Mgogoro wa Waislam UDOM waingia hatua mpya: Sheikh Ponda atoa tamko zito

Mimi nadhani serikali kwa kuwa haina dini isiruhusu chuo chochote wala taasisi ya uma kuwa na kanisa wala msikiti ikiwa mtu anataka kusali atajua tu namna yakuongea na Mungu wake, nadhani muumini mzuri ni yule anayeweza kumtafuta mola wake katika mazingira yoyote yale hawezi kukwamishwa na mazingira. Mfano ikiwa mtu atajua kama chuo fulani hakina kanisa au mskiti basi atachugua vyuo vya duni ambavyo nadhani vipo vingi tu ila ukichagua chuo cha umma ukubali masharti utakayo yakuta mule.

Hatuwezi kila siku tukawa tunadai kujenga nyumba za ibada kwenye maeneo ya uma sasa kila dhehebu hata lenye mtu mmoja likidai chuo si kitageuka kuwa eneo la kuabudia na kuna wengine hawana dini hivyo itakuwa ni kama tunawasumbua kwa kwa sala zetu ambazo kwao ni kama kelele. Watanzania wote ni sawa tusijione wengine tuna haki zaidi kuliko wengine hata kama ni wachache.
 
My take:

Huu mgogoro usipotafutiwa ufumbuzi wa hekima utaleta impression mbaya sana katika jamii.

Vijana wa Kiislamu na Wafanyakazi waislamu wachache waliobakishwa pale UDOM baada ya wenzao kuhamishwa watakuwa na grievances na dhana mbaya sana juu ya uongozi wa chuo na serikali na hivyo kuzalisha watu wenye hisia za kutilia mashaka mifumo ya nchi hii.

Kibaya zaidi ile dhana ya Mfumo Kristo kwamba ndo unatawala nchi hii inaweza kupata legitimacy katika fikra za wasomi hawa wa Kiislamu.

Kama wasomi watatoka katika vyuo huku wakiamini kuwa kweli kiba mfumo Kristo katika nchi hii basi ni hatari sana huko mbeleni maana kikawaida tulitegemea Taifa lingewatumia hawa wasomi kuelewesha wenzao kuwa hiki kitu hakipo.

Kwa Tanzania Taasisi ya Ponda ni Taasisi inayosikilizwa sana na waislamu nchini na Sheikh Ponda ni kiongozi wa Waislamu mwenye kuheshimiwa sana na Waislamu na hili tamko litasambaa nchinini katika misikiti yote na kuleta impact pengine isiyotakiwa katika nchi yetu.

Ni muhimu kwa serikali kupitia Waziri wa Elimu mama Ndalichako kuingilia kati na kulitatua suala hili maana Linagusa hisia za Waislamu nchini.

Suala hili lilikuwa raised hata mbele ya mheshimiwa rais alipoongea na viongozi wa dini majuzi

Hekima kubwa inahitajika katika suala hili.

My friend hata wakristu walipoondolewa ktk taasisi za umma hasa nssf hilo halikuonekana inakuja kwa waislamu ndo unaonekana wanabaguliwa.
Wacha dawa iwaingie vilivyo.
ingawa hii kitu huko mbeleni tutachinjana tusipokuwa makini maana kina ponda, dau, kikula,mlacha wana nguvu na ni kati ya wanazuoni wa kiislamu waanzilishi wa ubaguzi ktk taasisi za umma.
 
Hiyo ramani ilikosewa tu. Madawati huwa hayajai darasa zima kule mbele ya darasa huwa kunasalia nafasi kubwa. Au basi mnaweza kuswalia nje kwenye mti, Mungu popote tu yupo.

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app

Eti ramani imekosewa, kichekesho hiki.

Kuswali nje pia inawezekana, lakini kuna changamoto ya Jua kali kwa sala ya mchana na pia nyakati za mvua.

Kuhusu madawati kutokujaa madarasani, hiyo siyo kweli sana lakini fahamu tu Swala ya kiislamu huelekea direction maalum waislamu huiita Kibla, lazima sehemu ya kusalia iweze kuwa na space ya kutosha katika muelekeo huo.

Kwa hiyo kwa kuwa madarasa hayakujengwa kwa kufuata Kibla na hitajio la ibada ya kiislamu, basi ni muhimu waislamu wakajenga nyumba yao ya kuabudia yenye kuzingatia requirements hizi.

Tatu iwapo waislamu au wakiristo wataanza mahubiri yao katika darasa wanalosalia wanaweza kudisturb wanafunzi wengine wanaojisomea katika madarasa ya pembeni.

Nne, misikuti ya waislamu huwa na sehemu maalum ya kuwekea udhu, Madarasa hayana sehemu hizo!

Tano Msikitini watu huenda kusoma Qur'ani na kufanya meditation za kiislamu muda wowote ule hususan kipindi cha mwezi wa Ramadhani, hilo haliwezekaniki madarasani maana yana kazi nyingine

Kwa hiyo umuhimu wa nyumba za ibada bado uko palepale
 
Mkuu kama una imani kali hivyo basi nakushauri uwe unaenda nje ya chuo misikiti imejaa, kwamba ipo mbali siyo sababu kama una imani kali, pia angalia vyuo vya kiisilamu ukasome huko, chuo ni mahala pa kupata elimu Dunia zaidi na serikali haina dini, wala vyuo haviamini haya mambo ya Dini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni makosa yalifanyika. Hata udom kusipokuwepo na msikiti bado hakutaathiri utoaji wa elimu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Yangekuwa ni makosa kujenga msikiti na kanisa UDSM basi vingekuwa vimeshavunjwa!.
Ila nikujulishe tu kuwa hata mheshimiwa rais alifunga ndoa yake kwenye kanisa la chuo kikuu cha DSM!.
Na pia maprofesa, madokta na wasomi husali katika nyumba hizo, sidhani kama wewe una akili kuwazidi wote hao hata wasijue kuwa yalikuwa ni makosa kujenga nyumba hizo za ibada na hata serikali isizivunje mpaka leo hii!
 
Back
Top Bottom