Mgawo wa Umeme: Vifurushi vya TV, Kodi TRA zipungue

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,891
Nani asiyejua kuwa umeme haupo kwa siku zaidi ya masaa 12?

Kwanini bei za vifurushi vya TV Azam, Star Times, nk, bei ni ile ile?

Kwa biashara ambazo bila umeme ni kuwa hakuna kazi. Kulikoni kodi TRA ni ile ile?

Hizi zimekaa kiwizi wizi kama zile za nyakati za corona. Biashara hamna kodi pale pale.

Enyi Serikali na wauza vifurushi kama hivi vya TV, ni mbingu gani hupokea majizi?

Kwanini haki kwenu ni msamiati usiokuwa na maana?
 
Hapo kwenye vifurushi vya TV hawawezi kupunguza kwa sababu na wenyewe wanakabwa na TRA... Alafu pia kuna wengine wana Solar na Majenereta wanatizama TV bila shida
 
Nao nimewaongelea tukomae nao huko Kwa mwizi wetu mkuu serikalialiyeshibdwa kutupa umeme ambao tumeshaununua.

Wenye solar na generator Kwa ajili ya TV majumbani, wangapi?

Huku ni kutuibia mchana mchana huku hawa nao na matangazo ya vifurushi vya mwezi. Mwezi upi wakati umeme hamna?!
 
Nani asiyejua kuwa umeme haupo kwa siku zaidi ya masaa 12?

Kwanini bei za vifurushi vya TV Azam, Star Times, nk, bei ni ile ile?

Kwa biashara ambazo bila umeme ni kuwa hakuna kazi. Kulikoni kodi TRA ni ile ile?

Hizi zimekaa kiwizi wizi kama zile za nyakati za corona. Biashara hamna kodi pale pale.

Enyi Serikali na wauza vifurushi kama hivi vya TV, ni mbingu gani hupokea majizi?

Kwanini haki kwenu ni msamiati usiokuwa na maana?

Ngoja nichangie kidogo. Biashara ya TV ni kama bando la simu haijalishi simu ina chaja au laa wanachokifanya wao ni kuangalia muda umefika wa bando kwisha wanakata. Ni kweli inakera mmno unalipia TV halafu hakuna umeme malipo yanakuwa yamekwenda bure.
Angalau kwenye kodi nachojua kama utakuwa unaweka rekodi za kibiashara wataangalia mauzo yako au risiti ulizotoa.
 
Andiko Bora ila sijui Kwa Nini halijaenda viral
 
Kwenda viral si muhimu. Muhimu no kufikisha unumbe. Nilipo nimeamua kutonunua kifurushi cha TV. Ina maana gani kununua kifurushi wakati TV unaitumia Kwa hisani ya tanesco?
 
Ngoja nichangie kidogo. Biashara ya TV ni kama bando la simu haijalishi simu ina chaja au laa wanachokifanya wao ni kuangalia muda umefika wa bando kwisha wanakata. Ni kweli inakera mmno unalipia TV halafu hakuna umeme malipo yanakuwa yamekwenda bure.
Angalau kwenye kodi nachojua kama utakuwa unaweka rekodi za kibiashara wataangalia mauzo yako au risiti ulizotoa.

Simu inaweza kudumu bila umeme wa TANESCO lakini siyo TV. Hivyo biashara mbili hizi si sawa. Naweza tumia simu 24/7 hata umeme wa TANESCO ukiwa haupo nyumbani hata kwa mwezi mzima. Lakini siyo TV.
 
nilichosema siyo kwamba simu inakaa muda gani na chaji nimesema nilichomaanisha ni kuwa hata simu ikikata chaji na ukakosa sehemu ya kuchajia haijalishi bando litakuwa linaisha tu sawa sawa na TV ndugu
 
Nilichokazia ni kuwa:

"Kwa mgawo huu wa Umeme Kwa hakika vifurushi vya TV na hata kodi TRA ilikuwa fair zipungue."

Kwanini tununue vifurushi vya TV majumbani tusipokuwa na jenereta hali umeme haupo kwa masala 12 - 16 kwa siku?

Issue tofauti na simu kwa sababu hata nikichaji Kwa masala 4 kwa siku naweza itumia kwa masaa 30 mfululizo.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Kama vipi hata vifurushi vya simu vishuke,
Mda mwingi simu zimezima.

Ku chaji simu masaa 4 kwa siku inatosha kutumia masaa hata 30 mfululizo.

Simu hata wakiacha ila TV na kodi huu ni wizi was kutumia nguvu.

Ama kwa hakika mimi na washirika wangu sasa hivi ni zile stations 5 za nyumbani za bure. Na nikishazoea? Biashara na vifurushi vyao kwishney!
 
Back
Top Bottom