Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,092
My take:
Huu mgogoro usipotafutiwa ufumbuzi wa hekima utaleta impression mbaya sana katika jamii.
Vijana wa Kiislamu na Wafanyakazi waislamu wachache waliobakishwa pale UDOM baada ya wenzao kuhamishwa watakuwa na grievances na dhana mbaya sana juu ya uongozi wa chuo na serikali na hivyo kuzalisha watu wenye hisia za kutilia mashaka mifumo ya nchi hii.
Kibaya zaidi ile dhana ya Mfumo Kristo kwamba ndo unatawala nchi hii inaweza kupata legitimacy katika fikra za wasomi hawa wa Kiislamu.
Kama wasomi watatoka katika vyuo huku wakiamini kuwa kweli kiba mfumo Kristo katika nchi hii basi ni hatari sana huko mbeleni maana kikawaida tulitegemea Taifa lingewatumia hawa wasomi kuelewesha wenzao kuwa hiki kitu hakipo.
Kwa Tanzania Taasisi ya Ponda ni Taasisi inayosikilizwa sana na waislamu nchini na Sheikh Ponda ni kiongozi wa Waislamu mwenye kuheshimiwa sana na Waislamu na hili tamko litasambaa nchinini katika misikiti yote na kuleta impact pengine isiyotakiwa katika nchi yetu.
Ni muhimu kwa serikali kupitia Waziri wa Elimu mama Ndalichako kuingilia kati na kulitatua suala hili maana Linagusa hisia za Waislamu nchini.
Suala hili lilikuwa raised hata mbele ya mheshimiwa rais alipoongea na viongozi wa dini majuzi
Hekima kubwa inahitajika katika suala hili.