka hadharani kuwa mkazi wa Kigamboni ambaye hatakuwa na nauli ya kulipia kwenye panton, itabidi aogelee kwenda ng'ambo kwa kupiga mbizi!
 
Back
Top Bottom