Mgomo na Maandamano Dar, Tarehe 5/01/2016

Mgomo na Maandamano Dar, Tarehe 5/01/2016

Nimeongelea tatizo la usafiri kwa usiku, naona bendera ya taifa ikishushwa kila mtu anajiamulia la kwake na wananchi ndio wanaoumia.
Hatuwezi kuendelea kwa ratiba za 12 asubuhi mpaka 12 jioni, kuna huduma zinahitajika kwa masaa 24. Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha hao watoa huduma nao wana uhakika wa kupata huduma za usafiri.
Ni huduma gani hasa unazoziongelea?hizi za uchuuzi na udalali
 
Ongelea nauli za dala dala za huko huko london na paris acha kulialia
Nlichokiongelea hapo hujakielewa kwamba kwa wenzetu nauli ya treni/bus/ndege ni service ya kawaida tu na sio swala la luxury ??? Sina namna ya kukusaidia tena ,jumapili njema ,
 
Kimsingi nauli ni kubwa, hata ingekuwa 700, bado ni kubwa sana. Inawezekana haya mabasi walengwa .ni maofisa wenye kazi zao huko Posta na hii inaweza kuwa mbinu ya kuhakikisha watu wa hovyo hovyo hawapandi haya mabasi.
 
Mleta mada una matatizo katika kufikiri we umeibiwa mabilion ya tsh siojawahi kuona unahamasisha wanachi waandamane, mamilion hayo ni escrow na mengineyo badala yake ulikaa kimya kana kwamba kilichotendeka nissawa tu,hataivyo mbona mikoani wanalipa zaidi ya hiyo kwa umbali huohuo na ujawahi kuitisha maandamano we jiji kama limekushinda
 
Sioni haja ya kwenda kushiriki hicho kikao. Cha msingi hapa ni kwamba, ikiwa wataweka hiyo bei yao, basi watu wasusie kupanda hizo gari...ila ikiwa kwenye jamii hii hii wapo watu wengi ambao wataridhika na hiyo bei...hapo hatuna namna zaidi ya kuacha tu hiyo nauli inayopendekezwa na SUMATRA.

Uzuri ni kwamba mbadala wa usafiri upo na nauli za daladala nyingine hazijapanda...basi kwa watumiaji wa daladala wao waendelee kutumia hizo daladala za siku zote. Waachane na hizo gari za mradi wa DART hadi hapo wao wenyewe watakapo telemsha nauli.
 
Nlichokiongelea hapo hujakielewa kwamba kwa wenzetu nauli ya treni/bus/ndege ni service ya kawaida tu na sio swala la luxury ??? Sina namna ya kukusaidia tena ,jumapili njema ,
Kwa nini unaiona sh 700 -1400 ni luxury?kwa vigezo vipi hasa?

Kmimi sijawahi kupanda ndege kwa kuwa uwezo wangu ni wa basi....haimaanishi ndege ni anasa!!
Utakuta asilimia zaidi ya 50 wanaoelekea posta hawana shughuli ya maana zaidi ya kwenda kukwapua tu....kama maisha ya bongo yatawashinda acha warudi kimanzichana,kwa msisi na mamseri!!
 
Akili za wana ccm kama asilimia kubwa ya watanzania chakula kwa siku ni chini ya 1.5 dola kwa siku unategemea 1400 isiwe luxury ??, All noted with thanks Jingalao
 
ficha upambavu wako nyumbu wewe
 
elimu bure kwa wanafunzi, CCM ni ile ile, aha ni ile ile ...wapinzani mtaisoma namba
 
huko tuendako ccm wataanza kutoza hewa tunayovuta, time will tell
 
Sisi watu Wa kimara na Mbezi hiyo ni hela ndogo sana Kwetu, kwa sasa tunalipa kila siku elfu 2 kwenda na kurudi kwa usafiri Wa Noah
 
Akili za wana ccm kama asilimia kubwa ya watanzania chakula kwa siku ni chini ya 1.5 dola kwa siku unategemea 1400 isiwe luxury ??, All noted with thanks Jingalao
Unawaongelea watanzania au wakazi wa Dar?
Usihamishe mada tetea kwa data na facts....jiulize wanaotakiwa kwenda huko posta ni kina nani ?au ni watu wa kipato kipi hasa hasa ukizingatia kuwahi ???
 
Katika hili ndugu zangu wana Dar es salaama naomba na kukiri kuitwa mchochezi na nitawajibika binafsi. Naomba waliotayari kuniunga mkono wasiogope, mjitokeze.

UDART, waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo Kasi yatakayoanza kutoa huduma hiyo tarehe 10/01/2016 wamepeleka maombi kwa SUMATRA kuomba iidhinishiwe gharama ya usafiri jijini Dar iwe ni Sh. 1,200/- njia kuu (Morogoro Road) ambayo kimsingi ni kutoka Kimara hadi Posta na Sh. 700/- njia za pembeni ambayo ni kutoka hapo ulipo kwenda ama Posta au Kariakoo.

Mwanafunzi ni nusu nauli ya mtu mzima (Yani wanafunzi watalipa Sh.700 kwa njia kuu na Sh.350 njia za pembeni kutoka Sh.200 wanayolipa kwa sasa). Kama ilivyo ada SUMATRA wameitisha mkutano wa wadau tarehe 05/01/2016 katika ukumbi wa Karimjee Hall saa tatu na nusu asubuhi ili kujadili na kupitisha nauli hiyo.

Ndugu zangu tuna uzoefu wa mikutano hii kutumika kama muhuri maana watu hawaihudhurii, na wakiudhuria basi ni wachache sana. Na hapa ndipo jamaa hutumia mwanya huo kupitisha bei wanazotaka wao. Tumekuwa tukiona EWURA wakiitisha vikao vya wadau ili kupitisha bei za umeme na mafuta. Wadau wanaohudhuria ni wachache na mwisho wa siku ukilalamika unajibiwa "imepitishwa kwa kushirikisha wadau, mbona hukuja kutoa maoni yako?"

La pili ni kwamba bei hizi hupangwa kwa mtego. Mfano hapo UDART wanataka Sh. 1,000/- (njia kuu) na Sh. 500/- (njia za pembeni) sasa wakisema 1200 au 700 wanajua mkilalamika sana mtashuka hadi kwenye bei wanazozitaka, na mtakua mmeingia kwenye mtego wao huo.

Tukumbuke kwamba toka awali tuliambiwa ujio wa mabasi hayo utarahisisha gharama za usafiri mbali uharaka wake.

Kwa sasa daladala zetu hizi mtu akiwa na Sh. 1,000/- anaweza kusafiri safari moja (barabara kuu 500/-) na safari nyingine (400) njia ya pembeni akatumia Sh. 100/- kula karanga.

Ombi langu kwenu: (1) Tarehe 05/01/2016 tujitokeze kwa wingi pale Karimjee Hall kiasi cha ukumbi kutapika. Yeyote anayedhani anaguswa na suala la usafiri Dar asibaki nyumbani. Tuifanye siku hii kuwa Bunge Huru la Dar. Wanafunzi Vyuo vikuu, mama Ntilie, wafanyakazi viwandani, machinga, walimu na wadau wote wa usafiri wa umma tunaomba mjitokeze kwa wingi wenu kuja kupaza sauti.

Tukatae gharama hii ni KUBWA mno wala tusiingie mtego huu. Nauli ya 1200 kwa 700 ni kubwa sana na inamuumiza Mtanzania maskini anayetegemea usafiri wa daladala. Hebu fikiria mama anayekaa Kimara anasafiri kila siku kwenda Soko la Samaki Feri kununua Samaki aje akaange auze apate vijisent vya kuendesha maisha yake na wanae.

Kwa nauli ya sasa anatumia Sh.6000 tu kwa wiki nzima (yani 500/= × 2 × 6). Lakini kwa nauli ya mabus yaendayo kasi atalazimika kutumia Sh.14,400 kwa wiki (yani 1200/= × 2 × 6). Ongezeko la Sh.10,800/= sawa na asilimia 140%. Hili ni ongezeko kubwa sana ambalo watanzania maskini wanaotegemea usafiri wa daladala hawawezi kumudu.

Ni lazima gharama hizi zishuke la sivyo watuachie daladala zetu. Tukiungana kwa umoja wetu tutashinda nguvu ya mabepari wanaotaka kutumia umasikini wetu kutajirika maradufu. Mabasi haya ni mapya, barabara ni mpya hakuna sababu ya kupandusha nauli kwa kiasi hicho. Tusitafsiri kauli ya "kusoma namba" kwa kukandamiza maskini. UVCCM, BAVICHA nk mtusaidie kwa hili bila kujali itikadi zenu.

05/01/2015 tukusanyike kwa wingi pale Karimjee Hall kupinga nauli hizi za kinyonyaji.. Siku hiyo ifanyike kuwa BUNGE HURU la Dar.
 
Unawaongelea watanzania au wakazi wa Dar?
Usihamishe mada tetea kwa data na facts....jiulize wanaotakiwa kwenda huko posta ni kina nani ?au ni watu wa kipato kipi hasa hasa ukizingatia kuwahi ???
Utanichosha bure ,amini unacho amini wacha nibaki na imani /mawazo yangu pia
Ulivyokuja na 70% ya watanzania wanatembea kwa miguu ulimaanisha Dar ??
 
Sisi watu Wa kimara na Mbezi hiyo ni hela ndogo sana Kwetu, kwa sasa tunalipa kila siku elfu 2 kwenda na kurudi kwa usafiri Wa Noah
Kuna watu wanalilia mazuri huku wakisahau gharama!!At times we need stone faces to tell the truth to our community!Tuache ajenda za wanasiasa vilaza.
 
Ni huduma gani hasa unazoziongelea?hizi za uchuuzi na udalali
Mifano
1. Hospitali
2. Mawasiliano (simu)
3. Vituo vya mafuta
4. Zima moto
5. Ulinzi
6. Mabenki
7. Redio

Sijaongelea uzalishaji kwa upande wa viwanda ambavyo ndio vitahitaji zaidi huduma za saa 24.
 
Back
Top Bottom