aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
775
1,117
Nchi ya Tanzania imekuwa ikiongozwa na chama cha CCM katika kipindi kisichopungua miaka 50,Tanzania hii imepiga hatua za kimaendeleo kwa vipindi kutofauti kutoka kwa rais mmoja kwenda kwa rais mwengine katika vipindi vya miaka mitano yenye vipindi viwili kwa kila mmoja huku sera zikiwa ni kutoka katika chama kimoja ila tofauti ni namna katika maono na njia za viongozi hawa katika kufikia mafanikio yaliyo yakweli.

Vimepita vipindi vingi tofauti vya uongozi lakini rais Samia Suluhu Hassan ameweza kujipambanua katika aina yake ya uongozi huku akitaka utii wa sheria na katiba ya nchi kila mmoja wetu akiwajibika katika majukumu yake na taaluma yake kwa haki na uadilifu

Rais Samia ameweza kutekeleza vyema sera ya viwanda chini kwa kukaribisha wawekezaji katika sekta muhim ambazo zimekua na changamoto nyingi nchini mfano Sekta ya kilimo na afya
Kwakutambua kwamba pesa ya serikali ni kwa ajili ya kuwapatia wananchi huduma za msingi na kutekeleza miradi ya kimkakati Rais Samia ameweza kuisaidia pakubwa Serikali yake katika kuokoa pesa ambayo ingetumika kuwekeza katika ujenzi wa viwanda na kuiachia sekta binafsi ifanye biashara na kutoa ajira binafsi kwa wananchi

Jana tarehe 23/4 nchi ya Tanzania chini ya utawala wa Rais Samia imeshuhudia utiwaji sain wa mikataba 7 ya kibiashara yenye thaman ya trilioni 11 za kitanzania baina ya wafanyabiashara wa Marekani katika sekta ya Afya,kilimo,Utalii na nyenginezo ambayo itatoa ajira zipatazo 301,110 hii ni kwa mara ya kwanza

Ni katika awamu ya rais Samia pekee tumeshuhudia katika maonyesho ya dubai export 2020 Tanzania imeshuhudia utiaji wa sain mikataba yenye thaman ya Tsh trilion 17.35 ambapo ajira zaid ya 200,000 zitazalishwa katika kipindi cha miaka minne

Kwa ujumla rais Samia amefanikiwa pakubwa katika kusisimua uchumi wa nchi na kutekeleza kwa vitendo dhana ya uchumi na uwekezaji nchini,naiona Tanzania ikipiga hatua kubwa za kiuchumi chini ya utawala wa Samia kama vile ilivyo nyanyuka Marekani baada ya vita vya pili vya dunia

Ujenzi wa miradi ya maji kwa kasi,afya,elimu pamoja na kuendeleza miradi mikubwa ya kimikakati ni jambo moja kubwa linalo akisi uongozi thabit na maono yaliyo bora ya rais Samia kwani ameweza kuthamin juhudi za mtangulizi wake na kuithamin pesa ya serikali kwa kuto kutekeleza miradi

Ni jukumu letu kumuunga mkono rais Samia katika azma yake kubwa ya kuleta maendeleo na kuibua uchumi wa nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom