Mfalme Zumaridi akamatwa na Polisi Mwanza

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,398
Reaction score
14,520

Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linapenda kutoa taarifa kuwa leo tarehe 15.05.2025 majira ya saa nne asubuhi huko mtaa wa Buguku, kata ya Buhongwa, wilaya ya Nyamagana, limemkamata na linaendelea kumhoji Diana Edward Bundala ambaye pia hujitambulisha kwa jina la Mfalme Zumaridi, miaka 42, mkazi wa mtaa wa Buguku, kata ya Buhongwa, ambaye ameyageuza makazi yake kuwa kanisa, anatuhumiwa kuendesha shughuli za kidini bila usajili pamoja na kufanya mahubiri kwa waumini wake kwa sauti ya juu katika eneo hilo ambalo ni makazi ya watu na kusababisha usumbufu kwa majirani wanaoishi karibu na makazi yake.

Aidha, mwanamke huyo anahojiwa kuhusiana na taarifa inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii akionekana kwenye picha mjongeo akiwa na kundi la watoto wenye umri mdogo wa jinsia ya kike na kiume akiwaeleza kuwa yeye ndiye Mungu wao ambaye ana uwezo wa kuwatenganisha na kifo.

Uchunguzi kuhusiana na tukio hili unaendelea, Jeshi la polisi katika uchunguzi huo litashirikiana na taasisi nyingine za serikali; hivyo linawaomba wananchi wenye taarifa mbalimbali zinazoweza kusaidia uchunguzi wa tuhuma hizi wafikishe kwa Jeshi la polisi. Uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zinazostahili zitachukuliwa.

IMG_4878.jpeg
 
Kwan walivyomkamata kwa mara ya kwanza wakati ule ikawaje akawashinda kesi. Na serikali inashindwaje kumdhibiti yule binti? Si wapoge utepe hilo eneo mwaka mzima.
 
Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linapenda kutoa taarifa kuwa leo tarehe 15.05.2025 majira ya saa nne asubuhi huko mtaa wa Buguku, kata ya Buhongwa, wilaya ya Nyamagana, limemkamata na linaendelea kumhoji Diana Edward Bundala ambaye pia hujitambulisha kwa jina la Mfalme Zumaridi, miaka 42, mkazi wa mtaa wa Buguku, kata ya Buhongwa, ambaye ameyageuza makazi yake kuwa kanisa, anatuhumiwa kuendesha shughuli za kidini bila usajili pamoja na kufanya mahubiri kwa waumini wake kwa sauti ya juu katika eneo hilo ambalo ni makazi ya watu na kusababisha usumbufu kwa majirani wanaoishi karibu na makazi yake.

Aidha, mwanamke huyo anahojiwa kuhusiana na taarifa inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii akionekana kwenye picha mjongeo akiwa na kundi la watoto wenye umri mdogo wa jinsia ya kike na kiume akiwaeleza kuwa yeye ndiye Mungu wao ambaye ana uwezo wa kuwatenganisha na kifo.

Uchunguzi kuhusiana na tukio hili unaendelea, Jeshi la polisi katika uchunguzi huo litashirikiana na taasisi nyingine za serikali; hivyo linawaomba wananchi wenye taarifa mbalimbali zinazoweza kusaidia uchunguzi wa tuhuma hizi wafikishe kwa Jeshi la polisi. Uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zinazostahili zitachukuliwa.

View attachment 3334876
Huu ndio utaratibu unaotakiwa, sio kukwapua
 
Jirani nasikia ni Waziri fulani....ndio maana vita ni kubwa.
 
Mbona mwamposa hakamatwi?
Kwani kuna tofauti kati yao???
Tunakumbatia vitu amavyo vinatrudisha nyuma wazungu wakija kuona kiwanda cha nyama kimwekuwa sehemu ya ibada. Tunaishi maisha ambayo ulaya ilipitia miaka 400 iliyopita. Leo hii wako serious na utamaduni wao wa utu na ubinadamu.
 
Back
Top Bottom