Mfanyakazi wa Barrick apotelea mgodini

Mfanyakazi wa Barrick apotelea mgodini

Kingine vyombo vya habari vipo wapi kuandika vitu kama hivi..kazi yao kuandika vicky kamata atafunga ndoa ya 96 milions... Usalama wa Mtanzania ndio vitu vya msingi kabisa.
 
Hili ndilo jibu Mkuu
kwani hapa kuna watu wanataka MAUJIKO kuwa kazi ya kufanya chini ya ardhi (Jehanamu ni rahisi kivivyo) Mtenda Kaya alichotuelewesha ni kuwa hawa wenye Migodi km wa Bulyankulu wao ni pesa kwanza kwani mfanyakazi kapotea wanaambiwa kazi itaendelea na hata vyombo habari havitangazi bali ni Member wa JF
Mtendaji wa kaya wala usikate tamaa kutuhabarisha sisi watanzania kuhusu huyo mwenzetu na Wazazi wake waliofika hapo kumtafuta mtoto wao,
Hao wanaokupinga kuwa kufanya kazi Kaburini ni rahisi wana yao na usikute ni wale wanaopachikwa na maGodfather hivyo kuchota wakitakacho lakini walala hoi ni kila mahali ndio wanaoumia
huwezi kusema ukiwa kwenye kitengo cha Ventilation ni shushi wakati unaambiwa mwenzako kapotea
niheri wote kuwa na umoja ili Miner wote wawe katika maisha bora na salama
Kazi zisimame mpaka Wiliam apatikane huo wizi wa dhahabu ni hasara kwetu hakuna tunachoambulia

Nawashangaa wanaonipinga...uhalisi wa mambo ni kwamba wawekezaji hawa wanatuua kabisa.....sasa hivi walisha anza kulipua miamba wakati kuna mtu alishapotea...maana yake nini
 
Last edited by a moderator:
nawashangaa wanaonipinga...uhalisi wa mambo ni kwamba wawekezaji hawa wanatuua kabisa.....sasa hivi walisha anza kulipua miamba wakati kuna mtu alishapotea...maana yake nini

hajapatikana huyu mtanzania mwenzetu?
 
Mkuu sina haja ya kutafuta ujiko eneo hili tunapotumia majina yasiyo yetu na hata hapa hujanifahamu.Nimeingia hapo Buly kama Miner Trainee na trainers wangu akina Mwakitalu,Gibu na Caroly na uwezo na mipangi niliyokuwa nayo ndiyo iliyonipa nafasi ya kwenda long hole na si Convetional kwa Fritz Kussel kwenye ma-jack leg.Kuna watu wako hapo miaka nenda miaka rudi akiwemo yule Jumbo Operator anayeitwa Mhina ambaye naambiwa kaacha hivi karibuni alikuwepo Tangu TBRJ unawajua hawa wewe?Silicosis ni tatizo kwa watu waliokuwa na matatizo yao na wewe unaweza ukiwa makini...achana na pombe za Kakola na wanawake wa hapo piga kazi miaka yako mi 3 au mi 4 utakuwa umetoka.

Daah umenikumbusha mbali...Kakola kwenye lile basi bar lenu...Usafiri baiskeli, hivi watu wakiwa tilalila walikuwa wanapona kuanguka kweli?
 
Mungu awape amani wana bulya ,nimefanya hapo miaka kumi na sasa nimeondoka nashukuru mungu,najua ugumu wa hapo kwani nilikuwa kikosi cha uokoaji na nilishiriki vyema kuwatoa wale jamaa 3 waliofukiwa level 4040 ,poleni sana
 
Poleni watanzania na hasa Wachimbaji mnaoshuka ardhini
Mpaka saa hizi hakapatikana?
Niliuona uokoaji wa Wachimba mogodi huko Chile kwenye Luninga, wao walikuwa na vifaa vingi vya mawasiliano.
NI kweli hatujafikia huko ? ili kila anayeshuka shimoni akawa na mawasiliano?
Maana hakuna tofauti na Kaburi mtu kuzama peke yako

Umeongea point hata mimi najiuliza hapa ina maana mtu akiingia chini anakua hana chombo chochote cha mawasiliano like walkie-talkie ili kujua status yake.
 
Kwa bahati mbaya thread hii imeshindwa kutufahamisha hatima ya kijana mwenzetu Willy.
Tafadhali Mkuu @wa Kaya njoo tujuze
 
Last edited by a moderator:
Mi nilipo pata taarifa ya kwamba meneja mkuu wa mgodi kuruhusu ulipuaji wa miamba kufanyika na serikali ya Tanganyika haikuwa imetoatamko lolote, basi niliishiwa maneno
 
Mpaka leo hii tarehe 28 may hawajafanikiwa kumpata! Kwakweli ni utata tupu hata hamu ya kazi imekwisha wakati huo huo meneja alisharuhusu uzalishaji kuendelea! Miner wote hatuna amani kabisa hata vyama vyetu TAMICO na NUMET navyo viko kimya..kwa mawazo yangu vyama hivi vingeshawishi mgomo mpaka mwenzetu atakapopatikana...Tatizo jingine kubwa Simu wanapewa ma supervisor tu na baadhi ya ma operator wa mashine kubwa kama Jumbo unakuta katika kundi la wafanyakazi 50 Kuna wanne au watano wenye Simu...wengine hatupewi simu tunapokuwa underground...pia kuna simu zimewekwa za mezani chini ya ardhi ambazo ziko mbali mno na maeneo ya kazi! Baba na mama wa ndugu aliyepotea wapo wamepewa hifadhi ndani ya mgodi....mpaka sasa hata serikali ya wilaya haijatamka lolote na hakuna chombo chochotw cha habari kimelipoti isipokuwa Jf pekee...NAWASILISHA
 
Tuna hofu kuu imetubini tuwe tunakaa ki makundi makundi tuwapo chini ya ardhi! kumbuka mgodi huu umefika mbali sana Hatua 3940 kutoka surface
Ni mbali mno kutoka usawa wa ardhi
 
Mungu awasaidie sana, inahuzunisha na pia inabidi mkae mkijua kila unapoingia humo ni suala la kufa au kupona kuweni watu wa ibada na hofu ya Mungu. Pili kuweni na malengo na myashike hasa. Jiwekeeni malengo kwamba nitakuweko hapa kwa muda fulani niondokr nikafanye kitu kingine. Msitake kupazoea hata wakiongeza mshahara, ukweli haubadiliki a mine will still be a mine!
Nawaombea faraja wazazi wake maana bora upewe hata maiti kuliko kukaa hali hii.
Tuna hofu kuu imetubini tuwe tunakaa ki makundi makundi tuwapo chini ya ardhi! kumbuka mgodi huu umefika mbali sana Hatua 3940 kutoka surface
Ni mbali mno kutoka usawa wa ardhi
 
Mh Nilisikia Juzi bungeni waktu wanaoka huko shimoni, wakirudi uraiani hawafikishi miaka 5 wanakufa, na rekodi inaonesha watu zaidi ya 300 wakiotoka kule washakufa. Ilikuwa wanaongelea inshu za NSSF na hifadhi za jamii.<br>Poleni sana wadau. Inauma manake kapotea kama ndege ya Malaysia MH370.
 
Mpaka leo hii tarehe 28 may hawajafanikiwa kumpata! Kwakweli ni utata tupu hata hamu ya kazi imekwisha wakati huo huo meneja alisharuhusu uzalishaji kuendelea! Miner wote hatuna amani kabisa hata vyama vyetu TAMICO na NUMET navyo viko kimya..kwa mawazo yangu vyama hivi vingeshawishi mgomo mpaka mwenzetu atakapopatikana...Tatizo jingine kubwa Simu wanapewa ma supervisor tu na baadhi ya ma operator wa mashine kubwa kama Jumbo unakuta katika kundi la wafanyakazi 50 Kuna wanne au watano wenye Simu...wengine hatupewi simu tunapokuwa underground...pia kuna simu zimewekwa za mezani chini ya ardhi ambazo ziko mbali mno na maeneo ya kazi! Baba na mama wa ndugu aliyepotea wapo wamepewa hifadhi ndani ya mgodi....mpaka sasa hata serikali ya wilaya haijatamka lolote na hakuna chombo chochotw cha habari kimelipoti isipokuwa Jf pekee...NAWASILISHA

Hapa mi nailaumu serikali kwa kuwa sheria inasema linapotokea suala kama hili lazima mkaguzi wa migodi wa kanda (zonal mining officer) aje akague aandae ripoti ya kuufungia mgodi au kuruhusu uzarishaji kuendelea baada ya kujiridhisha.
Pia na nyie wafanyakazi hamna umoja mpaka leo hamna chama kimoja chenye nguvu mmegawanyika mara NUMET mara TAMICO hebu kuweni na organization moja yenye nguvu inayoweza kumtikisa kaburu.
 
Mkuu usiwalaumu mimi nimepitia kazi sio kama lakini pia ni risk. Malipo yakiwa makubwa na pia watu wakiwa wamekuja kwa malengo tofauti na vigumu kuwa na umoja. Umeishaambiwa mishahara ya expert ni juu ndo ilivyokuwa kwetu, na hizi tofauti ndo zinawafanya wawe vipofu. Ukiangalia hao miner pia kuna waliojitambua wamekuja kwa malengo ya hata miezi 6 12 24 sasa uanze kumwambia habari sijui za kuungana kwa malengo ya muda mrefu haingii kichwani kabisa. Ndo maana nawaambia kwa kila trip unayoenda weka malengo. Mimi niliweka 5 yrs nilipoacha walinishangaa but nilisema no freedom and family happiness is better than money. Nikapata kwingine.
Hapa mi nailaumu serikali kwa kuwa sheria inasema linapotokea suala kama hili lazima mkaguzi wa migodi wa kanda (zonal mining officer) aje akague aandae ripoti ya kuufungia mgodi au kuruhusu uzarishaji kuendelea baada ya kujiridhisha.
Pia na nyie wafanyakazi hamna umoja mpaka leo hamna chama kimoja chenye nguvu mmegawanyika mara NUMET mara TAMICO hebu kuweni na organization moja yenye nguvu inayoweza kumtikisa kaburu.
 
Mpaka leo hii tarehe 28 may hawajafanikiwa kumpata! Kwakweli ni utata tupu hata hamu ya kazi imekwisha wakati huo huo meneja alisharuhusu uzalishaji kuendelea! Miner wote hatuna amani kabisa hata vyama vyetu TAMICO na NUMET navyo viko kimya..kwa mawazo yangu vyama hivi vingeshawishi mgomo mpaka mwenzetu atakapopatikana...Tatizo jingine kubwa Simu wanapewa ma supervisor tu na baadhi ya ma operator wa mashine kubwa kama Jumbo unakuta katika kundi la wafanyakazi 50 Kuna wanne au watano wenye Simu...wengine hatupewi simu tunapokuwa underground...pia kuna simu zimewekwa za mezani chini ya ardhi ambazo ziko mbali mno na maeneo ya kazi! Baba na mama wa ndugu aliyepotea wapo wamepewa hifadhi ndani ya mgodi....mpaka sasa hata serikali ya wilaya haijatamka lolote na hakuna chombo chochotw cha habari kimelipoti isipokuwa Jf pekee...NAWASILISHA

We jamaa unapotosha sana aisee na naamini kwa watu wengi ambao hawauui mgodi wanaweza kuwa wana-buy hizi cheap stories zako.Dhahabu si Zabibu kuwa utaenda kwenye mti ukachume ni lazima ifuatwe huko chini iliko.Buly si miongoni mwa migodi mirefu.Ulizia hao wasauzi ulionao hapo wakupe habari ya Anglo-Platinum huko Jberg ndo ujue kuna migodi mirefu.

Ni upuuzi kuamini kuwa kila mtu anapaswa kuwa na chombo cha mawasiliano na hakuna mgodi wa aina hiyo duniani ndo maana kuna dispatcher kwa ajili ya ku-coordinate mawasiliano huko underground na surface.Unaweza kuimajin kila mtu akiwa na mawasiliano hali ingekuwaje hapo?Na hili la kusema mgodi unazalisha wagonjwa 300 umelitoa wapi?Hii Tabia ya Kitanzania ya kulalama tu kwenye kila jambo.Huna umuhimu wa kukaa UG kwa miaka 10 you just need to work hard spend wisely then utatoka.Kama ungekuwa ni wa muda mrefu kidogo untakuwa unamfahamu Ray Lavouie mzee wa Ki-Canada ambaye kafanya UG for 40 years na Buly peke yake kafanya about 16 years mbona alitoka poa tu akiwa mzee kabisa?Usipotoshe watu JF bana.

Mh Nilisikia Juzi bungeni waktu wanaoka huko shimoni, wakirudi uraiani hawafikishi miaka 5 wanakufa, na rekodi inaonesha watu zaidi ya 300 wakiotoka kule washakufa. Ilikuwa wanaongelea inshu za NSSF na hifadhi za jamii.<br>Poleni sana wadau. Inauma manake kapotea kama ndege ya Malaysia MH370.

Mkuu kwani kufa ni kwa sababu ya kufanya kazi huko tu?Zingatia pia idadi ya waajiriwa wa mgodi huo tu kwanza.Kuna waajiriwa zaidi ya 200o.Na kufa mtu anakufa tu hata kama anafanya ikulu ila siamini kama kuna watu waliokufa kwa work related issues na serikali ikaendelea kuruhusu mgodi uendelee kumaliza watu.Huu ni upotoshaji mkuu.Nimekaa for almost 3 years Underground am now healthy and sound doing my own stuff kwa capital niliyotoka nayo mgodini
 
Mpaka leo hii tarehe 28 may hawajafanikiwa kumpata! Kwakweli ni utata tupu hata hamu ya kazi imekwisha wakati huo huo meneja alisharuhusu uzalishaji kuendelea! Miner wote hatuna amani kabisa hata vyama vyetu TAMICO na NUMET navyo viko kimya..kwa mawazo yangu vyama hivi vingeshawishi mgomo mpaka mwenzetu atakapopatikana...Tatizo jingine kubwa Simu wanapewa ma supervisor tu na baadhi ya ma operator wa mashine kubwa kama Jumbo unakuta katika kundi la wafanyakazi 50 Kuna wanne au watano wenye Simu...wengine hatupewi simu tunapokuwa underground...pia kuna simu zimewekwa za mezani chini ya ardhi ambazo ziko mbali mno na maeneo ya kazi! Baba na mama wa ndugu aliyepotea wapo wamepewa hifadhi ndani ya mgodi....mpaka sasa hata serikali ya wilaya haijatamka lolote na hakuna chombo chochotw cha habari kimelipoti isipokuwa Jf pekee...NAWASILISHA

We jamaa unapotosha sana aisee na naamini kwa watu wengi ambao hawauui mgodi wanaweza kuwa wana-buy hizi cheap stories zako.Dhahabu si Zabibu kuwa utaenda kwenye mti ukachume ni lazima ifuatwe huko chini iliko.Buly si miongoni mwa migodi mirefu.Ulizia hao wasauzi ulionao hapo wakupe habari ya Anglo-Platinum huko Jberg ndo ujue kuna migodi mirefu.

Ni upuuzi kuamini kuwa kila mtu anapaswa kuwa na chombo cha mawasiliano na hakuna mgodi wa aina hiyo duniani ndo maana kuna dispatcher kwa ajili ya ku-coordinate mawasiliano huko underground na surface.Unaweza kuimajin kila mtu akiwa na mawasiliano hali ingekuwaje hapo?Na hili la kusema mgodi unazalisha wagonjwa 300 umelitoa wapi?Hii Tabia ya Kitanzania ya kulalama tu kwenye kila jambo.Huna umuhimu wa kukaa UG kwa miaka 10 you just need to work hard spend wisely then utatoka.Kama ungekuwa ni wa muda mrefu kidogo untakuwa unamfahamu Ray Lavouie mzee wa Ki-Canada ambaye kafanya UG for 40 years na Buly peke yake kafanya about 16 years mbona alitoka poa tu akiwa mzee kabisa?Usipotoshe watu JF bana.

Wewe ni mpotoshaji mkubwa! habari ya waginjwa 300 raia mwema wameiandika sana halafu hata pale bungeni utafiti huo umetolewa! tatizo lako ni hicho cheo ulichopewa mgodini! unataka kuniambia hatua 3940 ni pafupi? usipende kuleta ujinga kwenye issue serious kuna watu hawapo bulyanhulu wanajua zaidi kuliko wewe.. fuatilia vyombo vya habari siyo kukalia magazeti ya ijumaa mbu mbu mbu wewe
 
Mbongo akipata cheo husaliti mpaka nafsi yake ...Captain Philip ni mmoja wapo! upotoshaji wangu uko wapi? miners hawapewi simu'huyu bwana hajapatikana'mgodi upo 3940 level toka usawa wa ardhi'hofu mgodini ipo'300wagonjwa na hufa vyombo mbalimbali vimetafiti hadi bungeni imesonwa! upotoshaji wangu uko wapi? tena umeniobgezea machungu ...mwenzetu hayupo wewe unasema napotosha! ebo...
 
Back
Top Bottom