Mfahamu Black Alien: Mtu mwenye ndoto ya kufanana na viumbe vya ulimwengu mwingine (Aliens)

Unapojaribu kuandika ujinga kuwa makin ktk uandishi wako kusiwepo na maneno yenye shaka juu ya wenye mbongo zao, kipengere kwa ana karibu karne tangu aanze kujibadilisha maake ni kuwa atakuw na miaka zaidi ya mia ukiunganisha na umri wa utoto akiwa hajawa na maamuzi yake mwenyew yaan mtu mzima kiumri, kiakili n.k
Wewe mkuu hujaelewa kilichoandikwa ukaanza tu kumshambulia mwandishi! Hapo alipoandika neno karne, anamaanisha huyo black alien ndiyo mtu aliyejifanyia mabadiliko makubwa ya mwili kuliko mwingine yeyote katika karne hii. Hamaanishi kuwa jamaa kaishi karne nzima. Unajivua nguo mkuu, soma kwa makini kabla ya kutukana.
 
We umekuja kusoma huo uzi ushafanyiw marekebisho ya kiuandishi so tulia tu, na huo ukosoaji wangu na bujibuji ndo sabab kauedit huo uzi
 
Mtu anajiharibu unasema anajifanyia maboresho. Kwahiyo hapo ni namna ya kuonekana bora zaidi au ?!
 
Mwisho atajiua!

Michael Jackson naye alijibadili sana, lakini mpaka anakufa alikuwa anaonekana bado ana mfadhaiko wa akili.
Michael Jackson hakufanya kwa kusudi la kujibadilisha. Alikuwa na tatizo la Vitiligo, alikuwa anatunia madawa ili kuzuia ile ugonjwa ndo dawa zikabadili ngozi yoote
 
Kweli nimeshindwa kuanzisha mimi sabb ni kuwa nina akili timam sio tahira km wew, mada km hii yahitaji mafyatu km wew. Pili nimekosoa uandishi sabb haujapangiliwa kiakili kiasi kwamba mtu akisoma hata wa akili ya kawaida anagundua makosa, unajua ni kwann hadi wew umeshindwa kung'amua nini nilichomaanisha? Sabab ni huo utindio wa ubongo ulionao wa asili
Muhimu content,usahihi kwani anafanya mtihani?

Pia haujalazimishwa kusoma..pita nenda!
 
View attachment 2025735

Anthony Loffredo pia anajulikana kama black alien. Anashikilia rekodi ya mtu aliyejifanyia maboresho mengi makubwa kabisa katika mwili wake kuliko binadamu mwingine kwa karne hii.

Ameendelea kushika vichwa mbalimbali vya vyombo vya habari kwa ujasiri wake kwa kuamua kutenganisha kati ulimi wake, kukata masikio, kutapakaza tatoo toka kichwani mpaka kwenye nyayo, kujitoboa na mwili kwa kuongeza vyuma na hata kukata pua. -- Mpaka sasa amesha fanikisha maboresho muonekano kiupasuaji 34%.
View attachment 2025738

Mwanaume huyu mwenye umri wa miaka 33 sasa, kutoka Ufaransa amejidhamiria haswa katika ndoto yake ya kufanana na elieni "black elien". Kwa sasa sio mgeni katika meza za uparation tena. Hivi karibuni aliamua kufanya maboresho zaidi kwa kuondoa vidole vyake viwili ili kufananisha na ukucha haijatosha alishatoa pia hata mdomo wake wa juu kwa siku zilizopita mapema mwaka huu.
View attachment 2025742
Anthony - amekuwa akijifanyia mabadiliko mwilini kwake karibia miaka kumi sasa - amekuwa jasiri hata kujaribu kuchora tatoo kwenye jicho pamoja na kujua angeweza kupofuka.

Mwaka jana, Anthony alisafiri kwenda Spain kufanya uparasheni ya kuondoa pua kwa sababu aina hizo za uparasheni ni kosa kwenye nchi yake.
View attachment 2025743

Ana matumaini ya kupunguza uonekano wa kibinadamu, pia alishapandikiza vipandikizi kwenye uso vinavyoipa ngozi yake muonekano wa vinundu pia na muonekano wa reptilia kwenye paji la uso na alama ya mpasuko kukatiza kwenye mfupa wa shavu.
View attachment 2025744

Anthony anasema ndiyo kwanza yupo hatua ya tatu katika mabadiliko yake anayoyategemea.
Katika maboresho yake ya hivi karibuni alisikika akisema " najitengenezea amani yangu ya ndani."

View attachment 2025748
Huyu ameshafika kwenye kiwango cha juu kabisa cha uwendawazimu (ugonjwa wa akili). Hivi hata hao madaktari wanaomfanyia upasuaji wanakubali vipi kufanya upasuaji wa mabadiliko ya mwili kwa kiwango cha kumbadilisha mwonekano wake wa asili kwa kiwango kikubwa namna hiyo?
 
Dunia ya sasa inaendeshwa na pesa. Ukiwa na pesa hakuna linaloshindikana. Tafuta pesa mkuu utakuja kunielewa.
 
Huyu ameshafika kwenye kiwango cha juu kabisa cha uwendawazimu (ugonjwa wa akili). Hivi hata hao madaktari wanaomfanyia upasuaji wanakubali vipi kufanya upasuaji wa mabadiliko ya mwili kwa kiwango cha kumbadilisha mwonekano wake wa asili kwa kiwango kikubwa namna hiyo?
Hio ni biashara mkuu,we hujiulizi kwanini wenye baa huwa wanamuuzia mtu pombe wakati huo hata kusimama hawezi lakini analetewa tu
 
Back
Top Bottom