Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,083
- 9,250
Miundombinu bure, magari wameingiza bila kodi, biashara wanpewa monopoly yani wao tu njia nzima, lakini bado wantangaza mihela kibao.
hapa kazi tu
hapa kazi tu
Asilimia 70 ya watanzania wako vijijini wanatembea kms za kutosha tu kutoka kijiji A kwenda B....bado hawajapata barabara na usafiri wa uhakika.
Nyie wa Dar mliojaziwa miradi lukuki ya mawasiliano mnaleta nyodo....I REPEAT ASIYEWEZA KULIPA NA ATEMBEE KWA MGUU !!
Vifurushi vya simu unanunua sh.ngapi na katika watanzania maskini wewe haupo unataka kuingiza watu mkenge na bahati mbaya maskini pia hawapo humu JF ingekuwa poa kama ungetambua hadhira hii ni watu wanamna gani. Kibaya zaidi katika nchi hii ni kutumia watu vibaya. Bei bado haijatangazwa manake kuna bajaj, bodaboda na tax wanapanda. Kibaya zaidi njia hiyo walianza kulipa buku kitambo sana.Katika hili ndugu zangu wana Dar es salaama naomba na kukiri kuitwa mchochezi na nitawajibika binafsi. Naomba waliotayari kuniunga mkono wasiogope, mjitokeze.
UDART, waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo Kasi yatakayoanza kutoa huduma hiyo tarehe 10/01/2016 wamepeleka maombi kwa SUMATRA kuomba iidhinishiwe gharama ya usafiri jijini Dar iwe ni Sh. 1,200/- njia kuu (Morogoro Road) ambayo kimsingi ni kutoka Kimara hadi Posta na Sh. 700/- njia za pembeni ambayo ni kutoka hapo ulipo kwenda ama Posta au Kariakoo.
Mwanafunzi ni nusu nauli ya mtu mzima (Yani wanafunzi watalipa Sh.700 kwa njia kuu na Sh.350 njia za pembeni kutoka Sh.200 wanayolipa kwa sasa). Kama ilivyo ada SUMATRA wameitisha mkutano wa wadau tarehe 05/01/2016 katika ukumbi wa Karimjee Hall saa tatu na nusu asubuhi ili kujadili na kupitisha nauli hiyo.
Ndugu zangu tuna uzoefu wa mikutano hii kutumika kama muhuri maana watu hawaihudhurii, na wakiudhuria basi ni wachache sana. Na hapa ndipo jamaa hutumia mwanya huo kupitisha bei wanazotaka wao. Tumekuwa tukiona EWURA wakiitisha vikao vya wadau ili kupitisha bei za umeme na mafuta. Wadau wanaohudhuria ni wachache na mwisho wa siku ukilalamika unajibiwa "imepitishwa kwa kushirikisha wadau, mbona hukuja kutoa maoni yako?"
La pili ni kwamba bei hizi hupangwa kwa mtego. Mfano hapo UDART wanataka Sh. 1,000/- (njia kuu) na Sh. 500/- (njia za pembeni) sasa wakisema 1200 au 700 wanajua mkilalamika sana mtashuka hadi kwenye bei wanazozitaka, na mtakua mmeingia kwenye mtego wao huo.
Tukumbuke kwamba toka awali tuliambiwa ujio wa mabasi hayo utarahisisha gharama za usafiri mbali uharaka wake.
Kwa sasa daladala zetu hizi mtu akiwa na Sh. 1,000/- anaweza kusafiri safari moja (barabara kuu 500/-) na safari nyingine (400) njia ya pembeni akatumia Sh. 100/- kula karanga.
Ombi langu kwenu: (1) Tarehe 05/01/2016 tujitokeze kwa wingi pale Karimjee Hall kiasi cha ukumbi kutapika. Yeyote anayedhani anaguswa na suala la usafiri Dar asibaki nyumbani. Tuifanye siku hii kuwa Bunge Huru la Dar. Wanafunzi Vyuo vikuu, mama Ntilie, wafanyakazi viwandani, machinga, walimu na wadau wote wa usafiri wa umma tunaomba mjitokeze kwa wingi wenu kuja kupaza sauti.
Tukatae gharama hii ni KUBWA mno wala tusiingie mtego huu. Nauli ya 1200 kwa 700 ni kubwa sana na inamuumiza Mtanzania maskini anayetegemea usafiri wa daladala. Hebu fikiria mama anayekaa Kimara anasafiri kila siku kwenda Soko la Samaki Feri kununua Samaki aje akaange auze apate vijisent vya kuendesha maisha yake na wanae.
Kwa nauli ya sasa anatumia Sh.6000 tu kwa wiki nzima (yani 500/= × 2 × 6). Lakini kwa nauli ya mabus yaendayo kasi atalazimika kutumia Sh.14,400 kwa wiki (yani 1200/= × 2 × 6). Ongezeko la Sh.10,800/= sawa na asilimia 140%. Hili ni ongezeko kubwa sana ambalo watanzania maskini wanaotegemea usafiri wa daladala hawawezi kumudu.
Ni lazima gharama hizi zishuke la sivyo watuachie daladala zetu. Tukiungana kwa umoja wetu tutashinda nguvu ya mabepari wanaotaka kutumia umasikini wetu kutajirika maradufu. Mabasi haya ni mapya, barabara ni mpya hakuna sababu ya kupandusha nauli kwa kiasi hicho. Tusitafsiri kauli ya "kusoma namba" kwa kukandamiza maskini. UVCCM, BAVICHA nk mtusaidie kwa hili bila kujali itikadi zenu.
05/01/2015 tukusanyike kwa wingi pale Karimjee Hall kupinga nauli hizi za kinyonyaji.. Siku hiyo ifanyike kuwa BUNGE HURU la Dar.
utoto mbayaKama unaona ni ghali tembea kwa mguu!

Wewe ni Mburula kweli...huko unapopaongelea mauli za mabasi zikoje?Kumbe unajua kabisa hiyo asilimia 70 ya watanzania wanatembea kwa miguu ilihali rasilimali za taifa zinatafunwa na mchwa wachache ,au kutembea km za kutosha kwa miguu unaona ni sifa kwa dunia hii ya leo ambayo ni lazima ukimbizane na muda ili kuyafikia malengo yako ,angalia life expectancy sasa hivi ,halafu nusu ya maisha yako uwe umetumia kwenye safari huoni kama sio sawa ?? Watu wanaishi kwenye space stations huko ,wanaenda kwenye sayari huko ,kweli sisi tuendelee kukimbizana na hili la barabara au hospital ??? Ccm mmechoka sana mkuu
Naunga mkono hoja kuwa nauli ni kubwa.
Kwa upande mwingine wanaoishi mbezi mwisho wameshazoea hali ya kulipishwa 1000 iwe kutoka mwenge ama posta, mabasi rasmi huyeyuka ikifika saa 1 jioni na hubaki hayo ya 1000.
Naona DART wameona inawezekana, usafiri wa umma wakati wa usiku ni suala la kufatiliwa kwa karibu.
Umburula wangu ni upi Jingalao ??? Hili la nauli ya mabasi/Treni/ndege linafanywa ni swala la luxury na yote hii ni kuwa na sera mbovu zisizo tekelezeka mathalani BRN na wizi tu , ilihali kwa taifa linalopenda watu wake au lenye mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo usafiri sio swala luxury bali ni service tu ya kawaida na kila mwananchi kwa kipato chake anaweza kumudu ,hushangai unapanda ndege kutoka London kwenda Paris kwa pound 40 ila kutoka Dar hadi Arusha kwa precision ni laki mbili na ushee ??Wewe ni Mburula kweli...huko unapopaongelea mauli za mabasi zikoje?
Kwa uzoef nilionao watu wengi hasa wanaojiita 'wananchi wa kawaida' huwa hawahudhurii mikutano hii. Wanangoja bei zitajwe ndo warudi hapa na ID zao feki kulalama
Nimeongelea tatizo la usafiri kwa usiku, naona bendera ya taifa ikishushwa kila mtu anajiamulia la kwake na wananchi ndio wanaoumia.Jiongeze usidhani wt wanaweza hiyo Nauli MTU analizimika kuamka sa,9 usiku kupata Gari ya Nauli 1 ya Serikali sio kwamba hapendi lkn hana sasa Kimbilio la wengi waliochoka nao wakiweka Nauli juu unadhani itakuwaje...
Ongelea nauli za dala dala za huko huko london na paris acha kulialiaUmburula wangu ni upi Jingalao ??? Hili la nauli ya mabasi/Treni/ndege linafanywa ni swala la luxury na yote hii ni kuwa na sera mbovu zisizo tekelezeka mathalani BRN na wizi tu , ilihali kwa taifa linalopenda watu wake au lenye mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo usafiri sio swala luxury bali ni service tu ya kawaida na kila mwananchi kwa kipato chake anaweza kumudu ,hushangai unapanda ndege kutoka London kwenda Paris kwa pound 40 ila kutoka Dar hadi Arusha kwa precision ni laki mbili na ushee ??
Ccm mmechoka mazee