BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,144
Mfanyabiashara aua majambazi watatu
Hellen Mlacky, Moshi
Daily News; Tuesday,June 24, 2008 @00:03
Majambazi watatu, akiwamo raia wa Kenya wameuawa kwa kupigwa risasi na mfanyabiashara waliyekuwa wakipora katika baa yake juzi usiku. Kwa mujibu wa Polisi majambazi wengine watatu walikimbia na fedha walizokuwa wamepora na kutokomea pasipojulikana na kutelekeza mali nyingine walizokuwa wameiba baada ya kushambuliwa.
Wanadaiwa walikuwa tishio kwa kuwavamia wateja katika baa mbalimbali na nyumba za kulala wageni katika maeneo ya Marangu na kuwapora mali zikiwamo simu za mkononi na fedha.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Ramadhani Baruti, aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa tatu usiku katika eneo la Mamba Kiria, wilayani Moshi Vijijini.
Alisema kuwa usiku wa tukio hilo majambazi sita wakiwa na bastola walivamia baa ya Market View mali ya Erick Shayo (40) na kuwaweka wateja chini ya ulinzi huku wakifyatua risasi hewani.
Wateja walitii amri na kuamriwa kutoa mali walizokuwa nazo, wakapora kaunta na baadaye katika vyumba vitatu vya wageni. Baruti alisema kuwa baada ya majambazi hao kutekeleza azma yao kwa nusu saa waliondoka kwenye baa hiyo na kwenda baa ya Egbert Maleko ambako mauti yaliwakuta.
Kaimu Kamanda huyo alisema kuwa wakati majambazi hao walipowaweka wateja chini ya ulinzi, Maleko alipata upenyo na kukimbia nyumbani na kuchukua bunduki yake aina ya shotgun yenye risasi nane na kuwashambulia majambazi, kwanza kwa kumpiga risasi ya shingoni aliyekuwa na bastola aliyeanguka chini na kuiachia, akampiga mwingine usoni hadi akadondoka nje ya baa na wa tatu alipigwa risasi makalio.
Alisema kuwa baada ya majambazi hao kupekuliwa mmoja alikutwa na kitambulisho cha Kenya chenye namba 4899725 kilichotolewa Machi 27 mwaka 2001 huko Uasingishu, Loitoktok. Polisi wanasema alikutwa na bastola aina ya Beretta yenye namba 642206 ikiwa na risasi sita.
Majambazi wengine hawakutambuliwa majina wala uraia wao na wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 na 40. Polisi inamshikilia Honest Fares Moshi (29), mkazi wa Mamba Marangu kwa mahojiano zaidi kwa kuhusishwa na tuhuma za tukio hilo na kuendelea kuwasaka wengine waliokimbia.