Meya Manispaa ya Moshi amelikoroga, aunga mkono ushoga

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
B81BFA40-AC3A-4DB8-B384-443F12394682.jpeg


Hali si shwari ndani ya baraza la madiwani la Manispaa ya Moshi ambako madiwani wamekuja juu wakimtaka meya wao, Juma Raibu kujiuzulu fasta baada ya clip moja kusambaa mitandaoni ambako amesikika akiunga mkono mapenzi ya jinsia moja.

Juma Raibu anadaiwa wiki iliyopita alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa mwanaumme mmoja aliyeko kwenye mapenzi ya jinsia moja hapo mjini Moshi na katika salamu zake amenukuliwa akiunga mkono mapenzi hayo na kusisitiza Manispaa ya Moshi iko tayari kulinda haki zao na kwamba itawapa ushirkkiano katika kudi haki zao.

Hii iliwaibua madiwani hao na wakambana vilivyo kwenye kikao cha maandalizi ya baraza la madiwani (Pre Council) kilichokuwa na madiwani wengi wa CCM wakimtaka aachie ngazi kwa kile walichodai amewadhalilisha madiwani na baraza zima la madiwani lakini moto ulizisi kuwa mkali kiasi cha madiwnai hao na meya wao kurushiana maneno mazito yaliyopelekea baadhi ya madiwani hasa wanawake kutoka nje ya kikao.

"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku zote imekuwa haiungi mkono mapenzi ya jinsia moja leo meya anatoa wapi nguvu ya kuunga mkono mapenzi hayo? Kwa kweli hili limetudhalilisha sana sisi madiwani na njia sahihi kwa meya ni kuachia ngazi?,"amesikika diwani moja alipowatonya wanahabari jana wapohudhuria kikao cha baraza la madiwani.

Kutokana na kasheshe hilo, jana madiwani wote wanaotokana na CCM waliitwa kwenye kikao cha ndani ofisi ya CCM Manispaa ya moja na katibu wa CCM manispaa hiyo Ibrahim Mjanaheri kikao kilichofanyika saa nane mchana mara baada ya kikao cha baraza la madiwani kumalizika kwa lengo la kwenda kutliza hali ya hewa.

Hata hivyo leo tena mara baada ya kikao cha barza la madinwai kilichoketi kwa siku mbili jana na leo, madiwani ihao mpaka muda huu wapo kwenye kikao cha ndnai ofisi ya CCM mkosa kikao ambacho kipo chini ya katibu wa CCM mkoa, Jonathan Mabihya leo ni hilo hilo la ktuliza mabo ambayo kwa kwlei yanakwenda kombo.

Hadi muda huu kikao cha madiwani hao na viongozi wa CCM mmkoa kinaendelea, mmoja wa madiwani walioko ndnai ya kikao amesma moto ni mkali sana la lazima juma Raibu ataachia ngani na hilo ni suala la muda tu kama ilivyotokea kwa Job Ndugai aliyekuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Wacha mvua inyeshe tuone panapovuja
 
Dah!
Hii ni hatari, CCM baada ya kuachiwa shamba la bibi kisiasa wanaupigia debe ushoga kwa nguvu zote.
Yaani miaka 60 baada ya uhuru, CCM imeamua kuwapelekea ushoga wachaga pale Moshi.

Haya sasa Meya wa Moshi mjini kupitia CCM anaunga mkono ushoga kwa 100%.
Kumekuchaa!
... kuna thread ilianzishwa humu 2 days ago kuhusu ushoga kutamalaki Moshi; I can now connect the dots! Unapata support ya nguvu toka chama chakavu.
 
Mstahiki Meya wa Mji wa Moshi Juma Rahibu amekumbana na kashfa kubwa ya kushiriki kikao cha Mashoga. Katika hali ya kushangaza na kustahajabisha.

Mstahiki Meya wa Moshi alihudhuria kikao hicho cha Mashoga na kutoa nasaha. Wadau wa siasa wamejikuta wakibabaika na kushangazwa huku watani wao wakuu wa siasa wakiwabeza kwa kuwaambia siku hizi wamebedili msimamo kimya kimya kwa kuunga mkono ushoga.

Ngongo kwasasa Rau madukani.
 
Huyu nae mnampa sifa za kijinga!...kila siku kuaandikwa andikwa tu utadhani basi ni mtendaji!...hamna kitu ni Mr Misifa ya kijinga tu!
 
Back
Top Bottom