Mfanyakazi wa Barrick apotelea mgodini

Mfanyakazi wa Barrick apotelea mgodini

Level aliyopotelea mhanga inaitwa 4130 kuna madai tofauti kuhusu kupotea kwake,(1) mashine hatari kabisa iitwayo scoop na yenye nguvu za kutisha ilimgonga,na kisha operator wa mashine ile kumbeba ktk mashine na kisha kumtupa ktk shimo refu maarufu kwa jina la open hole ili kuficha ushahidi.(2)alipowaaga wenzake kuwa anaenda kujisaidia bila shaka kwa bahati mbaya mno akatumbukia ktk open hole ambayo ipo kama mita 20 tu kutoka pale alipokuwa na wenzake.(3)kachukuliwa na majini au mizimu,mimi ni mfanyakazi wa BARRICK kitengo cha chini ya ardhi,japokuwa wengi hawasadiki ila kule chini kuna mauzauza mengi sana,siku moja miezi miwili tu iliyopita saa 11:30 jioni nikiwa nimechelewa kutoka chini ya ardhi ktk level ile ile ya 4130 aliyopotelea mhanga,niliitwa na mtu asiyeonekana,sikuitika,na mahali pale watu wote walikuwa wametoka ilikuwa maeneo ya rockbreaker.

Scoop 14 nona mkuu habari ya mgodi staki hata kuisikia
 
hatari yake ipo vipi?

1400 Scoop ni mashine kubwa, yenye nguvu. Mashine hizi hutegemewa sana kwa uzalishaji wa kifusi madini kule Under Ground, na kwa kuongeza inauwezo wa kunyenyua hadi tani arobaini kwa mkupuo mmoja kwenye kijiko (bucket
 
Mgodini hakuna lolote hakuna chochote...huko ni kufuata magonjwa tu! nenda getini wakati wafanyakazi wanaingia au kutoka! wengi wamechoka wanachechemea viuno na migongo anatamani anapokuwa kwenye basi la kumrudisha nyumbani anyooshe miguu yake kama anataka kulala-*akifika kwake ni kulala hata kula wanakula wamelala! kuna wengine wamefungiwa vyuma miguu mwaka wa pili anatembea na chuma mguu ushaoza...na supervisor anampa kazi kama kawaida
 
hivi huko underground kuna wafanyakazi wanawake wanaoingia?
 
hivi huko underground kuna wafanyakazi wanawake wanaoingia?

Miaka ya 1999-2001 aliwahi kuwepo mama wa ki-Australia alikua ni surveyor, na miaka ya kabla ya 2013 palikua na fundi pia manesi waohuenda under ground.
Lakini sijawahi kuona mchimbaji mwanamke pale bulynhulu
 
Si hatari kivilee ukilinganisha na ajari za kawaida za balabalani. Ni bahati mbaya kuwa mwenzetu ametangulia ni sehemu salama zaidi ukilinganisha na maeneo mengine hasa nchini mwetu.
 
hatari kweli kweli
 
Si hatari kivilee ukilinganisha na ajari za kawaida za balabalani. Ni bahati mbaya kuwa mwenzetu ametangulia ni sehemu salama zaidi ukilinganisha na maeneo mengine hasa nchini mwetu.

Mkuu, usirahisishe kusema sihatari kufanya kazi under ground mine. Midhani mazingira ya U/G ni hatarishi kuliko watanzania wengi wanavyo amini au kuaminishwa.
VIHATARISHI:-
1-Joto kali
2-Vumbi laini
3-Giza totoro
4-Kelele za kupita kiasi
5-Mashine huko ardhini
6-Miamba legevu
7-Matumizi ya lifti
9-Upungufu wa oksijeni
10-Kutembea kwa miguu
Namengine meeeengi mkuu
 
joto la zone 9-3946 ni hatari...mtu anamwaga maji kwenye buti hata lita nzima sababu ya jasho overall unakamua kama unataka kuanika sababu ya joto
 
Sorry wakuu actually kwa maana ya kuuwa sana lakini hata hivyo athali zake huwa ni muda mrefu na hazitibiki.anyway ni hatari mkuu hata mimi huwa nagombana na mabosi wangu kwenda kufanya kazi hata ya muda.
joto la zone 9-3946 ni hatari...mtu anamwaga maji kwenye buti hata lita nzima sababu ya jasho overall unakamua kama unataka kuanika sababu ya joto
 
Nlivomaliza chuo nlikua matamani sana kufanya kazi hapo mgodini kakola,bro wangu mi mfanyakazi anafanyakazi hapo na anacheo kidogo,alinikatalia katakata kufanya kazi hapo,alinichukiza sana na kwa bahati mbaya akua na sababu za msngi za kunizuia..ila sasa nmeanza kumuelewa taratibu....

Nenda kapige kazi wewe achana na braza ako sometym hataki kuona unafanikiwa, bulyanhulu kuna kazi za kada tofauti tofauti sio lazima uwe miner. Kwani chuo umesomea nini?
 
Nenda kapige kazi wewe achana na braza ako sometym hataki kuona unafanikiwa, bulyanhulu kuna kazi za kada tofauti tofauti sio lazima uwe miner. Kwani chuo umesomea nini?

ni vigumu kupata kazi uliyosomea watu wengi wanaanzia na u Miner lattet huwa ni vyepesi kupanda juu...mbona mimi nimekuwa miner kwa miaka 3 wakati huo nilikuwa graduate Ventilation Engneer...mwaka jana ndo nikapanda kwenye kada yangu
 
Back
Top Bottom