Mfumo ule ule unataka kurudi kupitia UKAWA!


Cha msingi chagua mbunge wa upinzani mengine baadae:mvutaji:
 
Ww ni ccm kuwatosa kina nani??? Unadhani cc mabwege tumekugundua hatoswi mtu na bado
 
ETi MUDA HUU BAADA YA KUHAMA NOD MA CCM YANAWAITA MAFISADI WAKIWA MLE CCM SIO MAFISADI DAH
SASA KINA KINANA, MUHONGO, NGELEJA, TIBAIJUKA HAMPIGI KELELE MBONA???
 
Walishindwaje kuwatumikia wananchi miaka 12 iliyopoita halafu waweze leo?
Kinachotokea hivi sasa ni muhimu sana na tena kilichelewa. Kwa kuwa watanzania ni wale wale imelazimu wajigawe mara mbili au hata tattu washindane. kinachotakiwa ni kushindana kwa faida ya nchi. Mchezo wa SEE SAW hauwezi kuendelea ikiwa upande mmoja utazidi sana upande wapili. sasa mchezo utabance
 

1. Lowassa Richmond ( zingine sijui)
2. Sumaye EPA, RADA, NDEGE YA RAIS, MIGODI BIZWAGI na mingine (vingine sijui)
3. Pinda ESCROW,

Kwa kifupi wote wezi tu
 
Poor analysis
 
mfumo maana yake nini? kwani mfuno si ulitengenezwa na watu hao hao? leo watakuja na mfumo gani mwingine kama watu ni walewale? UCHU WA MADARAKA TU HAMNAA LINGINE. period!
 
Nasikitika kwa mwalimu wako kukuganganya na ningekushauri urudi shule tu.kama siasa ni uongo niambie nani anaamua barabara fulani ijengwe au na kwa mujibu wa mwalimu wako barabara pia ni uongo?shule ni uongo?Pole ndugu
Ahadi zaViongozi wa Siasa ni uongo mtupu. Vipi Ahadi ya Kiongozi wenu aliyesema Hivi ninanukuu (MAISHA BORA KWA KILA M-TANZANIA) Haya kuna maisha gani bora Tangu Huyu Mkuu atangaze hiyo iKampeni au ilani yake ya Uchaguzi tangu ashike Madaraka kuna maishagani bora hapo Tanzania? kam Sias sio uongo wa hali ya juu ni kitu gani? Nenda kasome tena Shule wewe sijuwi umesoma chini ya muembe wewe ? Mutadanganywa na Viongozi wa Siasa wao Viongozi wananufaika nyinyi walal hoi munazidi kuumia kazi kwako au kazi kwenu Walala Hoi ni Siasa za Viongozi wa kisia za uongo mtupu.
 
hawa ndio walikua wanahalibu waliweka makundi...hayo makund peleka ukiwa
 
Hatari kubwa ni mwisho wa siku fikra tulizozikataa kwa watawala wa sasa zinaweza kabisa kuibukia kwa watawala wajao... ndio maana ni muhimu sana kupinga (dissent) pale inapoonekana ni lazima.
 
Mimi sioni tatizo kabisa hao watu wanaotoka CCM na kujiunga na upinzani.

Ndo uhalisia wa siasa huo.

Watu huhama na kubadili kambi mara zote na si Tanzania tu bali ni duniani kote.

Kama wana nia ya kweli ya kuimarisha upinzani na kujenga upinzani wenye nguvu basi mimi sina tatizo kabisa.

Acha tu watoke huko CCM.
 

NN... hili lina ukweli sana ila kuna kitu kingine cha kuangalia ambacho nadhani kwa Tanzania ni tofauti sana na tumetengeneza wanasiasa wanyemeleaji.

a. Suala la kutokuweka timetable vizuri ya uchaguzi hadi miezi tu kabla ya Uchaguzi imetengeneza wanasiasa uchwara sana. Fikiria kwa mfano, sheria ingesema kwa mfano wagombea wa nafasi mbalimbali wawe wamejitokeza na kujulikana angalau miezi 12 kabla ya Uchaguzi Mkuu na wawe angalau wanachama wa vyama husika mwaka mmoja kabla hawajagombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma (public office).

b. Suala la uwezekano wa kuwa na wagombea wasiochaguliwa (a.k.a wenye kupita bila kuchaguliwa) ni mojawapo ya mambo yanayochangia sana rushwa. Kwa mfano tungeweka kama ilivyo kwa Urais.. mgombea asiye na mpinzani wa chama kingine anaruhusiwa kupambanishwa na mtu au watu wengine kutoka chama chake au kama hamna basi apigiwe kura ya ndio au hapana.

Ilivyo sasa, utaoana kuwa wengi wanaohama hakuna anayehama kwa sababu hasa amepingana kifikra au kiitikadi na chama chake. Fikiria hivi.. leo hii kuna kundi la "ulipo tupo"; kundi hili ni wazi halijaifuata CDM hata kidogo bali wamemfuata yule bwana alipo. Sasa ikitokea hayupo au anaamua kujitoa tu.. unafikiria wale wa "ulipo tupo" wataendelea kumpigia kura mgombea au wagombea wa CDM tena? si watasema "hayupo na sisi hatupo"?
 

Hilo hata mimi nimeliona na nimeliona kama ulivyoliona wewe. Nilishangaa sana inakuwaje sisi hatuwajui wagombea urais ni akina nani ikiwa imebaki miezi minne tu.

Kwa kweli kuna haja ya kujua mapema zaidi ya hapo [miezi minne] wagombea wa urais ni akina nani. Miezi mitatu na miwili haitoshi kabisa, kwa mtazamo wangu.


Ndo maana wasiwasi wangu ni kama ikitokea UKAWA wanashindwa, ina maana hawa akina Johnny-come-lately watahama upinzani na kurudi tena CCM?

Kwangu itapendeza zaidi kama wakibakia na kuendelea kuuimarisha upinzani na hapo walau watakuwa wametuonyesha kwamba kifikra na kiitikadi sasa wamebadilika.

Lakini ngoja tusubiri tuone.....
 
Hatari kubwa ni mwisho wa siku fikra tulizozikataa kwa watawala wa sasa zinaweza kabisa kuibukia kwa watawala wajao... ndio maana ni muhimu sana kupinga (dissent) pale inapoonekana ni lazima.

Hofu yangu,hoja yangu,fikra zangu na hasira zangu zimejikita katika hoja hiyo haswa.mabadiliko tuliyoaminishwa na kuyaimba miaka takribani miaka ishirini na zaidi ndio haya?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…