kama wakitaka kugoma wagome tu watajikuta ni wachache wanaogoma halafu wengine watatumia huo mwanya kuuza then utakuta wanaanza malumbano wenyewe kwa wenyewe.. watanzania bwana sijui ni lini tutakua na ule umoja wa kweli kuamua kukataa jambo.. tatizo letu tunakua tunapelekwa na uoga.. kama tungesimama kuanzia siku nyingi sana kutetea hali ya mafuta na uchumi wa nchi yetu unapoendelea,, wala tusingekua na wafanya biashara wasio na huruma kama hawa jamaa wa mafuta...! ila tumewaachia mpaka sasa tunalia wenyewe
na kama hatutakuja kuangalia mambo mengine ya msingi bado tutaendelea kulia na kuumia hivihivi kisa tunaendekeza woga.. ! ninajaribu kufanya uchunguzi wa kuhusu bei ya mafuta kwenye nchi kama za Rwanda na burundi ili nijue... nimesikia huko kunaunafuu wa bei ya mafuta wakati wanachukulia kwenye bandari yetu hapa..! ila tuwe waangalifu sana laasivyo mambo mengine yanayohusu maisha yetu ya kila siku yatakuja kua msumari mkali sana kwenye miili yetu kama hatutakkua waangalifu na kusimama na kukataa mapema
kumbuka,,,,,,"usipoziba ufa utajenga ukuta",,,,,