Mgomo kupinga mafisadi wanukia nukia

Lawson

Member
Sep 25, 2007
69
4
ushirika wa vyama vya upinzani nchini umeitaka serikali kuunda tume huru kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tuhuma za ufisadi zilizotolewa na ushirika huo hivi karibuni, vinginevyo vitatangaza mgogoro wa kitaifa. Kutokana na kiburi na kutojali kwa serikali kuhusu tuhuma zinazoikabili, kuanzia mwezi November mwaka huu tutatangaza migomo nchi nzima hadi hapo ufumbuzi wa juu ya tuhuma za ufisadi alisema mwenyekiti wa TLP bwana Augustine Mrema. bwana Mrema alitangaza msimamo huu kwa niaba ya vyama vya upinzani vyenye ushirikiano. Wametaka tume hiyo ishirikishe wataalam, wandishi wa habari, viongozi wa dini, wanasheria ana wananchi wa kawaida. Aidha wamemtaka JK kuitisha mkutano kongamano la kitaifa kujadili kile wanachodai mwelekeo na ufisadi unaofanywa nchini na watu wachache wa kujilimbikizia mali. Vile vile wamesambaza barua kwa mabalozi ambao nchi zao wachangia asilimia 40 ya bajeti wakiwataka wasimsikilize bwana Membe kuwa hiyo ni propaganda ya kutaka kuwanyamazisha.
 
ushirika wa vyama vya upinzani nchini umeitaka serikali kuunda tume huru kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tuhuma za ufisadi zilizotolewa na ushirika huo hivi karibuni, vinginevyo vitatangaza mgogoro wa kitaifa. Kutokana na kiburi na kutojali kwa serikali kuhusu tuhuma zinazoikabili, kuanzia mwezi November mwaka huu tutatangaza migomo nchi nzima hadi hapo ufumbuzi wa juu ya tuhuma za ufisadi alisema mwenyekiti wa TLP bwana Augustine Mrema.

Badala ya kuishinikiza serikali kama vyama vya upinzani, watumie nguvu ya wananchi kuishinikiza serikali.
 
Hii vita ikipiganwa kutoka ndani ya Tanzania haitakuwa na mafanikio, kwa sababu kuna kundi la watanzania wanaonufaika na ufisadi huo na wanaweza kufanya kila wanaloweza kuvuruga vita hiyo. External approach ni nzuri zaidi, ni kuwatumia mabalozi, donor community, WB, IMF za zaidi, ndani Tanzania tunadanganyana, it will not go nowhere.
 
Hii vita ikipiganwa kutoka ndani ya Tanzania haitakuwa na mafanikio, kwa sababu kuna kundi la watanzania wanaonufaika na ufisadi huo na wanaweza kufanya kila wanaloweza kuvuruga vita hiyo. External approach ni nzuri zaidi, ni kuwatumia mabalozi, donor community, WB, IMF za zaidi, ndani Tanzania tunadanganyana, it will not go nowhere.


Hii presure inatakiwa itoke kwa watanzania wenyewe ambao ndio wanaumizwa na ufisadi. Then mambo ya kichachamaa kam kule Burma international comunities watatoa kauli zao. Watanzania ndio wanao umia, wenzetu si ajabu wananufaika na ufisadi mfano makampuni ya madini yamekuwa listed kwenye stock exchange kwa nchi zao na zote zinachangia pato la taifa kwao. Uingereza walipata soko kwa kuuza rader kwa Tanzania. Mabadiliko yanatakiwa yaanzie humu ndani na dalili ilishaanza kuonekana. kitendi cha kuomewa mawaziri ni Moshi unaofuka ipo siku moto utawaka na jumuiya ya kimataifa watayasikia yanayoendelea.

Ukijaribu kusoma taarifa za Bank ya dunia kuhusu tanzania utashangaa sifa wanazozitoa labda sisi hatuzioni ila naamini ni kwa sababu Tanzania ni wateja wao na wananufaika nao.
 
Ukijaribu kusoma taarifa za Bank ya dunia kuhusu tanzania utashangaa sifa wanazozitoa labda sisi hatuzioni ila naamini ni kwa sababu Tanzania ni wateja wao na wananufaika nao.

Unajua tatizo ni kuwa ripoti zinazopelekwa huko IMF na WB zinatoka kwa serikali, kama tukizipeleka sisi wenyewe waTz nadhani wanaweza kuona ukweli halisi. Siku zote serikali inataka kujipaka rangi nzuri. Hata hao wafanya kazi wa WB na IMF walioko TAnzania wanakula nao, kwa hiyo ni vizuri kuanzia juu hukohuko kwao.
Lakini hata hivyo una point kuwa pressure ya nyumbani tusiache, the two can work well
 
Hapa wapinzani wanataka kufanya jambo ambalo halitawaongezea ila litawapunguzia. Hapa ndipo wanapohitaji real political strategists, sasa wawashinikize serikali na watu waandamane n.k ili kiwe nini? Ni chama gani kati ya hivyo vinne chenye uwezo wa kuunda serikali endapo serikali itaanguka (collapse)? Kuna jambo ambalo wanaweza kulifanya ambalo litaonesha kiini cha mgogoro huu.. lakini hilo la kutaka kuamsha hisia za kuishinikiza serikali kwa maandamano.. kunanirudisha kwenye swali langu la siku kadhaa za huko nyuma... "Mko tayari"?

Wakicheza vibaya karata walizonazo, CCM itajipatia ujiko mwingine wa bure..!!!
 
Hapa wapinzani wanataka kufanya jambo ambalo halitawaongezea ila litawapunguzia. Hapa ndipo wanapohitaji real political strategists, sasa wawashinikize serikali na watu waandamane n.k ili kiwe nini? Ni chama gani kati ya hivyo vinne chenye uwezo wa kuunda serikali endapo serikali itaanguka (collapse)? Kuna jambo ambalo wanaweza kulifanya ambalo litaonesha kiini cha mgogoro huu.. lakini hilo la kutaka kuamsha hisia za kuishinikiza serikali kwa maandamano.. kunanirudisha kwenye swali langu la siku kadhaa za huko nyuma... "Mko tayari"?

Wakicheza vibaya karata walizonazo, CCM itajipatia ujiko mwingine wa bure..!!!

Nadhani kama ni kuandamana sio kwa nia ya kuiangusha serikali bali ni kutaka serikali iunde tume huru ya kuchuza ufisadi ambayo naamini kwa tanzania haiwezi kuwa huru kwa mantiki ya huru. Pia nadhani kama ni maadamano ni ya kuifanya serikali iwawajibishe wanaotuhumiwa kwa ufisadi mf kuwasimamisha watuhumiwa kwenye nafasi zao wakati uchunguzi unaendelea tukiangalia mfano wa BOT uchunguzi unafanyika na wakati mthumiwa ni mkuu wa benki na bado yupo madarakani.


Pia maandamano hayo yasiyokuwa na nia ya kuiangusha serikali wala kufanya vurugu (kuvuruga amani) yanaweza kucreate more political awareness kwa wananchi ambao ndio wataamua ni serikali gani iwe madarakani kupitia uchaguzi huru. Nadhani hata kama sio kuunda serikali vyama vya upinzani vitaget kuingiza wabunge wengi bungeni ili kubalance power kwenye chombo hcho muhimu cha maamuzi na si kulenga uraisi. Ni ukweli ulio wazi kuwa kwa hali ya vyama vya upinzani havinauwezo wakuunda serikali kwa sasa lakini sasa hivi ni kujijenga kwanza.
 
Unajua tatizo ni kuwa ripoti zinazopelekwa huko IMF na WB zinatoka kwa serikali,

ni kweli mkuu unaweza kusoma hata hili tangazo linalojitokeza hapo JF juu kabisa la world bank {TANZANIA: Moving Forward)]na kweli kwa nnje Tanzania wanasifa nzuri sana na wakati mwingine wanachukuliwa kama mfano wa kuigwa lakini in real sense sio.
 
YNIM, sasa wakiandamana, halafu serikali isiwachukulie hatua (isijichukulie hatua) na tume huru haitaundwa then what?
 
YNIM, sasa wakiandamana, halafu serikali isiwachukulie hatua (isijichukulie hatua) na tume huru haitaundwa then what?

Itakuwa kama ile petition ya Msola ajiuzulu na hajajiuzulu (jocking). Ila ni kama utamaduni wa serikali kupuuza so hili halitakuwa geni sana lakini walau meseji itakuwa sent.
 
Yeah! Strikes zinakubalika kimataifa coz ni njia mojawapo ya kudai haki kidemokrasia.Tanzania sasa inabidi tufikie mahali tudai haki zetu kwa uchungu.Tumedai kwa kutabasamu imeshindikana! sasa tudai kwa uchungu.Let us switch on PEOPLE'S POWER
 
Naungana na wazo la upinzani la kuitisha maandamano/ mgomo wa kitaifa. Nakuhakikishia mpaka sasa bado ccm wanadhani wanadhalilishwa tu na wapinzani na wanaamini wangetakiwa kuchukuliwa hatua kali! Mgomo wa umma ndio ungetoa picha halisi ya jinsi wananchi wanavyochukia mambo yao. Kama ccm wasingekuwa na kiburi wasingethubutu kwenda mikoani kabla hawajachukua hatua dhidi ya tuhuma hizo. Ninadhani walienda kupima joto la kisiasa lilivyo, kutokana na ufisadi wao na sasa ilitakiwa joto liongezeka zaidi.
 
Nakubaliana na kuandaa political tension, ila muda ni mfupi sana walioutoa haswa ukizingatia kuwa ni lazima jamii iwe imeandaliwa vya kutosha na kujua nini haswa kinawafanya wao walazimeke kuandamana.

Zichukuliwe hatua za haraka kwenye kuuandaa umma ili waelewe kuwa ni sababu zipi zimewafikisha hapo waliipo na umasikini wao.
 
YNIM, sasa wakiandamana, halafu serikali isiwachukulie hatua (isijichukulie hatua) na tume huru haitaundwa then what?

Na je, kama sasa hivi wapinzani watakaa tu kimya bila kufanyq chochote, then what?

Nakumbuka hata kuna watu walipinga sana hoja ya kutaja majina ya mafisadi kabla hajatajwa wakitoa hoja kam hii, kwamba je, wasipochukuliwa hatua itakuwaje, lakini sote nafikiri tumeona impact ya kutaja yale majina katika siasa zetu. I believe every political actity that awakens people has merit and should be supported. We know these guys will never do anything by a way of demonstration and so if we just kept quite or wrote several articles on papers, but at least we know that people will know their woes better and be ready to take action come 2010.
 
Ninachofikiria ambacho wanaweza kufanya will put more pressure than maandamano... Siamini katika "kufofanya kitu" naamini katika "kufanya kitu chenye matokeo siyo kufanya kitu kama alama tu".. tumekuwa na alama nyingi sana zisizoelekeza kokote!
 
Mie nakubaliana na wazo la kufanya haya maandamano nchi nzima yakiambatana na mgomo pia wa nchi nzima. Nadhani wapinzani wanapata consultation toka kwa stategists wazuri ambao wametumia reception ya mawaaziri wa CCM huko mikoani kuweza kuplan this next move. Kwa vile wananchi wameonekana kuchukia ujio wa makada wa CCM na ujumbe wao, then the best move ni kuendeleza pressure i.e. confront the beast baada ya initial provocation (kutaja list of shame). Hii itahakikisha serikali inaendelea kuwa on its toes na wakati huo huo ita-galvanise wananchi to support wapinzani.
 
Dawa ni kutumia wananchi na TECHNOLOGIA kuwaondoa hawa mafisadi na wala rushwa wanaoofilisi nchi kwa KASI MPYA, NGUVU MPYA, UFISADI UPYA. Kwa kutumia email na simu za mkononi, dawa ni yao ni KU-TEXT "MGOMO NCHI NZIMA, JANUARY 1, 2008" wao wenyewe wataonja joto ya jiwe. Kuanzia leo message zangu zitakuwa "MGOMO NCHI NZIMA, JANUARY 1, 2008." Tumechoka na huu ufisadi wakati sisi wananchi wa kawaida hata kwenda chuo kikuu hatuwezi.

Next time text "MGOMO" kwa mshikaji au ndugu, mpaka kieleweke na hela za wananchi zirudi.

"MGOMO"
 
Back
Top Bottom