Mwenye kujua tafsiri ya hii ndoto jamani anisaidie: Hivi ukiota unamkimbiza mtu maana yake nini?

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,142
Salam wakuu, naimani humu nyote ni wazima wa afya na mimi pia na mshukuru Mungu mzima kabisa japo harakati ngumu ila sichoki kumshukuru Mungu kwa kila hali.

Turudi kwenye mada jana usiku wakati nimelala kuna ndoto ikanijia na hii ni mara yangu ya kwanza kuota ndoto ya namna hii nashindwa kuelewa hii ndoto ilikuwa inaamaana gani

Iko hivi kwenye ndoto nilijiona natoka nyumbani mlangoni wakati nafunga mlango ili niende zangu nje kwa mbali nikaona mtu kavalia kanzu nyeupe cha kushangaza usoni alikuwa mweusi tii na ana macho makubwa mekundu kiasi cha kuogopesha wakati naendelea kumshangaa ghafla nikaona anaanza kunisogelea mimi nikaanza kutoa sauti za vitisho kumtishia na kumuuita wewe na nani na unataka nini.

Nikaona amesimama nami nikaanza kumsogelea na kumhoji ghafla nikamuona anaanza kukimbia nikaamua nami nianze kumkimbiza. Akawa kila akifika mahali anasimama then ananiangalia kwa nyuma kisha nikiwa karibu nae anaendelea kunikimbia.

Akafika sehemu kama kuna kona ya nyumba hivi alivyokata ile kona nami wakati naisongelea ile kona nyumba ghafla nikamuona amesimama huku ananiangalia tukakutana uso kwa uso then nikastuka usingizi.

Dah aisee kuja kustuka ilikuwa ishafika alfajiri saa 11 hivi nikashindwa kulala kabisa.

Mimi naamini katika ushirikina lakini linapokuja suala la ndoto ya namna hii nashindwa kuielewa, mwenye kujua maana ya hii ndoto anaweza kunisaidia?

Natanguliza shukurani wakuu
 
Unapokaa kodi umelipa?
Wenye nyumba tabia zao hizo akiona unamcheleweshea pesa yake
Kodi nalipa kwa wakati tena kila baada ya miezi mitatu kodi inaisha mwezi huu wa kumi. Tarehe 1 Mwezi ujao natakiwa kulipa.
 
Kama huangaliag m video ya TikTok bas Ongeza juhud kwenye jambo lako na vaa ujasir
Mambo ya tiktok huko bado sijayafahamu vizuri maana mimi si mtumizi sana wa huu mtandao. Ila asante kwa ushauri ngoja nitaenda kuyafuatilia haya mambo ya ndoto huko tiktok
 
Katika ulimwengu usioonekana kuna muhuni anakufanyia visa flan flani kama kukutishia
Nashangaa sana hili jambo apa ninapoishi naishi sijawahi kugombana na majirani hata mmoja kiufupi najitahidi sana kuishi vizuri na watu salamu natoa bila shida japo sipendi mazoea na watu. Sasa huyu anayetaka kunitisha kiroho sijui ana dhumuni gani kwangu nashindwa kuelewa mkuu
 
Wewe unanguvu za Rohoni za kushinda...

Kifupi umemshinda adui ..

Endelele kuomba ..

NB: unaweza ukawa na nguvu za giza za kumshinda adui au za Mungu...
 
Nashangaa sana hili jambo apa ninapoishi naishi sijawahi kugombana na majirani hata mmoja kiufupi najitahidi sana kuishi vizuri na watu salamu natoa bila shida japo sipendi mazoea na watu. Sasa huyu anayetaka kunitisha kiroho sijui ana dhumuni gani kwangu nashindwa kuelewa mkuu
Kwani mtu mbaya huwa anajali umemfanya nini, tena mwingine anakuwa rafiki yako kabisa lakini anakusumbua tu, wewe rudibkwa Mungu wako atakuonyesha au kukupa tafsiri yake.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Wewe unanguvu za Rohoni za kushinda...

Kifupi umemshinda adui ..

Endelele kuomba ..

NB: unaweza ukawa na nguvu za giza za kumshinda adui au za Mungu...
Shukurani ngoja niendelee kuzidisha ibada zangu pengine ni maadui wameshaanza visa
 
Ni Jinn hilo linatafuta jinsi ya kuingia mwilini kwako sijajua ni zuri au baya,ila naona ni Jinn mbaya Ruhani angekujia na sura nzuri sio ya kutisha na mpaka unamkimbiza sio mzuri. kitu pekee nacho kushauri ni maombi Ibada sana kwa mujibu wa dini yako,jinn awe mzuri au mbaya akiingia kwenye maisha yako lazima akupe misusuko ndo akae sawa halafu kama mbaya ndo atakupa shida mpaka UTASEMA,inaonekana uko vizuri ndo maana umemkimbiza endelea kufanya unachofanya kama maombi zidisha.
 
Hakun huko n nmesem coz mostly n comedian moves za tiktok so if hujawah bas ujumbe nmekupa take it or leave it
Mambo ya tiktok huko bado sijayafahamu vizuri maana mimi si mtumizi sana wa huu mtandao. Ila asante kwa ushauri ngoja nitaenda kuyafuatilia haya mambo ya ndoto huko tiktok
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom