Mgogoro wa Waislam UDOM waingia hatua mpya: Sheikh Ponda atoa tamko zito

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,251
2,000

My take:

Huu mgogoro usipotafutiwa ufumbuzi wa hekima utaleta impression mbaya sana katika jamii.

Vijana wa Kiislamu na Wafanyakazi waislamu wachache waliobakishwa pale UDOM baada ya wenzao kuhamishwa watakuwa na grievances na dhana mbaya sana juu ya uongozi wa chuo na serikali na hivyo kuzalisha watu wenye hisia za kutilia mashaka mifumo ya nchi hii.

Kibaya zaidi ile dhana ya Mfumo Kristo kwamba ndo unatawala nchi hii inaweza kupata legitimacy katika fikra za wasomi hawa wa Kiislamu.

Kama wasomi watatoka katika vyuo huku wakiamini kuwa kweli kiba mfumo Kristo katika nchi hii basi ni hatari sana huko mbeleni maana kikawaida tulitegemea Taifa lingewatumia hawa wasomi kuelewesha wenzao kuwa hiki kitu hakipo.

Kwa Tanzania Taasisi ya Ponda ni Taasisi inayosikilizwa sana na waislamu nchini na Sheikh Ponda ni kiongozi wa Waislamu mwenye kuheshimiwa sana na Waislamu na hili tamko litasambaa nchinini katika misikiti yote na kuleta impact pengine isiyotakiwa katika nchi yetu.

Ni muhimu kwa serikali kupitia Waziri wa Elimu mama Ndalichako kuingilia kati na kulitatua suala hili maana Linagusa hisia za Waislamu nchini.

Suala hili lilikuwa raised hata mbele ya mheshimiwa rais alipoongea na viongozi wa dini majuzi

Hekima kubwa inahitajika katika suala hili.
 
the_forum

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
749
1,000
Mmeamua kutokusoma wala kutopeleka watoto wenu shule,mnawapeleka madrasa! Haya ndo matokeo wachache wanakidhi vigezo hasa kutumika ktk ngazi za juu za kielimu...

Acheni udini,huu uzi tu ni udini tosha! Nendeni shule acheni kushauriana mambo yasiyo na tija.

Kama wamehamishwa,huko walipoenda si wapige kazi tatzo nini? Au kuna mkate gani walikua wanapata walipokua UDOM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha chuki, kebehi na dharau mkuu, sisi sote ni Watanzania, angalia impact ya mustakbali wa Taifa letu, mshikamano wa kitaifa n.k!
Kuhamisha Waislamu watupu katika chuo kilichojaa watu wa imani zote kunapelekea dhana ya udini!
 
gambagumu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
959
1,000
Aache kuingilia taasisi za serikali kwa mgongo wa dini, kila uongozi kwenye kila taasisi ina namna yake ya kushughulikia changamoto, kama walihamishwa walishindwa kutimiza wajibu wao wa msingi na kuanza kujenga misikiti ni vyema sana wamehamishwa, maana hao ni chanzo cha mafarakano, halafu woliajiriwa na taasisi z serikali wameajiriwa kwa mujibu wa sifa walizo nazo na sio dini.
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,251
2,000
AACHE KUINGILIA TAASISI ZA SERIKALI KWA MGONGO WA DINI, KILA UONGOZI KWENYE KILA TAASISI INA NAMNA YAKE YA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO, KAMA WALIHAMISHWA WALISHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAO WA MSINGI NA KUANZA KUJENGA MISIKITI NI VYEMA SANA WAMEHAMISHWA, MAANA HAO NI CHANZO CHA MAFARAKANO, HALAFU WOLIAJIRIWA NA TAASISI Z SERIKALI WAMEAJIRIWA KWA MUJIBU WA SIFA WALIZO NAZO NA SIO DINI.
Uhamisho wao unaonyesha kuna dhana ya "dini" zao kuwa sababu ya uhamisho wao!.
Haiwezekani ukahamisha watu 11 halafu 100% ya hao uliowahamisha wakawa wa dini moja then ukaja kusema kuwa hakuna kitu behind!

Utakuwa unadanganya!
 
TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,473
2,000
Elimu, Elimu, Elimu.
Kuwa na mawazo ya kukandamizwa kutokana na dini ni upungufu wa akilina mawazo yaliyo pevuka.

Yaani mpaka karne hii bado mpo binadamu mnaolia kukandamizwa kwa sababu ya dini?.

Hivi ukisoma elimu dunia kwa undani na elimu ya huko kwengine ipi yenye faida mujarabu?.
 
Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,546
2,000
Mmeamua kutokusoma wala kutopeleka watoto wenu shule,mnawapeleka madrasa! Haya ndo matokeo wachache wanakidhi vigezo hasa kutumika ktk ngazi za juu za kielimu...

Acheni udini,huu uzi tu ni udini tosha! Nendeni shule acheni kushauriana mambo yasiyo na tija.

Kama wamehamishwa,huko walipoenda si wapige kazi tatzo nini? Au kuna mkate gani walikua wanapata walipokua UDOM?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii imepitwa na wakati waislamu mbona wanasomesha watoto shule mkuu haya yalikua madai miaka 10 baada Uhuru kama kuna tatizo la msingi litatuliwe kabla ya kuleta madhara
 
msani

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
1,739
2,000
Hili tatizo tulililea wenyewe hasa kwa kuanzia kwa mkuu wa chuo kipindi hicho. Tulisikia tetesi za udini kutawala chuo na shughuli za dini kushika hatamu hadi kwenye uongozi na ajira. Lilikuwa ni bomu lililotengenezwa na kiongozi aisye na uadilifu na sasa likaota mizizi ndio litatusumbua. Lakini jumuiya ile ni kubwa tukiruhusu kila dini wajenge jengo lao la kuabudu hapatatosha pale itakuwa ni fujo. Wanaotaka kuabudu waende nje ya chuo la sivyo waendelee na ule utaratibu wa kutumia madarasa kufanya ibada zao ambapo sio permanent.
 
digalangosha

JF-Expert Member
Aug 30, 2013
1,427
2,000
Acha maneno ya dharau dhidi ya Waislamu, sote ni Watanzania, Haki inabidi itendeke kwa makundi yote ya kijamii kwa ajili ya kutunza amani ya nchi
Sasa udom wamefata misikiti au kusoma.....? Mbona wakiwa kwenye maofisi ya umma hawalilii misikiti...??

Mie nipo halmashauri moja hapa sijaona waislam wakililia msikiti,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,251
2,000
Hili tatizo tulililea wenyewe hasa kwa kuanzia kwa mkuu wa chuo kipindi hicho. Tulisikia tetesi za udini kutawala chuo na shughuli za dini kushika hatamu hadi kwenye uongozi na ajira. Lilikuwa ni bomu lililotengenezwa na kiongozi aisye na uadilifu na sasa likaota mizizi ndio litatusumbua. Lakini jumuiya ile ni kubwa tukiruhusu kila dini wajenge jengo lao la kuabudu hapatatosha pale itakuwa ni fujo. Wanaotaka kuabudu waende nje ya chuo la sivyo waendelee na ule utaratibu wa kutumia madarasa kufanya ibada zao ambapo sio permanent.
Watumishi wa Kikiristo ni wengi kuliko Waislamu hapo UDOM toka zama za uongozi wa awali , kwa hiyo kudai kulikuwa na upendeleo wa ajira kwa waislamu ni UONGO WA MCHANA!.

Labda kama una maanisha kuwa Waislamu wasipate nafasi kabisa ya utumishi katika Taasisi za umma hapo ndo uone kuwa imekaa sawa!
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,251
2,000
Basi wakubali kusali kwenye madarasa....!

Sent using Jamii Forums mobile app
Madarasa kazi yake ni kusomea.Kutaka kuyafanya yawe ni nyumba za ibada ni kwenda kinyume na malengo ya ujenzi wake!

Cha msingi ni kufuata plan ya awali tu, kuwa maeneo yaliyotengwa katika ramani kwa ajili ya kujenga msikiti na kanisa basi vijengwe mahali pake!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom