Mfahamu Fernando Arajulo mpanga mikakati katika uvamizi wa benki ya Banco Rico Arjentina

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
KUTOKA MAKTABA.

Mimi binafsi ni mpenzi wa kusoma sana historia.Ngoja nikupe historia ya wizi wa benki ulitokea nchini Arjentina.

MPANGO ULIVYOPANGWA.
Kundi la watu hawa walikuja na wazo mwezi wa kwanza mwaka 2006, ambao uliruhusu wao kuwapoteza polisi kipindi wanavyovamia benki ya Banco Rico mjini Acassuso nchini arjentina. Wezi wa benki walichukua miaka miwili kujipanga.
Kabla ya tukio mtu aliyeitwa Julian Zalloecheverìa alifatwa na rafiki yake Beto de la Torre kuungana na kundi lingine lililoitwa Super bandas,kundi hili lilidhamiria kuiba sefu boksi za kuhifadhi pesa kutoka ndani ya benki ya Banco Rico jijini Acassuso.

Fernando Arajulo,
alikuwa mpanga mikakati na mchora ramani nzima( mastermind) nyuma ya mpango huu.alikuwa na jukumu la kuwaandaa wezi halisi watakaofanya tukio. Mpango huu ulijumuisha kutengeneza njia za chini zitakazoelekea mpaka ndani ya benki. Njia za chini kwa wavamizi zilikuwa sehemu muhimu kwenye mpango na fedha zilizotumika.njia hizi zilitengenezwa na mshiriki aliyeitwa Sebastian Garca Bolster.


Ila njia hizi zilitengenezwa kwa kutoingilia ndani ya benki, kuingia ndani wavamizi wangeenda moja kwa moja kupitia mlango wa mbele na kuchukua watu wa ndani mateka, na katika mchakato wa kuhakikisha mamlaka zinajua wavamizi wa benki wapo ndani na hapa ndipo mpango ulipopangwa.

Kwa kuingia ndani ya benki kupitia mlango wa mbele na kukamata watu kama mateka ndani ya benki, walipanga kutengeneza hali ya kununua muda kwa kuendelea kuzungumza na polisi, ila kutumia njia za chini kama njia za kutorokea!
Wavamizi wa benki walikuwa katika mchakato pindi mamlaka ilipopokea simu saa 12:38 mchana mwezi wa 1/2006, muda mchache baadae Polisi walizingira benki pande zote. Mlinzi wa benki ndiye alikuwa wa kwanza kuachiwa huru na akatoka akiwa na silaha yake, pindi mamlaka ilipokuwa ikijipanga mlinzi akasema “kuna mateka wengine ndani”

Dakika 10 baadae kijana mdogo aliachiwa , mvamizi aliyevaa maski usoni alionekana mlangoni akimuachia mateka mwingine muda huu alionekana ni mwanamke, halii hii ilionyesha utulivu na kutambua kwamba wavamizi hawa wanataka mazungumzo.

Ndani ya benki kulikuwa na wavamizi watano, walikuja na nguo kama wachoraji, wezi wawili walivaa ma sweta ya kufunika kichwa, mmoja alivaa kama daktari, mwingine alikuwa mdogo zaidi, mwingine alivaa wigi la rangi na alijulikana kama Susana.
Mmoja mwenye nguo za greyi alionekana kuwa na ujasiri sana, kutokana na hali iliyokuwepo,hakuonekana kuogopa Polisi 200 waliokuwa wamewazingira kila sehemu.
Ghafla akawapa taarifa polisi nje akiwaonya kwa sauti “ waambieni watu mliowaweka juu ya maghorofa waondoka vinginevyo tutaua mateka mara moja”. Safari zaidi ya masaa nane ilianzia hapa.


Mateka wapatao 23 walishikiliwa kwa siku nzima mjini Acassuso katika benki ya Banco Rico.siku nzima mamlaka ilikuwa inajadili mbinu ya kuokoa mateka na kumaliza tatizo hilo. Ila muda kadri ulivyoenda ukimya uliendelea ndani ya benki, wakawa wanashangaa wavamizi watakuwa wanawaza nini?

Walipata ugumu kuhisi hali halisi iliyokuwa ndani, mateka walikuwa wakila pizza na soda ambazo wavamizi waliomba kutoka kwa polisi, na walikuwa wakiimba wimbo wa siku ya kuzaliwa kwa mmoja wa mateka aliyeko hapo, ila hapakuwa na dalili za wavamizi.

Polisi walipochoka ukimya huo na kuchunguza nini kinaendelea, wakakuta mateka tu na barua iliyosema “MSIUMIE SANA”


Wezi wametumia njia ya chini sio kuingilia ila kutokea nje ya benki, wameshuka kupitia mifereji ya maji machafu na wamekimbilia chini kwa boti za mipira.

Katika historia hii ya Fernando Arjalo kama mastermind inakadiriwa kiasi cha $8 milioni kutoka katika sefu boksi 145 za kuwekea pesa ziliibiwa katika benki ya Banco Rinco jijini Acassuso nchini Arjentina.

Nitamalizia jinsi walivyokamatwa.
 
Back
Top Bottom