MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MGOMO: Madaktari 319 wafutiwa leseni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kadu, Jul 11, 2012.

 1. Kadu

  Kadu Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]MGOMO:Madaktari 319 wafutiwa leseni[/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Waandishi Wetu
  BARAZA la Madaktari Tanganyika limewafutia usajili madaktari wote waliokuwa katika mafunzo ya vitendo (Internship), baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mgomo wakiwa kazini.Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa Dar es Salaam jana imeeleza kuwa madaktari 319 wamepoteza sifa ya kuendelea na taaluma hiyo hivyo usajili wao umesitishwa rasmi kuanzia jana.Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk Donan Mmbando amewataka madaktari hao kurudisha hati zao za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari.

  "Kwa kuzingatia masharti ya sheria kuhusu kupata usajili wa muda, Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhia kwamba madaktari wote ambao walijihusisha na mgomo, wamepoteza sifa na kwa sababu hiyo usajili wao umesitishwa kuanzia tarehe 11 Julai, 2012."

  "Madaktari wote wanaohusika wanatakiwa kurejesha hati za usajili wa muda kwenye Ofisi ya Msajili wa Madaktari kabla ya terehe 17 Julai, 2012."

  Dk Mmbando alisema, awali Baraza hilo lilipokea malalamiko kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwamba baadhi ya madaktari waliopata usajili wa muda ili kuwawezesha kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship), waligoma kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kati ya Juni 23 na Juni 29 mwaka huu.

  Alisema madaktari hao walipangiwa kutoa huduma katika Hospitali za Muhimbili, KCMC, Rufaa Mbeya, Sekou Toure na Bugando za Mwanza, Amana, Temeke na Mwananyamala za Dar es Salaam, Haydom - Arusha, St Francis-Ifakara na Dodoma.

  Alisema kutokana na mgomo huo, uongozi wa hospitali husika uliwaandikia barua iliyomtaka kila daktari aliyeshiriki kwenye mgomo huo kuripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Dk Mmbando alisema kutokana na malalamiko yaliyowasilishwa kwenye Baraza hilo, Msajili wa Baraza, alimwandikia kila daktari aliyelalamikiwa Taarifa ya Kusudio la kufanya Uchunguzi dhidi yake, juu ya malalamiko yaliyowasilishwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

  Alisema baada ya kuyafanyia kazi malalamiko hayo, Baraza limebaini kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madaktari, Sura ya 152, madaktari waliokuwa kwenye mgomo na ambao kwa sasa wameondolewa katika hospitali walizokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo, wamepoteza sifa za kupata usajili wa muda.

  Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (MAT), Dk Edwin Chitage alisema alikuwa hajapata rasmi taarifa hizo licha ya kusikia fununu... "Sijapata taarifa rasmi lakini ni jambo tulilolitarajia na hatutashangaa tukisikia hilo kwa sasa subiri nithibitishe halafu nitatoa msimamo wetu."
  Kiongozi wa madaktari kortini

  Katika hatua nyingine, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kudharau amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi ya kuwataka kusitisha mgomo kupitia vyombo vya habari.

  Amri hiyo ilitolewa Juni 22, mwaka huu na Jaji Sekela Moshi na kuwataka madaktari kurejea kazini mara moja, lakini amri hiyo haikutekelezwa.

  Jana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka alimsomea Dk Mkopi hati ya mashtaka na kumweleza Hakimu Faisal Kahamba kuwa kati ya Juni 26 na 28, mwaka huu, Dk Mkopi akiwa Rais wa MAT, alidharau amri iliyotolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi Juni 26, mwaka huu ikimtaka kutoa tangazo kwa wanachama wa chama hicho kupitia vyombo vya habari kwamba wasishiriki katika mgomo.

  Kweka alidai kuwa Juni 27, mwaka huu Dk Mkopi aliwashawishi wanachama kushiriki kufanya mgomo kitu ambacho ni kinyume na amri iliyotolewa Juni 26, mwaka huu.

  Hata hivyo, Dk Mkopi alikana mashtaka hayo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kiongozi huyo wa madaktari yupo nje kwa dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 8, mwaka huu itakapotajwa na kuangaliwa kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.

  Afya ya Dk Ulimboka
  Wakati huo huo, afya ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka imezidi kuimarika.
  Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitage alisema jana kwamba: "Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, kwa sasa afya yake imezidi kuimarika, anakula mwenyewe lakini pia anazungumza mwenyewe na rafiki zake wa hapa nchini kwa njia ya simu."

  Katika siku za karibuni, hali ya Dk Ulimboka ilielezwa kubadilika ghafla na kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) kutokana matatizo mbalimbali, yaliyotokana na kupigwa ikiwamo figo kushindwa kufanya kazi.

  Alisafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi Juni 28, mwaka huu kwa ushauri uliotolewa na jopo la madaktari lililokuwa likimhudumia.

  UN yanena
  Katika hatua nyingine, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Dk Alberic Kacou amepokea barua ya MAT kuomba ulinzi kwa Dk Ulimboka anayeendelea na matibabu Afrika Kusini kwa madai kuna kikosi kilichotumwa kuhakikisha harudi nchini akiwa hai.

  Akizungumza jana Dar es Salaam jana, Dk Kacou alisema suala hilo la kutoa ulinzi watalitoa baada ya kuwasiliana na wote waliohusishwa kwenye waraka wa ombi hilo.

  Mgomo wamalizika
  Mgomo uliokuwa ukiendelea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Mifupa (Moi), Dar es Salaam umemalizika na huduma katika hospitali hizo zimerejea kama kawaida jana.

  Waandishi wa habari waliotembelea hospitali hizo waliona wagonjwa wakiwa wanaendelea kupokewa na kupatiwa huduma kama ilivyokuwa awali, kabla ya mgomo uliodumu kwa takriban majuma mawili yaliyopita
  Habari hii imeandikwa na Tausi Mbowe, Tausi Ally, Leon Bahati na Issa Lazaro, Geofrey Nyang'oro
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Source: gazeti la mwananchi
   
 2. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Sio wa kwanza ama Mara ya kwanza kufutwa.....suluhu halishi inabidi ianzie kwenye chanzo cha matatizo sio kwenye matawi na kutishana.
  Kuna waliofukuzwa mwanzoni mwa miaka ya 2000 sass wanapeta na maisha mazuri na mazingira mazuri ya kazi kwingineko! Kumbuka kila mmoja apende asipende lazima augue tu, na biashara ya hospital itavuma kwingineko. Tisa kumi ni pale madaktari wa Jeshi watakaposema sasa basi.
   
 3. Mbutunanga

  Mbutunanga Senior Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  They have just made 319 Ulimbokaz, sijui wanakumbuka!!
   
 4. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  kosa jingine...
   
 5. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  hawawezi wakafanya suluhu kwa mtindo huu
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Ubabe wa serikali utawaumiza zaidi wananchi wanaotegemea hospitali za serikali, siyo hawa madaktari waliofutiwa leseni kwani bado wana ubongo wao. Leseni ni karatasi tu, kulifuta hakuondoi knowledge ambayo madaktari hawa wameshajisheenza vichwani mwao. Time will tell!! Miaka kadhaa iliyopita, Mwinyi mdogo aliwafukuza madakatri Tanzania kutokana na mgomo kama huu; baada ya muda kidogo nikakutana na dakatri mmoja aliyefukuzwa Tanzania akiwa anaendelea na taaluma yake huko Trinidadi tena kwa heshima kubwa sana.

  Kwa vile viongozi wetu wamejijengea tabia ya kwenda kutibiwa nje ya nchi hata mafua tu; hawaoni kabisa umuhimu wa kuendeleza sekta ya tiba nchini. Kufungwa kwa hospitali ya Dr. masau kulitokana na waziri kutaka masau ashirikiane na hospitali moja huko india ambako serikali ilikuwa inapeleka wagonjwa wa moyo. kulikuwa na kila suspicion kuwa waziri mhusika alikuwa na faida kutokana na wagonjwa wa kitanzania kupelekwa katika hospitali hiyo ya india; in other words, kuwapo kwa hospitali inayotoa huduma nzuri tanzania kwao ni kuwakoseasha ulaji. After all hata wanapokwenda kufanyiwa check-up ya mafua wanalipwa per diem kama kawaida; an added advantage.

  Wwakati waziri mkuu wa kenya alipougua, alilazwa Hospitalini Nairobi, lakini kwetu kiongozi akiugua, ni lazima apelekwa nje ya nchi. Mzee mandekla hutibiwa Afrika ya kusini pale pale, je sisi tutakomboka lini iwapo viongozi tulio nao ndio hao?.

  Ningekuwa daktari mimi, kila mtu kwenye meza yangu angepata aspriri hata kama ana ugonjwa wa moyo hadi pale watu wote watakapoamka na kuiondoa serikali hii madarakani kwa kura nyingi. Kura chache hazitishi kwa vile watachakachua. watu hao hao wakishatibiwa wanasimama upande wa serikali kuwalaani madaktari.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,418
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Ndio matatizo ya kuwa na Kiongozi DHAIFU na Serikali DHAIFU siku zote haina utaratibu wa kukaa meza moja na wadau mbali mbali ili kutafuta suluhisho la matatizo husika kwa amani wao wanaona ubabe tu wa kutishana na kukomoana ndiyo njia muafaka. Wangekuwa wanatibiwa nchini sidhani kama wangefikia uamuzi wa hovyo kama huu.
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sijui akili za mbayuwayu alizosema akichanganya na zake ndiyo mwisho wa panel ya urais ilipofikia katika kusuluhisha hili!!!!!
   
 9. Taz

  Taz JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 305
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  No they didn't! This is what I call shooting yourself in the foot. Yaani katika hali kama hii ambapo madaktari wanalalamika mshahara wameona suluhisho ni kuwafuta kazi kabisa?
   
 10. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #10
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,610
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Kila siku nasema CCM kumejaa vichwa maji na Serikali yake, yaani madaktari wanaddai haki yao then wanakuja kufutiwa leseni zakoo, hatari kwa kweli na 2015 sio mbali......
   
 11. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani uamuzi wa kuwafutia lesseni ni hasara kwa serikali yenyewe, imetumia muda na gharama kuwasomesha,bado tunaupungufu mkubwa wa madaktari na hilo pengo la madaktari 319 pengo lao ki-uhalisia haliwezi kuzibika kwa muda mfupi. Ndiyo tunasema wapo 700 wanaomaliza mwezi ujao lakini bado uwepo wao ulikuwa hauwaondowi hao 319 kazini bali ilikuwa inapunguza uhaba mkubwa wa madaktari Tanzania.

  Ni vyema uamuzi huu ukaangaliwa kwa njia pana zaidi ili kuepuka maamuzi ya kukomoana, mgomo umeisha wapewe onyo la waruhusiwe kuendelea na kazi. Katika hali ya kawaida ni kwa vile tu hana tabia ya kufanya tathmini ya maamuzi yetu, kufukuza madk 319 kunaathiri pia uchumi wa nchi kwa namna moja au nyingine.
   
 12. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #12
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  interns huwa hawana liseni... serikali sasa iache ujinga wa kuhadaa kwani wananchi watajua inawahadaa na chuki itaongezeka

  leseni yua practice hutolewa baada ya dr kumaliza intern na kufanya kazi miaka miwili na kuendelea na kupata approval

  THIS IS ANOTHER CHEAP LIE TO PEOPLE
   
 13. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #13
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kichuguu acha ujinga wa gwanda kutetea mgomo wananchi waendelee kuteseka magwanda yanawaza ikulu2 lakingi hayaangalii maisha ya watanzania ebo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Ujinga ni pamoja na kukubali kuonewa halafu ukanyamaza; iwapo wewe unataka madaktari waonewe halafu wakae kimya basi utakuwa ni mmoja wa wajinga wakubwa. Usalama wa raia katika hospitali za serikali uko mikononi mwa serikali siyo mikononi mwa madaktari; wao ni wafanyakazi tu. Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa ina madakatari watakaofanya kazi vizuri kwa kujituma, siyo kwa kusukumwa. Kama wewe ukiwa siyo mjinga, ni dhahiri kuwa hutapenda madakatari warudi kazini ilihali hawaridhiki; ila kwa wajinga wa aina yako, mnadhani kuwa kuwalazimisha kurudi kazini ndiyo jibu. Ukiwa na bahati utatibiwa kwa asprini na maji, na ukiwa na bahati mbaya utapewa dawa ambayo ita-react na mwili wako na kukupeleka pabaya. Swala la tiba siyo swala la kujadili kijinga kijinga kama akili yako inavyokutuma; ni jambo linalohitaji akili na busara kubwa sana. Tatizo serikali yetu imekuwa imekuwa inaongozwa na watu wajinga wa aina yako ambao hawana hata miligramu moja ya ubongo.
   
 15. JOHNSON

  JOHNSON Member

  #15
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 20, 2008
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kijana angalia shibe ya leo njaa ya kesho, lazima kuangalia pande zote za shilingi, tatizo vijana mda wote siasa tu. yangu macho.
   
 16. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #16
  Jul 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,163
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  Ok replacement iko wapi? Au anawafukuzatu kwa hasira zake?, asidhani kuwa ni kama kubadili baraza la mawaziri.
   
 17. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,796
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  Medical council has acted unfairly. Mimi nilidhani hili baraza ni similar to institituion of Engineers ambayo inasajili wahandisi and as such should not be playing politics(revoking en mass usajili wa interns wote is suspect). Which begs the question is medical council a goverment body or a proffesional body?
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Kuwafutia leseni ina maana kuwa hawaruhusiwi ku-practice medicine Tanzania; ila bado wanaweza kwenda nchi nyingine inayotambua medical degrees za MUHS na kufanya kazi chini ya daktari mwingine kwa muda fulani kabla ya kuanza kufanya kazi zao independently. Sisi wananchi tusioweza kwenda kutibiwa na kufanyiwa check-up nje ya nchi ndio loosers zaidi kwenye sakata hili.
   
 19. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  Visasi ubabe sijui vitatufikisha wap,kufukuza hao interns na kumpeleka dr Mkopi mahakamani sio suluhisho la mgogoro ktk sekta ya afya,serikali iache kutafuta njia ya mkato ktk ufumbuzi wa serious problems which are affecting our country,halafu mimi hua najiuliza ni nan huwa wanamshauri huyu mtawala wetu?manake maamuzi mengine ni km vile ametoka usingizini.
   
 20. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Unganisha huu mtandao kwa makini:
  Mkiti wa baraza la madaktari Tz ni dr. Donan Mmbando,
  Acting Chief Medical Officer (CMO) ni dr Donan Mmbando
  Mkurugenzi wa idara ya Kinga ni dr Donan Mmbando

  halafu, Kama CMO ndiye aliye draft barua ya Wizara kuwashitaki interns kwa baraza, na ndiye aliyefanya uamuzi wa kuwafutia leseni kama Mkiti aw baraza

  Pia, kiprotokali ni dr Donan Mmbando ndiye huipatia ikulu pamoja na waziri wa afya majibu ya maswali yanayohusu mgomo. Kwa maneno mengine ukiona serikali ikitoa kauli yoyote kuhusu mgomo, hiyo kauli imeandaliwa na dr Donan Mbando

  Dr Donan Mmbando kama CMO ndiye anayetakiwa kuhakikisha upungufu wa madaktari Tz unakwisha
   
Loading...