Mgeni kukuacha na madeni kisa ukarimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgeni kukuacha na madeni kisa ukarimu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Billie, Mar 21, 2012.

 1. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Kuna tabia nimeikumbuka wakati naishi nyumbani kwetu(kwa baba na mama).Ilikuwa akija mgeni mama anafanya juu chini apate pesa ya kununua hata mapaja ya kuku na ikiwezekana pilau linapikwa siku hiyo na sisi watoto tunabaki tunakula ugali maharage mgeni anarundikiwa vinono kwa kweli roho ilikuwa inaniuma sana hili swala sema udogo ndio ulininyima kauli.KWA SASA NIPO KIGETOGETO ILA NIKIWA NA MJI WANGU MAALUMU HII TABIA NI MARUFUKU mwendo ni kugawana utachokikuta na huwezi kuniingiza kwenye madeni kisa we mgeni.NYIE MNALIONAJE HILI?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  100 percent co-signed!
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaha! Jamani,..
   
 4. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Siku hizi kuna ugeni? akijua zipo abanduki, kashachungulia jikoni kiroba cha kilo 25, korie na mazagazaga kibao ndio anahamia kabisa.
  Ugeni wa zamani kama katoka kijijini utafurahi anakuja na mazaga kibao, unga au mahindi,kuku n,k utaacha kumpikia pilau?
   
 5. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Billie huo ndio ukarimu wa kiafrika hasa,babu zetu na hata karibuni baba zetu walifanya hivyo vitu lakini kwa sasa maisha yamebadilika sana na uchumi kwa familia za chini hata za kati sio nzuri kufikia hatua ya kukarimu beyond your means.

  Nakumbuka kwenye miaka ya 80 tulikuwa tukienda kwetu Tabora vijijini kutembelea familly members tulikuwa tunachinjiwa kuku au kambuzi basi ilikuwa kwa ajili ya sisi wageni tu,tunakula, kama ugeni ni wa siku moja basi tulifungashiwa mabaki ya chakula.
  Na babu yangu alinisimulia zamani sana,wanyamwezi walikuwa na mila kwamba kwa mfano mimi ninarafiki yangu ambae alikuwa anaishi mbali labda mwendo wa siku mbili enzi hizo kwa miguu(hakukuwa na gari wala baiskeli)basi akija kunitembelea nampisha kwenye chumba changu analala na mke wangu kwa kipindi atachokuwepo hapo.Yaani huo ndio ukarimu wa kiafrika alivyokuwa.

  Ila kwa maisha ya sasa hivi hapana,inabidi kushare kile kilchopo na kama uwezo upo basi kuimprove kidogo ili kumuintartain mgeni/wageni wa kipindi kifupi tu watakapo kuwepo maana kama wageni wamekuja na watakaa week kadhaa au miezi basi utafilisika kwa ajili ya wageni
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  I hate the ritual of 'glass za wageni' sijui na nini! Mgeni atakachoambulia kwangu ndo size yake. The best china in the house is for me and my family and they deserve them! Inabidi uishi leo, kesho who knows!
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  nimekumiss sana, yaani sana kupita maelezo.
   
 8. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Kulikuwa na vyombo kwa ajili ya wageni?
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ha haaa! kwani mgeni ndo alitaka? Wazazi wako ndo walitaka kujionyesha kwa mgeni they care so wakumlaumu ni wazazi wako
   
 10. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  @Kikungu, bahati nzuri nipo na mama yangu hapa (Mnyamwezi wa Sikonge, Ipole) nimemuuliza kuhusu ukarimu wa kuachia chumba; amekataa amesema hiyo ilikuwa kwa Watusi (kumbuka unyamwezini kuna watusi wengi tu).

  Ila ya kufingirizwa (kupakiwa mapaja ya mbuzi) inaendelea mpaka sasa hata kwetu!
   
 11. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kaunga wewe ni ndugu yangu kabisa,Ipole kuna wajomba zangu pale,sisi kwetu Kikungu,pale Chabutwa unaingia kushoto.
  Muulize mama kama yeye ni Mnyamwezi Mkonongo.Nyamwezi inachukuliwa kama general lakini kuna Wakonongo,Wasumbwa,Wanyinyembi nk.Babu yangu alikuwa na asili ya Wakonongo na miaka mingi sana hicho kitu kilkuwepo na si babu yangu alinisimulia bali miaka mingi kidogo nilihudhulia misa ya msiba ya familly member,padre alitoa habari hii kama sehemu ya mahubiri.PM me please i wanna chart a bit about your familly if you don't mind
   
 12. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Bora awe amekuja kwa style hiyo
   
 13. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Tehe tehe kweli kulikuwa kuna vyombo hivyo kwa ajili ya wageni umenikumbusha mbali sana.
   
 14. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Ndiyo nakubali kuwa ni wazazi ndio waliocheza branda ndiyo maana natoa ahadi kuwa sitarithi utamaduni huo
   
 15. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Jamani msiniache na mimi wa PUGE
   
 16. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Eeee mwe wakukaya ninye?habari nsoga sana,nde PM igolo mmwe
   
 17. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,119
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  washukuru mungu nimepanga ka nyumba kazima na kakizaman kana vyumba ka vitano hivi kila wakija wageni lazima wapete sehemu ya kulala, nikifanikiwa kujenga yangu watajuta vyumba tuwili twa kulala changu na wife na cha mtoto wangu ful stop na bonge la sebure tuone watalala wap.
   
 18. Lucas

  Lucas JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 2,451
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  are you "msukuma"?
   
 19. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  @Kikungu, mama yangu ni pia mkonongo asili ya Inyonga kwa maana ya baba na babu zake. Bado anakanusha; as u say Wanyamwezi ni general, na ujue utusi si Kabila bali ni maumbile na ndio maana ukienda Burundi au Rwanda kwa kuongea wahutu na Watusi hakuna tofauti; na hiyo ya Watusi inaleta sense kwa sababu hata wamasai walikuwa na mila hiyo.

  Tena amesema si marafiki tu; hata baba mkwe anaweza jivinjari na mkamwana anachofanya ni kuchomeka mkuki nje na mwanae anajua dad anashughulika!

  Too bad nimeenda huko few time, as far as Msuva; ndugu wengi wako mjini siku hizi; pia kinyamwezi changu kibaya sana (cha kuunga na gundi).

  We will chat more privately!
   
 20. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Mmnh; nikikutembelea utanilisha miharage? Tusiache mila jamani, twaweza boresha though!
   
Loading...