Mfumo wa kuajiri kupitia Ajira Portal na kuita watu kwenye usaili physically mikoa ya mbali unamaliza pesa za serikali na wananchi

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,333
8,252
Naomba serikali iliangalie hili.

Katika utafiti niliofanya nimegundua jambo hili:

Mfumo wa kuajiri kupitia ajira portal na kuita watu kwenye usaili wa mchujo physically mikoa ya mbali unamaliza pesa za serikali na wananchi.

Fedha zinazotumika kusafirisha maafisa utumishi kutoka ofisini kwao mpaka mikoa unakofanyika usaili ziokolewe. Usaili unafanyika siku hadi nne fedha zinapotea.

Fedha zinazotumiwa na wasailiwa kusafiri, kulala na kula wakiwa kwenye hiyo mikoa unakofanyika usaili ni nyingi pia.

Fedha zinazotumika kuchapisha mitihani ya wasailiwa 900 kwenye kazi inayohitaji watu wawili zinapotea. Hivyo ziokolewe.

Nguvu inayotumika kusahihisha mitihani ya watu 900 kutafuta watu wawili ni kubwa sana kuliko uhitaji. Akili itumike hapo. Muda mwingi, nguvu nyingi na fedha nyingi inatumika kutafuta watu wawili.

Solution: Usaili wa mchujo ufanyike online itakua vyema zaidi ili kuokoa fedha, muda na nguvu inayotumika kuwafanyia usaili. Zipo software nzuri zenye uwezo wa kufanyisha mitihani ya mchujo online bila udanganyifu wowote. Dunia imebadilika badala ya kuendelea kuprint mitihani, kukusanya, kuhifadhi, kusahihisha, tutumie njia za kidigitali.

Tubadili mfumo, tutumie akili kuliko nguvu. Tuokoe muda na fedha zinazotumika kutafuta watu wawili kwa jambo dogo.

Kupitia hii app, kuna institution iliweza kuwafanyia usaili wa mchujo watu elfu 30 kwa wakati mmoja. Walifanya mtihani. Kupitia hii app mitihani haiwezi kuharibika. Huwezi kuangalizia inakunote yenyewe. Huwezi kupiga kelele inakudetect yenyewe. Dunia imebadilika saivi.

1. ExamClient(For computer)

Google Chrome browser is suggested for downloading with the link below, Please click and input your Passport/ID No.


2. Proctor Assistant(For Mobile phone/Tablet)

For Android mobile phone, please download the APP from the designated link:


For iPhone, please find and download Proctor Assistant from APP Store directly.

IV. Testing procedure

1. Please prepare the test environment, equipment, Internet, paper and pens as required.

2. Mute your mobile phone/tablet (while the phone should be turned on flight mode and then connect to WiFi), run the Proctor Assistant APP, check your identity and environment according to the guidance of invigilators, and place it 1 meter behind your rare side.

3. Start the computer, close the anti-virus software(or add ExamClient into Whitelist of antivirus software) and other irrelevant programs, and run the ExamClient no later than one hour before the test. After passing the device and network detection, enter your Passport/ID No. and password to enter the exam.

4. Read the test disciplines and wait for the test to begin.

5. Test begins, no submitting nor leaving is allowed before the end of the test.

6. End of testing time, please wait for invigilators confirm your submitting status.

7. Submitting status confirmed, tear up all paper.

8. Leaving by quitting the ExamClient and Proctor Assistant.
 
Wanatakiwa watumie mfumo wa online acha ubishi. Hiyo namba iliyowekwa hapo ni mfano tu.
Online?🤣.. hiyo online watafanyaje mtihani?

Ushawahi fanya written interview? Kama ushawahi huwa kuna MCQs? Kama hakuna unategemea online msailiwa ataandikaje essay?

Halafu hiyo online utawazuiaje watu ku-cheat? Huko online nani atakuwa msimamizi? Si wasailiwa wote watapata 100%?

Hebu acha ubishi, kuna mambo mengine hata mataifa yaliyopiga hatua kimaendeleo hawayafanyi online. Interview ya kazi huwezi kufanyia online, la sivyo cheating itakuwa kubwa sana.
 
Online?🤣.. hiyo online watafanyaje mtihani?

Ushawahi fanya written interview? Kama ushawahi huwa kuna MCQs? Kama hakuna unategemea online msailiwa ataandikaje essay?

Halafu hiyo online utawazuiaje watu ku-cheat? Huko online nani atakuwa msimamizi? Si wasailiwa wote watapata 100%?

Hebu acha ubishi, kuna mambo mengine hata mataifa yaliyopiga hatua kimaendeleo hawayafanyi online. Interview ya kazi huwezi kufanyia online, la sivyo cheating itakuwa kubwa sana.
App zipo rafiki naomba fanya utafiti vizuri.
 
App zipo rafiki naomba fanya utafiti vizuri.
Mkuu acha ubishi basii....

Kuna vitu vya kufanyika online ila siyo interview... Mfano applications za kazi kufanyika online ni sahihi kabisa..... Ila interview? Hiyo haitokaa itokee.

Mfano mimi nimeapply udaktari, ikifika siku ya interview nitashindwa nini kumtafuta daktari mzoefu anifanyie hiyo interview?

Ukitaka kuandaa "Setting" ya online interview ambayo itazuia udanganyifu basi jua gharama zake ni kubwa zaidi maana utahitajika uwe na CCTV, wataalam wa mifumo nk.
 
Njia inayotumika kwa sasa ni sahihi zaidi.

Changamoto kubwa ni nafasi zinatangazwa ni chache sana ilhali waombaji ni wengi, hii inapelekea wengi kukata tamaa wanapoenda kwenye kituo na kurudi hola akiweka na gharama za nauli na malazi.

Njia zinazowezekana ni hizi pamoja na changamoto zake.

1. Mchujo ufanyike kuanzia kwenye vyeti, hii itapunguza idadi ya wanaokwenda kwenye written ila pia utaleta ubaguzi mkubwa sana, itakua kama UDSM vs ufaulu wako, kwa hivyo hii njia sio fair.

2. Kuweka vituo kila mkoa, hii ni nzuri kwa maana itawapunguzia usumbufu waombaji kwenda mikoa ya mbali kwa ajili ya usahili, ila changamoto kubwa hapa ni gharama kubwa zitatumika kuweka watumishi kila mkoa, pili uvujaji wa mitihani utakua rahisi zaidi ni hovyo kupelekea usumbufu katika uratibu wa zoezi zima.

3. Online interview, ni njia nzuri inatumika na makampuni makubwa, ila mchujo wake ni mkubwa sana, unakuta mpaka kufikia hatua ya kufanya interview kuna panga kubwa limepita na hizi nafasi mara nyingi ni zile zenye kuhitaji mtu mwenye CV nzito hivyo upanguaji unaanzia kwenye uzoefu na mambo mengine, pia interview za namna hii hufanyika kwa njia ya video conferencing jambo ambalo no wachache wanaweza kuwa na access nalo kutokana na changamoto ya mitandao, kwa ujumla hii njia haifai kwa mazingira yetu.

SULUHU
1. Sekta binafsi ndio inatakiwa ichachuliwe iweze kutoa ajira nyingi ni jukumu la serikali kuandaa mazingira ya sekta binafsi kukua kwa kasi na kutoa ajira kwa vijana wengi, kutegemea ajira za serikali tu hakuwezi kuondoa tatizo la ajira nchini.

Tunaweza kuilaumu serikali haitoi ajira ila walipo mitaani ni wengi kuliko nafasi zilizopo, ni sawa na hapo nyumbani kwako/kwenu umeajiri mlinzi mmoja, ila kuna walinzi 300 wanakulaumu huko nje hutoi ajira kwa walinzi, sasa utaajiri walinzi 6 si itakua matumizi mabaya ya fedha😂

Kingine mifumo yetu ya elimu ni mibovu kuliko, nasikitika sana hatuondoki na ujuzi wowote wa kueleweka vyuoni, research hatufanyi za maana zinazofanyika ni michongo tu ili watu watunukiwe phd's ila hazina tija kwa taifa.

Tuna wahandisi wa kutosha ila makampuni makubwa yote yanatoka nje, je tuseme kwamba tuna IQ ndogo kama wazungu wanavyotuona jibu ni hapana tuna maandalizi mabovu kuanzia ngazi ya chini kabisa.

End.
 
Back
Top Bottom