Mgomo mkubwa wa wenye vituo vya mafuta 2011!

Mgomo mkubwa wa wenye vituo vya mafuta 2011!

leo wengi wa kununua ya buku kumi kumi tutalala kunako barabara
 
HTML:
Hii kasumba yote waliyoileta ni serikali ya CCM, Hawa jamaa ndio kwanjia moja au nyingine wanahaki ya kugoma kutokana na muda wa serikali hii kushusha bei ya mafuta kwa muda wa siku moja tu haiingii akilini! Naomba msininukuu vibaya hata mimi napenda sana mafuta yashuke bei lakini hawa jamaa wenye vituo vya mafuta wakati bajeti ilishapitishwa nao pia walishanunua mafuta kwa bei iliyokuwepo ambayo ni ya juu kulingana na utaratibu wa serikali kushusha bei lazima wenye vituo ile kwao! kwa wazo langu ni kua hawa jamaa wangepewa muda kama wa wiki moja wawe wameuza mafuta kwa bei iliyokua inaendelea and then baada ya muda huo kuisha ndipo waanze kuuza mafuta kwa bei pungufu tuliyoisikia hapo jana! unazani wenye vituo wanapenda kuingia hasara???...!

tunawezaje kujustfy kwamba akiba ya mafuta waliyonayo wamenunua kwa bei ya zamani, kumbuka ni zaidi ya mwezi sasa toka wamepunguziwa hizo tozo, yaani from 1st July. lakini pia mbona bei zikipanda hawasubiri mpaka akiba waliokunayo iishe?
Unadhani hata sisi watumiaji wa hayo mafuta tunapenda hasara?
 
Hata Arusha kuna kamgomo ka wauza mafuta, kuanzia phillips mpaka sakina ni kituo kimoja tu kimefunguliwa Bp karibu na triple A
<br />
<br />
Mkuu! Hata pale Mianzini kwa Bamprass naona wanatoa huduma kama kawa na hata pale Philips naona huduma ni kama kama kawa. Na ni nini hasa chanzo cha kutaka kugoma? Ni bei imeshuka sana?
 
Wenye vituo vya mafuta vyote wamegoma. Kikwete chukua uamuzi mgumu, taifisha vituo vyote viwe mali ya umma. Nyerere alifanya hivyo wakati wa azimio la Arusha.
 
Asiye taka kuuza bei iliyopangwa arudishe leseni na aanze kuuza mafuta ya kupikia. Pia achukue akili za mbayuwayu achanganye na za kwake ,,, eh ndio,,, ndio maana yake. Eh serikali haitamvumilia mfanyabiashara yeyote atakayegoma eh! ha ha ha maana ha haa tueleweke hivyo bwana. Maana nalo hilo ni jambo kubwa tutakaponyamaza sisi kama serikali hatutaeleweka. hata kama ni kura na pesa zao sizihitaji kabisaaaaa.

Serikali ipi? Ni hii iliyoshindwa kudhibiti uchakachuaji hadi kupandisha bei ya mafuta ya taa?
 
hapa tunachezewa akili tu baada ya miezi 3 bei itarudi pale pale na kuzidi kupaa!kwani bei ya kikomo ya juma hili ni Tsh 2004!sasa kila wiki bei muongozo itakuwa inapanda kidogokidogo mapaka pale tutakapofikia ile ya awali na kuipita!


Absolutely right! Kama wametumia hawa EWURA ktk hii system yao ya cap price aah! tumekwishney, tena sio miezi mitatu, just mwezi ujao tu watakuja na hoja ya maharamia wa somalia wamezuia meli so bei imepanda.
 
Mimi sihitaji takwimu zozote,ninachosubilia ni mafuta kushuka bei.waziri alikwisha tangaza na pia ewura wamekutana na haowamiliki wamekubaliana ndiyo maana wamesema watatangaza bei mpya.
Ni waziri gani huyo mkuu? Ni huyu geresha au?
 
Labda mnieleweshe maana sioni hiyo bei iliyoshuka ila naona maneno mengi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. Kwani wameondoa shilingi ngapi???
 
taarifa iliyopo ni kuwa mmiliki yoyote wa kituo cha mafuta atakayegoma atanyan'ganywa leseni yake.. kwa hiyo wana JF msiwe na wasi wasi.. kwani wao mara ngapi tumepandishiwa bei ya mafuta lakini hatukugoma kununua? taarifa kutoka ewura .. atakayegoma leseni yake inachukulia full stop

Na wewe unakubali kuwa wanayoyasema ni kweli?? hao wenye vituo vya mafuta ndio hao hao sasa wanamdanganya nani??? Shame on them
 
duh! wapi tunakwenda sasa jamani wana jf wenzangu kila mahali mgomo.
 
Hana ubavu huo kwani wamiliki ni mafisadi amabo magamba yameshindikana kung'oka wakishirikiana na waarabu wachache ambao wanatuibia hata mwezi wa Ramadhan
 
Wenye vituo vya mafuta vyote wamegoma. Kikwete chukua uamuzi mgumu, taifisha vituo vyote viwe mali ya umma. Nyerere alifanya hivyo wakati wa azimio la Arusha.
Akili hiyo hana, akifanya hivyo atapata wapi mafuta ya kwenda Marekani kuangalia mechi ya Ngasa na MAN U. Maamuzi magumu aliyoyafanya kwenye kipindi chake cha utawala hadi leo hii ni pale alipowaambia viongozi wa DINI WANAKULA MSUBA NA AMEWAKAMATA.
 
Nchi haiendeshwi hivyo. Ni biashara hulia hata wakiamua kufunga ni juu yao.
 
Back
Top Bottom