MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

Safi sana,hawa watoto wanaburuzwa na Chadema, wacha wasage lami mitaani tuone kama CDM watawasaidia.ikishindikana warudi vijijini kwao wakalime.MASKINI CHADEMA IMEWAPONZA.
 
Saa hizi serikali ndo imekuwa "haina utaratibu wa kukaa meza moja na wadau mbalimbali?!!
Nyie watu kwa kugeuza maneno, hivi ni serikali ndiyo ilikataa kuongea na madaktari pale Karimjee siyo?

Wee naona ndio wale wale wa magamba mnaoendelea kuzisikiliza na kuamini ngojera za Serikali DHAIFU, "Serikali haina uwezo"...Hakuna hata neno moja lililobadilishwa. Madaktari wamegoma mara tatu sasa na mara zote Serikali imeshindwa kutimiza madai mbali mbali ya Madaktari ikiwemo kuboresha sekta ya afya nchini kwa kisingizio "serikali haina uwezo" wakati nci yetu ina utajiri wa hali juu. Ila inapokuja kwenye matanuzi ya Serikali DHAIFU siku zote huwa na uwezo wa kutanua.

[h=1]Masikini serikali! (Mwanahalisi)[/h]
e6faaa817268d28347d2eecce1d2e5dc.jpg

Na editor - Imechapwa 04 July 2012

Maoni ya Mhariri

SERIKALI imefunga milango na madirisha. Haitaki tena majadiliano na madaktari juu ya mazingira ya kazi na ujira.
Hii inakuja baada ya mgomo wa madaktari na utekaji na utesaji kinyama wa Dk. Steven Ulimboka, mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania.
Ni kama Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa asiyekubaliana naye amejifukuza kazi. Tishio kali!
Lakini ndani ya gazeti hili, daktari mmoja amenukuliwa akisema, “…wakati mwingine ninamwangalia mgonjwa, nina uwezo wa kumwokoa, lakini hakuna vifaa. Anakufa mbele yangu.”
Huo ni upande mwingine ambao serikali haijaangalia. Yenyewe imekazania kusema “…madaktari wanataka posho! Posho! Posho!”
Daktari anayenukuliwa anaona bila vifaa, hospitali yake ni kituo cha mwisho; mahali pa kusubiria kifo. Serikali haitaki kusikia hilo. Sasa serikali imeona, kwa vitendo kuwa ingekuwa na vifaa, Dk. Ulimboka asingepelekwa Nairobi na, au Afrika Kusini.
Serikali inaona kila siku, kwamba kama kungekuwa na vifaa, viongozi wake wasingekuwa wanapiga foleni kwenda kutibiwa nje. Kinachokosekana si maarifa, bali zana na mazingira bora ya kazi. Serikali haitaki kusikia.
Sasa serikali inasema italeta madaktari kutoka nje ya nchi. Kwamba tayari imetenga Sh. 200 bilioni kuwagharamia.
Serikali imefanya lini makubaliano na madaktari hao? Hizo fedha serikali imezitoa wapi kulipa watu wa nje? Maandiko matakatifu yaliishaonya: Usichukue chakula cha watoto na kumpa mbwa!
Je, madaktari wa nje watakuja na vifaa? Kama hawatakuwa na vifaa si watakuwa wanafanya utalii tu wa kujifunza lugha au kufanya tafiti za kuendeleza utaalam wao?
Tunatangaziwa haraka kuwa baadhi ya madaktari wamekubali kurejea kazini. Hivi serikali inaamini wanakwenda kufanya kazi kwa moyo uleule?
Serikali yoyote ikifunga milango ya mawasiliano, hata kwa njia ya migomo; inakuwa imeziba mifereji ya fikra na matumaini ya muwafaka. Yanakuwa maisha ya kuvimbiana.
Tunaitaka serikali kufanya mambo yafuatayo: Kwanza, iunde tume huru ya kuchunguza waliomtendea unyama Dk. Ulimboka. Pili, iwasikilize madaktari. Tatu, ituhakikishie kuwa italinda uhai wetu na mali zetu.

Hivi kuwafukuza ama kuwafutia leseni mainterns doctors ndio kumaliza mgogoro uliopo baina ya serikali na madoctor?
What if madaktari wengine (registars and residents) nao wakiamua kugoma ili kulinda na kutetea haki za wanataaluma wenzao??
Hapa serikali imeshemsha vibaya, kwakuwa madaktari walikuwa wamesitisha mgomo na kurudi kuendelea na kazi, hatua hii itakwenda kuibua mgogoro upya.
 
BARAZA la Madaktari Tanganyika limewafutia usajili madaktari wote waliokuwa katika mafunzo ya vitendo (Internship), baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mgomo wakiwa kazini.Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa Dar es Salaam jana imeeleza kuwa madaktari 319 wamepoteza sifa ya kuendelea na taaluma hiyo hivyo usajili wao umesitishwa rasmi kuanzia jana.Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk Donan Mmbando amewataka madaktari hao kurudisha hati zao za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari.

“Kwa kuzingatia masharti ya sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhia kwamba madaktari wote ambao walijihusisha na mgomo, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012.”

“Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya terehe 17 Julai, 2012.”

Dk Mmbando alisema, awali Baraza hilo lilipokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba baadhi ya madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kati ya Juni 23 na Juni 29 mwaka huu.

Alisema madaktari hao walipangiwa kutoa huduma katika Hospitali za Muhimbili, KCMC, Rufaa Mbeya, Sekou Toure na Bugando za Mwanza, Amana, Temeke na Mwananyamala za Dar es Salaam, Haydom - Arusha, St Francis-Ifakara na Dodoma.

Alisema kutokana na mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo huo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Dk Mmbando alisema kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa kwenye Baraza hilo, Msajili wa Baraza, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la kufanya Uchunguzi dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Alisema baada ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo, Baraza limebaini kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda.
 
Safi sana, imekula kwao. Wameingizwa kichwakichwa na magwanda. Haya sasa, kila mtu afe na lwake, hakuna wa kuwatetea...si Mbowe, Lema, Slaa au Mnyika. Wao wanaendelea kupeta na posho zao wakati maskini ma dr uchwara wameachwa juani solemba.
 
Mimi nilitegemea uwahurumie walalahoi wenzio manake kiukweli ndio ambao wanateseka mpaka sasa hivi.....madaktari inawahusu nini?......kilaza wewe!
 
Mimi nilitegemea uwahurumie walalahoi wenzio manake kiukweli ndio ambao wanateseka mpaka sasa hivi.....madaktari inawahusu nini?......kilaza wewe!

Wewe pia ni kilaza. Badala ya kuwahurumia ma-dr limbukeni wazembe wachumia tumbo ambao sasa kimenuka kwao, unaleta unafiki wa kuwahurumia walalahoi ambo hao ma-dr wamewaua bila sababu. Huna hoja, kama wewe ni dr uliyegoma, pole, imekula kwako.
 
Hapo kwenye nyekundu sijui kama unajua unachoandika......wameshasema hawahusiki na hawaungi mkono hilo jambo sasa ulisanganye watu hapa...na wewe mtoa mada jambo hili limejadiliwa tangu jana usiku ..MODS UNGANISHENI....
 
Mimi nilitegemea uwahurumie walalahoi wenzio manake kiukweli ndio ambao wanateseka mpaka sasa hivi.....madaktari inawahusu nini?......kilaza wewe!

Imekula kwa madaktari muda wao wote wamefanya kazi ya bure, kwani kwa sasa inabidi waanze upya shule, ni huruma sana kwao ila ni funzo next time wawe waangalifu na wanasiasa uchwara wa cdm

Imekula kwa madaktari muda wao wote wamefanya kazi ya bure, kwani kwa sasa inabidi waanze upya shule, ni huruma sana kwao ila ni funzo next time wawe waangalifu na wanasiasa uchwara wa cdm

Sinaga mda wa kubishana na vilaza kama wewe!.....haya nenda kamwambie nape ushapost jf akupatie ujira wako.....nakuona hata ulivyoandika hapa unaonekana una njaa yaani hujakula toka asubuhi!

Imekula kwa ndugu zako na wewe mwenyewe pia .....unadhani hao ccm waliokutuma kuja kupost huku wanatibiwa tanzania kama wewe?
 
Wewe pia ni kilaza. Badala ya kuwahurumia ma-dr limbukeni wazembe wachumia tumbo ambao sasa kimenuka kwao, unaleta unafiki wa kuwahurumia walalahoi ambo hao ma-dr wamewaua bila sababu. Huna hoja, kama wewe ni dr uliyegoma, pole, imekula kwako.

Taratibu basi mbona watokwa jasho hivyo???? pili pili usiyoila yakuwashia nini ndugu ??????.....subiri hao madaktari waje kwako kuomba ugali afu ndio utajua kama imekula kwao au kwako......kilaza wewe.....kibaraka mchumia tumbo ni wewe mwanaume mzima unaelipwa elfu mbili na Nape!.......afu wewe ndie limbukeni na mzembe manake huna hata maarifa ya kujitafutia riziki mpaka utumiwe na chama cha mabwepande!
 
Inanikumbusha juu ya Hayati Professa Msuya aliyewahi kuwa Chief Academic Officer wa UDSM. Huyu bwana historia yake ni kwamba aliwahi kusoma Muhimbili Medical School kusomea MD, wakamkong'oli ati kabeba bichwa tu ka Zero.

Akajiondokea zake Uganda akasoma Makerere BSc na akasonga mbele hadi kupata PhD, akarudishwa Muhimbili Medical School kufundisha madaktari kwenye somo matata sana la BIOCHEMISTRY.

Akawafunza adabu kwamba alikuwa anajua sayansi ya binadamu na angeweza kuzalisha madaktari, akazalisha madaktari kadhaa.

Sasa unamfukuza daktari hapa kwako wakati hobby yako ni kuruka majuu kutibiwa mafua. Fikiria unaenda South Africa unakutana na Bingwa ambaye ndiye yule uliyemsemea mbofumbofu na kumtimua kwa kuwa anakuomba kitu kidogo umwongesee maana anategemewa sana. Atakutibu kwa kanuni za kiganga na viapo vyake.

Lakini akiamua kukuingiza darasani kwamba umekuwa mpuuziana kusomesha watu na kutimua kwa faida ya siasa zako, akajitambulisha kwamba angekuua kama angetaka maana umemfuata alikojificha ili kukukimbia wewe mbaya wake, lakini kwamba amekuacha hai akupime bichwa lako limebeba tope au ubongo, unafanyaje?

Of course utachekacheka kinafiki ukiugulia moyoni, sidhani utarudi tena hapo kutibiwa, labda kwa kutumia mbinu zilezile za kukenua meno na porojo kedekede kwamba "unajua tena siasa bwana...."
 
We must have a clause in our new constitution whereby Presidents will be accountable/prosecuted for the actions and decisions they made while in office which were detrimental to the interests of the nation.
 
Wee naona ndio wale wale wa magamba mnaoendelea kuzisikiliza na kuamini ngojera za Serikali DHAIFU, "Serikali haina uwezo"...Hakuna hata neno moja lililobadilishwa. Madaktari wamegoma mara tatu sasa na mara zote Serikali imeshindwa kutimiza madai mbali mbali ya Madaktari ikiwemo kuboresha sekta ya afya nchini kwa kisingizio "serikali haina uwezo" wakati nci yetu ina utajiri wa hali juu. Ila inapokuja kwenye matanuzi ya Serikali DHAIFU siku zote huwa na uwezo wa kutanua.

Masikini serikali! (Mwanahalisi)

e6faaa817268d28347d2eecce1d2e5dc.jpg

Na editor - Imechapwa 04 July 2012

Maoni ya Mhariri

SERIKALI imefunga milango na madirisha. Haitaki tena majadiliano na madaktari juu ya mazingira ya kazi na ujira.
Hii inakuja baada ya mgomo wa madaktari na utekaji na utesaji kinyama wa Dk. Steven Ulimboka, mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania.
Ni kama Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa asiyekubaliana naye amejifukuza kazi. Tishio kali!
Lakini ndani ya gazeti hili, daktari mmoja amenukuliwa akisema, "…wakati mwingine ninamwangalia mgonjwa, nina uwezo wa kumwokoa, lakini hakuna vifaa. Anakufa mbele yangu."
Huo ni upande mwingine ambao serikali haijaangalia. Yenyewe imekazania kusema "…madaktari wanataka posho! Posho! Posho!"
Daktari anayenukuliwa anaona bila vifaa, hospitali yake ni kituo cha mwisho; mahali pa kusubiria kifo. Serikali haitaki kusikia hilo. Sasa serikali imeona, kwa vitendo kuwa ingekuwa na vifaa, Dk. Ulimboka asingepelekwa Nairobi na, au Afrika Kusini.
Serikali inaona kila siku, kwamba kama kungekuwa na vifaa, viongozi wake wasingekuwa wanapiga foleni kwenda kutibiwa nje. Kinachokosekana si maarifa, bali zana na mazingira bora ya kazi. Serikali haitaki kusikia.
Sasa serikali inasema italeta madaktari kutoka nje ya nchi. Kwamba tayari imetenga Sh. 200 bilioni kuwagharamia.
Serikali imefanya lini makubaliano na madaktari hao? Hizo fedha serikali imezitoa wapi kulipa watu wa nje? Maandiko matakatifu yaliishaonya: Usichukue chakula cha watoto na kumpa mbwa!
Je, madaktari wa nje watakuja na vifaa? Kama hawatakuwa na vifaa si watakuwa wanafanya utalii tu wa kujifunza lugha au kufanya tafiti za kuendeleza utaalam wao?
Tunatangaziwa haraka kuwa baadhi ya madaktari wamekubali kurejea kazini. Hivi serikali inaamini wanakwenda kufanya kazi kwa moyo uleule?
Serikali yoyote ikifunga milango ya mawasiliano, hata kwa njia ya migomo; inakuwa imeziba mifereji ya fikra na matumaini ya muwafaka. Yanakuwa maisha ya kuvimbiana.
Tunaitaka serikali kufanya mambo yafuatayo: Kwanza, iunde tume huru ya kuchunguza waliomtendea unyama Dk. Ulimboka. Pili, iwasikilize madaktari. Tatu, ituhakikishie kuwa italinda uhai wetu na mali zetu.

Umesema sana mkuu, lakini usisahau kwamba wanawaleta madaktari kutoka nje kwa tija well calculated kwa upande wao, hawaleti bora madaktari. Na hao madaktari watakaa wakiwaangalia wanavyokufa watanzania wenye vichwa vilivyojaa tikiti maji, maana ndio haohao wanaoishabikia serikali yao inapoboronga, hatimae watalii hao watawazalisha dada zetu na kuondoka zao wakituachia sanasana ukimwi.
 
TAARIFA RASMI KUTOKA BARAZA LA MADAKTARI:Madaktari Waliokuwa Kwenye Mgomo na Ambao Kwa Sasa Wameondolewa Katika Hospitali Walizokuwa Wakifanya Mafunzo Kwa Vitendo,Wamepoteza Sifa za Kupata Usajili wa Muda (Provisional Registration).

haki.JPG

Baraza la Madaktari Tanganyika limepokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba, baadhi ya Madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship),waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kati ya tarehe 23 na 29 mwezi Juni 2012. Madaktari hao walipangiwa kutoa huduma kwa wagonjwa katika hospitali za Muhimbili, K.C.M.C, Rufaa Mbeya, Bugando, Amana, Temeke,St. Francis- Ifakara, Mwananyamala, Sekou Toure, Haydom na Dodoma. Kufuatia mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii aliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la Madaktari Tanganyika kwamba, Madaktari waliogoma walikataa kutoa huduma za kitaalamu, ikiwa ni wajibu wao, na kwamba kitendo hicho kilihatarisha maisha ya wagonjwa katika hospitali husika na pia ni kinyume na maadili ya taaluma ya udaktari.
Kufuatia malalamiko hayo, Msajili wa Baraza la Madaktari Tanganyika, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la Kufanya Uchunguzi (Preliminary Examination) dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baraza la Madaktari Tanganyika limebaini kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, Madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda (Provisional Registration).
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhika kwamba madaktari wote ambao majina yao yameorodheshwa katika Taarifa hii, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo, usajili waoumesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012.Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajiliwa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya tarehe 17 Julai, 2012.

Dkt Donan Mmbando
MWENYEKITI- BARAZA LA MADAKTARITANGANYIKA
11 Julai, 2012.

4.jpg
5996140674267894691-7596869519964286945
 
Dumela Mbegu acha upuuzi wamefutiwa usajili wa muda na sio wa kudumu. Mna macho ya kusoma lakini hamuoni
 
Jamaa anataka kudhihirisha yeye si DHAIFU kama wengi mnavyodhani ni mwendo wa mwaga mboga nimwage ugali mpaka kuche.
 
Back
Top Bottom