Mfanano wa taarifa za habari za ITV na UTV (Azam). Je, kuna kuvujishiana habari ili kuimarisha Ushindani?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,231
6,471
Ukiondoa TBC, taarifa za habari za saa mbili usiku za ITV na UTV zinafanana karibia kila kitu. Habari zinazotangazwa ni zilezile.

Kuna habari sio mbaya kufafanana kama vile habari iliyotoka kwa Rais, Mawaziri nk. Sasa shida ni kufanana hadi habari ndogondogo. Katika zama hizi za upatikanaji habari nyingi kwa njia rahisi ni Jambo la kushangaza kwa vyombo vya habari kufanana habari hizohizo.

Je, kuna uwezekano kuna chombo kwa kujihami imeamua kuhakikisha inapata taarifa zote za upande wa pili ili kuvuna wafuasi na wapenzi wa chombo chenzake?
 
Haina shida mkuu ilimradi zote kama zina maudhui muhimu.
 
Ndo maana siangaliagi taarifa za habari kwenye Tv zetu. Bora JF Unapata news with balanced editorial contents na comments.
 
Itv ni maarufu muda mrefu sana!! Na labda inaangaliwa zaidi saa mbili kamili usiku!!
 
Mara nyingi waandishi wa habari huwa wanashare taarifa, pia hata usafiri huwa wanatimia gari moja. Kukiwa na tukio kigoma waandishi wa ITV, AZAM, TBC etc waambiana wote wanaenda kwenye tukio pia watu wana wa waoji kuhusu mada wote wana moji huyoyuyo, ndo maana ukiona mtu anaingea unaona mic za itv azam etc
 
Kinachonikera upo Bar ya mtaani unakunywa bia anakuja mnywa maji analilia habari ambayo angeangalia nyumbani kwake na mke
Hiyo inaudhi sana, halafu ukute mtu umeshakunywa safari kubwa 8 kisha mtu na vimaji vyake vya 1000 anataka mtazame habari. Mkimwambia ukweli anaanza kuwasimanga na bia zenu.
 
Hiyo inaudhi sana, halafu ukute mtu umeshakunywa safari kubwa 8 kisha mtu na vimaji vyake vya 1000 anataka mtazame habari. Mkimwambia ukweli anaanza kuwasimanga na bia zenu.
Watu tumekuja kulewa sio kuona mtu mmoja ametumbukia chooni
 
Ukiondoa TBC, taarifa za habari za saa mbili usiku za ITV na UTV zinafanana karibia kila kitu. Habari zinazotangazwa ni zilezile.

Kuna habari sio mbaya kufafanana kama vile habari iliyotoka kwa Rais, Mawaziri nk. Sasa shida ni kufanana hadi habari ndogondogo. Katika zama hizi za upatikanaji habari nyingi kwa njia rahisi ni Jambo la kushangaza kwa vyombo vya habari kufanana habari hizohizo.

Je, kuna uwezekano kuna chombo kwa kujihami imeamua kuhakikisha inapata taarifa zote za upande wa pili ili kuvuna wafuasi na wapenzi wa chombo chenzake?
Binafsi nikipitia Jamii Forums, Jukwaa Ia siasa, habari mchanganyiko, kimataifa na mapenzi, habari za ITV au Azam na tv zingine huwa ni rivission tu, kwasabb yote nakua nimeyashajua...
 
Back
Top Bottom