ushirika wa vyama vya upinzani nchini umeitaka serikali kuunda tume huru kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tuhuma za ufisadi zilizotolewa na ushirika huo hivi karibuni, vinginevyo vitatangaza mgogoro wa kitaifa. Kutokana na kiburi na kutojali kwa serikali kuhusu tuhuma zinazoikabili, kuanzia mwezi November mwaka huu tutatangaza migomo nchi nzima hadi hapo ufumbuzi wa juu ya tuhuma za ufisadi alisema mwenyekiti wa TLP bwana Augustine Mrema. bwana Mrema alitangaza msimamo huu kwa niaba ya vyama vya upinzani vyenye ushirikiano. Wametaka tume hiyo ishirikishe wataalam, wandishi wa habari, viongozi wa dini, wanasheria ana wananchi wa kawaida. Aidha wamemtaka JK kuitisha mkutano kongamano la kitaifa kujadili kile wanachodai mwelekeo na ufisadi unaofanywa nchini na watu wachache wa kujilimbikizia mali. Vile vile wamesambaza barua kwa mabalozi ambao nchi zao wachangia asilimia 40 ya bajeti wakiwataka wasimsikilize bwana Membe kuwa hiyo ni propaganda ya kutaka kuwanyamazisha.