Maghrib Moja Msikiti wa Mwembechai Nyuma ya Sheikh Ponda 1998

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
MAGHRIB MOJA MSIKITI WA MWEMBECHAI NYUMA YA SHEIKH PONDA 1998

Mwaka ni 1998 niko ndani ya basi la Raha Leo natokea Tanga.
Karibu Maghrib inaingia basi linakaribia Msikiti wa Mwembechai.

Msikiti huu ulivamiwa na askari wakakata umeme wakaingia ndani na kupiga mabomu ya machozi na baadhi ya Waislam waliokuwa ndani ya msikiti wakakamatwa na kupigwa.

Umma mzima wa Waislam ulikuwa katika huzuni.

Nikaamua nishuke hapo Mwembechai angalau nisali Maghrib hapo na kwa kitendo hiki changu iwe kama vile nimefika hapo msikitini kuwahani ndugu zangu na kutoa pole.

Msikiti wa Mwembechai ulikuwa umefikwa na makubwa.

Waislam mitaani wakawa wanauliza, "Wako wapi BAKWATA na viongozi wa Waislam?"

Nimeingia msikitini kusali.
Msikiti umejaa.

Yaliyowafika Waislam hayakuwavunja nguvu.
Yale yakawa kama vile ni kichocheo kwao kumwelekea Allah zaidi.

Msikiti umejaa pomoni.
Niko safu za nyuma wala Imam simuoni.

Kutoka safu niliyokuwa nimesimama naisikia sauti ya Sheikh Ponda amepiga takbira ya kuhirimia na mimi nakijua kiraa chake.

Mashaallah utapenda kumsikiliza Ponda akisoma Qur'an.

Kachagua sura mnasaba na hali iliyokuwa inawakabili Waislam wa Tanzania wakati ule.

Allah anazungumza na Waislam wanaosimama bega kwa bega kuipigania dini yake kwa nafsi zao na mali zao...

Maneno ya Allah ya kuwatia moyo Waislam na jinsi Sheikh Ponda alivyokuwa anaisoma Qur'an kwa taratibu na upole nasikia baadhi ya maamuma wanalia ndani ya sala, machozi yanawatoka.

Maneno ya Allah yamefika panapotakiwa.

Naondoka Msikiti wa Mwembechai baada ya sala ya Maghrib fikra nyingi zinanipitikia.

"Wako wapi viongozi wa Waislam?"

Waislam wanauliza hadi ifikie watu kupigwa ndani ya misikiti na isiwe lolote?

Kile kitendo cha umma wa Waislam kusali nyuma ya Sheikh Ponda wakaisikiza Qur'an ndali ya sala na kumsujudia Allah nyuma yake na yakawabubujika machozi kwangu mimi ile ilikuwa bishara tosha.

Nilihisi Sheikh Ponda In Shaa Allah atawaongoza Waislam kwa mengi.

Toka siku ile Sheikh Ponda amesimama na Waislam katika kila lililowafika na Waislam wamemkubali kama kiongozi wao.

Sheikh Ponda hakusimama kusema, ''Nichagueni.''
Sheikh Ponda Mashaallah kajaaliwa kalamu.

Kaandika kitabu, "Juhudi na Changamoto."

Katika kitabu hiki Sheikh Ponda ameeleza tatizo la udini linalokabili Tanzania, tatizo ambalo serikali inaliogopa kukubali kuwa lipo na waathirika ni Waislam.

Serikali inajua hatari ya dhulma lakini wanaamini tatizo hili litajiondoa lenyewe.

Hofu ya kutaka tatizo litambulike fikra hii linatisha serikali yenyewe kwani athari yake itafika mbali sana iwapo itakubalika kuwa lipo tatizo na linahitaji ufumbuzi.

Kupitia matukio tofauti na kupitia maisha yake mwenyewe Sheikh Ponda, msomaji atasoma na kuiona kwa ushahidi dhulma iloyojijenga dhidi ya Waislam nchini bila kificho toka uhuru wa Tanganyika upatikane mwaka wa 1961.

Katika kitabu hiki, ''Juhudi na Changamoto,'' Sheikh Ponda anamchukua msomaji kutoka tatizo moja hadi lingine kwa ushahidi wa nyaraka na picha.

Sheikh Ponda hakika kaifanyia nchi yetu hisani kubwa kwa kuandika kitabu hiki.

1699814454441.jpeg

1699814508523.jpeg

1699814545321.jpeg

1699814580003.jpeg
 
Sheikh Ponda ni Ibilis mkubwa anataka kuifanya Tanzania Somalia nyingine.Hajui Tanzania idadi ya wakristo (76%)ni kubwa ukilinganisha na idadi ya waislam.
 
Sheikh Ponda ni Ibilis mkubwa anataka kuifanya Tanzania Somalia nyingine.Hajui Tanzania idadi ya wakristo (76%)ni kubwa ukilinganisha na idadi ya waislam.
Utakuwa hujaelewa movement zake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom