Watanzania tumekosa mtetezi kwenye suala la umeme, sasa tunaangamia

Kipondo Cha ugoko

JF-Expert Member
Apr 12, 2023
655
1,042
Ndicho nachoweza kusema, machozi ya Watanzania kuhusu kero mbalimbali kwa sasa hayana mtu wa kuyafuta. Sio watawala, sio wapinzani, sio taasisi za kidini Wala yeyote yule. Watanzania tunapigwa bakora za ukosefu wa maji ya uhakika,kupanda kwa gharama za maisha(sukari) kupanda kwa bei za vifurushi vya simu, ukosefu kabisa wa umeme n.k .

kusema kweli kero zote za ukosefu wa maji, kupanda kwa gharama za maisha na uhuni tunaofanyiwa kwenye mitandao ya simu ni kama Watanzania tumekubaliana nayo. Ila hili la umeme kwa kweli hapana.

jamani umeme umekua kero na unatuumiza sana sisi Watanzania wa chini hakika tunaumia tunaumia tunaumia haswa!!!!

Jambo la kusikitisha ni kwamba naona viongozi sio wa upinzani Wala watawala wanaoguswa na hili tatizo, nchi iko gizani karibia mwaka mzima sasa lkn watu wako kimya kana kwamba hakuna kitu chochote kinacholisumbua taifa.

Viongozi wa upinzani nawambieni ktk jambo ambalo inabidi mlivalie njuga ni hili la umeme hakika litapa credit kubwa sana kuelekea mwaka wa uchaguzi 2025.

Watanzania hawana hamu Tena na huyu mama, sio vijijini wa mjini hakika nawambieni. Biashara haziendi watu wanapata hasara kweli kweli! Samaki wanaharibikia kwenye mafriji, nyama zinaoza mabuchani, wauza maziwa nadhani mnanielewa vzr vile mnapata hasara!

Wapi wanangu wa kuchomelea (welding) hasara mnayopata Sina haja ya kuwasimulia, mafundi aluminium, viwanda vidogo vidogo na vikubwa, watu wa saloon (Berber shop), mama ntilie nk. nk....!!
aisee hakika tunalia machozi ya samaki.

Sometime najiuliza hivi kweli viongozi wetu wanakaa kwa amani kbs maofisini kwao ili Hal, Watanzania wenzao wanateseka kiasi hiki na umeme?? Wasivyo na mishipa ya aibu Bado wanapita kudai Kodi kwenye biashara za saloon na mabucha ya samaki na biashara nyingine zinazo athiliwa Moja kwa Moja na ukosefu wa umeme, jamani chonde chonde mtatuuaaaaa.

Mwisho :sasa nimeuona umuhimu wa upinzani kwa usitawi wa nchi, kumbe upinzani ni wamuhimu sana hasa kwenye vyombo vya maamuzi tusichukulie poa! Tunahitaji upinzani dhabiti ktk nchi yetu. Leo hii mwaka unaenda kukata nchi iko gizani lkn husikii mbunge yeyote akisemea swala la umeme, husikii diwani yeyote akisemea swala umeme, hatusikii mwenyekiti Wala kigoda wote kimyaaa!! Kazi kubwa walioambiwa ni kusifu kisichokuepo.

Lkn naamini wapinzani wangekua kwenye vyombo vya maamuzi makelele Yao yangewashitua watawala wangetafuta namna ya kulishughulikia swala hili na Watanzania tungepata afueni.

Kumbuleni mpaka sasa hakuna mwenye jibu ni lini mgao (Mimi nauita ukose wa umeme kbs) tutaondokana nao.

Poleni waganga njaa wenzegu kwa bakora za mgongo hakika chozi letu ni lasamaki.

By kinyozi wa saloni mtoni mtongani.
 
Lkn naamini wapinzani wangekua kwenye vyombo vya maamuzi makelele Yao yangewashitua watawala wangetafuta namna ya kulishughulikia swala hili na Watanzania tungepata afueni.
Umejichanganya mkuu! Wapinzani wanapigania;
  • Uraia pacha wa watoto wao
  • Ruzuku, inaingia mifukoni mwao
  • Nafasi za mamlaka/madaraka

Uwe muungwana tu kusema, aliwahi kuwepo mtu aliyewahi kukerwa na hizo kero na akaonesha nia ya dhati kuzitatua, SIO WAPINZANI.

Unajua kuwa sukari imepanda, kisa mvua? Wapinzani wamefanya nini?

Unajua kuwa umeme ni shida, unaambiwa matengenezo, mara mvua hakuna, unakubaliana nayo hayo? Wapinzani wamefanya nini?

Unajua kuwa mamlaka za maji zimefeli vibaya, wapinzani wako kimya!

Unayo taarifa, nauli zimepanda, wao kimya?

Unajua kuwa hatuna dawa, hatuna chakula cha akiba? Bashe anakanya twende, wao wanafanya nini?

Ni mengi mno ya hovyo nchi hii, CCM wanatengeneza matatizo kwaajili ya maslahi yao...wapinzani wanapambania maslahi yao.

Niambie, maandamano ya kwanza kabisa waliyokusudia kufanya, dhima yake ilikuwa nini?
 
20240208_221223.jpg
 
Mpinzani akutetee kivipi wakati wewe mwenyewe autetei upinzani?! Yakija maandamano unaungana na wakatili wako, shida zikikufata unataka mpinzani akutetee,

Hivi mtajifunza lini kutafuta haki zenu bila lawama?! Kibaya zaidi mnalalamikia chooni ambako uko peke yako nani atakusikia?

Bahati mbayaa umesikika, utaikana hata sauti yako udanganye labda ulikuwa unaota au majini yalipanda
Simamieni haki zenu kwa nguvu, zote, hak aiombwi, haki inachukuliwa

Acheni uchawa, uchawa ni unafikk na ukiuchunguza vizuri una hakisiana na ushoga
Hivyo tu
 
Back
Top Bottom