Mfahamu David Kihenzile, Naibu Waziri Mpya wa Uchukuzi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945
Na; Thadei Ole Mushi.

Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na Manaibu Waziri yaliyofanywa siku sita zilizopita yanatoa somo kwenye mambo mawili makubwa.

1. Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuachana na Mawaziri na Manaibu Mawaziri ambao aliwarithi toka kwenye awamu zilizopita. Maingizo ya watu wapya nje ya mfumo wa JPM na JK yanatoa somo kuwa walioaminiwa toka kwenye awamu hizo wanatakiwa wachape kazi kweli kweli. Kuna somo moja tunajifunza toka kwa Rais Magufuli alipoingia madarakani aliamua kutafuta Personalty Mpya kabisa akaziingiza kwenye mfumo wa Baraza la Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Ma Dc, Wakurugenzi na kwenye maeneo mengine ya kiutendaji. Faida kubwa ya kutengeneza watu wapya ni kuwa wanakuwa waaminifu sana kwako (Loyal) na hawatataka kukuangusha. Tafuteni watu kama Kina Makonda, Polepole, Ole Sabaya, Dr. Bashiru, Prof Kabudi na wengine ambao walitoka nje ya mfumo uliokuwepo kabla uone walivyokuwa loyal kwa Magufuli. Hizi teuzi mpya hazitamwangusha Mama labda wakose uwezo wa kiakili.

2. Tafsiri ya pili inayojitokeza hapa ni kuwa kutokana na haya maingizo mapya Waliokuwa wamezoea kila Mara kujisoma kwenye mkeka ni kengele ya tahadhari kuwa waongeze ubunifu, waongeze juhudi na waache mambo ya kutamani Uraisi siku zijazo vinginevyo watapukutika wote kabla ya 2025. Kwa sasa Mheshimiwa Rais yupo very Defensive anawafuatilia kwa ukaribu sana.

Anyway, Mhe. David Mwakiposa Kihanzile ni nani?

Kwanza, Ninawiwa sana kuchambua hizi personality mpya ili muwafahamu na muone kuwa wana uwezo mkubwa kuliko hata waliokuwepo na bado wapo wengi tu.

1. David Mwakiposa Kihanzile ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini

2. Mwaka 2020-2023 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira.

3. Mwaka 2023 Kamati ziliiunganishwa na kuunda kamati nyeti na nzito ya Viwanda, Biashara, Kilimo & Mifugo akachaguliwa tena kuwa Mwenyekiti

4. Mwaka 2021 Aprili alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge na mwaka 2023 alichaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Bunge akimsaidia Mheshimiwa Spika kuongoza Bunge.

5. Mhe. David Mwakiposa Kihenzile Ni Rais wa Reedcross Tanzania, Redcross aliingia kuwa Rais akiwa na miaka 35 tu. Ndiye Rais mdogo kuliko wote Duniani, Waliowahi kuwa Marais hapo ni pamoja na Makam Mwenyekiti wa CCM Mzee kinana, na Mwenyekiti wa Mkoa Dodoma Adam kimbisa

Akiwa RedCross Amefanya mambo yafuatayo:-

1. Wanachama na Voluntia wameongezeka toka 3,000 mwaka 2019 hadi 400,000 mwaka 2023.

2. Miradi imeongezeka zaidi na wafadhili kuongeza imani zaidi kwa Nchi,

3. Mahusino na Serikali yameongezeka zaidi na zaidi na taasisi ya Redcross.

Jimboni aliingiaje na kafanya nini?

Aliongoza kura za maoni Jimbo la Mufindi Kusini na wananchi kumchagua kwa 97.3% na kumfanya kuwa Mbunge aliyepata kura nyingi zaidi Nyanda za juu Kusini. Aliwashinda wagombea wa CDM na ACT

Alipoingia Kero kubwa ilikuwa ni ukosefu wa barabara za lami na Maji. Kwenye Maji alikuta Vijiji 5 tu na kwa Miaka 2 amepata miradi kwenye Vijiji 65 kati ya 71 vilivyopo bado Kijiji kimoja. Barabara za lami za MAFINGA kwenda MGOLOLO zimeshasainiwa na mkandarasa anatarajiwa kuanza kazi. Ile ya NYOLOLO MTWANGO Mkandarasi yuko site, na pesa zinaletwa zaidi aendelee ujenzi. Barabara za MAFINGA MAKAMBAKO na IGOWOLE KASANGA NYIGO zimewekwa kwenye mpango wa usanifu wakina ili 2025/20230 ujenzi kiwango cha lami uanze. Barabara ya lami ya kutoka Sawala mpka Ikaning'ombe km 30 imekamilika na sasa ujenzi umeanza kutokea ukaning'ombe hadi Luanda.

Pia, kwa muda huu mfupi kafanya yafuatayo, serikali imetenga pesa ujenzi kituo cha Afya cha Mgololo, kituo cha afya itandula na kituo cha afya Mtwango na kile cha Mninga, jumla vinne.

Ujenzi wa chuo cha VETA umeanza, na pia serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuanza kiwanda cha parachichi.

Jambo lingine na Kufurahisha kwa Kihanzile ni kuwa alifanikisha Dili la World Vision kugawa Mitamba ya Ng’ombe kwa wananchi kama walivyofanya Rwanda 2006 kwenye mradi wa Girinka kwa kuwasaidia wananchi kupambana na umaskini badala ya kuwaandikisha kwenye TASAF.

ELIMU
Kielimu ana Shahada ya Uzamili ya ya Utawala Katika Biashara (Masoko) na Stashahada ya uzamili ya Mahusiano ya Kimataifa kutoka Chuo cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar esa Salaam. Kwa sasa anasoma PhD UDOM na anamalizia masomo ya shahada ya kwanza ya Sheria.

Jambo la Kufurahisha kwa Kihanzile kwenye Elimu ni kwamba akiwa O level pale Mbozi Mission katika wanafunzi 122 waliomaliza naye kidato cha nne ni yeye Peke yake aliyepata One na akapangwa Mzumbe High School.

All in All Mufindi kisiasa ilikuwa haijulikana sana lakini uwepo wa Kihanzile Pale Mufindi imejitambusha sana Tanzania.

Ole Mushi

E1LB9WDXsAEHYM4.jpg
 
Safi, kuna watu hata ukisoma CV zao unaona kabisa ni watu makini pia wana sifa ya kutuongoza sasa sijaelewa kabisa nini huwa kinawabadilisha kabisa kwasababu kuna mmoja huyo alithibutu kutufukuza kabisa wizarani ila kabla akiwa mbunge alikuwa msaada wetu mkubwa jimboni kwake.
 
Wengine walisema kwanini hakugombea kule Ipinda? Maana kakuzwa zaidi kule.
 
View attachment 2744075
Okay. Yupo Chama gani?
 
Back
Top Bottom