Mgeni kukuacha na madeni kisa ukarimu

hahahahahahahahhaahhah lohhhhh
Nimecheka dahhhh we hufai kwa kweli ..

usema ukweli matukio mengi ya udogoni ni vigumu sana kusahahu.

kilichokuwa kinanishangaza zaidi ni pale umuombe mzazi kitu . atakwambia fedha hamna subiri mwisho wa mwezi.
lakini mgeni akitokea iwe katikati ya mwenzi au la. hela za kwenda buchani sijui kununua mchele zinapo. huwa
nilikuwa najiuliza je wazazi wetu wanaweka hizi fedha akiba ajili wa wageni tu au? Na hapo siku mgeni anaondoka
atapewa nauli na fedha za kula njiani atabeba na maharage debe moja , mahindi debe tatu, maboga yaaani dahhhh.

Huu upuuzi ndo ulinifanya nianzishe topic hii ni moja ya indicator ya umasikini wa mawazo.Mtu unakuta kazaa matoto saba na bado ana mimba nyingine umeona huruma umchukue mmoja umsomeshe anataka kukuongezea na wengine na ukikataa lawama
 
Fixed point na Afrodenzi mmenikumbusha mbali sana!
Kuna mamdogo alikuwa anaishi like 60 kms away na familia yake. Ana 5 kids na sie tulikuwa 6. Imagine xmas na new year lazma tuhame nyumba! Sasa chumbani tunalala us 3 gals na wao 4 gals! Yaani kulikuwa na extra matress on one bed ila sijui tulikuwa tunapumuaje. It was the best times!
yaani nyie xmas na pasaka tu? ......................
tena unazungumzia habari ya extra matress? mlikuwa mna raha kweli wenzetu. sisi wageni wakiwa wengi mnalala kwenye mkeka, kwa kingoni tunaita MPASA.
 
tehe tehe tehe yaani nilikuwa sina raha imenibidi nicheke saana safi sana Fixed point kwa kutupa flash back ya maisha uliopitia.Kwenye kuku hapo ndo kuna ugomvi unakuta kuku umewazolea ma.vi kwa muda mrefu alafu mlaji anakuwa mgeni isitoshe watoto wanapewa miguu na kichwa mmependelewa sana unapewa kikwapa cha kuku tehe tehe hizi mambo ulaya hamna kabisa.
mgeni akija lazima ukae jikoni na mama kusaidia kukatakata, maana angalau utapata utumbo na miguu. sisi kikwetu mgeni akichinjiwa kuku anapewa na chungu ili ammalize na akimbakiza tu anafungiwa aende naye.........
ila na mimi siku hizi nafaidi sana hao kuku kwa watu, na ninawaonea huruma wale watoto wmbao wanakosa huyo kuku sisi tunapofaidi, ha haaaaaaaaaa, pay back time.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom