Meremeta Report: Released to the Public (Revised & Free!)

sasa Mkuu turudi kwenye mada, kama unaona Mzee Mjj alivyobainisha kuwa kuna sababu nyingi zinatajwa kuhusiana na Meremeta kutegemeana na nani ameitoa wapi na katika mazingira gani. Mimi Nadhani This day Pia sasa ni wakati wa kuweka pamoja hizi sababu na kutoka na Hitimisho wasomaji wao tujue Meremeta ilikuwa ya nani kwa ajili ya nini?

Uko sahihi kabisa, si Thisday pekee, bali magazeti na wanasiasa wengine wa Tanzania pamoja na wanaharakati ili tufike mahali wahalifu wa sasa na wa zamani wawe wanaogopa kuiba si hali ya sasa ambako mwizi anaitwa MJANJA
 
Hili la Meremeta litafikia mwisho wake tu.. lakini kama mkondo wa maji ni lazima uongozwe vizuri shambani vinginevyo unaweza kugharikisha na kuharibu mazao.
 
Duuu! kweli sasa hivi mambo yanakwenda behind the curtain, na kama tusipokuwa makini hata humu JF tutapigwa kizungumkuti maana naona hata namba ya members sasa hivi inaongezeka kwa kasi sana hasa baada ya kutoka ripoti ya Meremeta
 
Hili la Meremeta litafikia mwisho wake tu.. lakini kama mkondo wa maji ni lazima uongozwe vizuri shambani vinginevyo unaweza kugharikisha na kuharibu mazao.

MJJ kufikia hatima na wahusika kuchukuliwa hatua kunatakiwa kuwe na concerned. Sasa Hivi jamii ya watanzania imekereka, lakini naloliona linakuwa gumu kwetu ni hatua ipi na nani aongoze mapambano? Tungeweza kama walioko kwenye serikali yetu wako safi, lakini kama ulivyobainisha kwenye "Kikwete sio safi; Yes I said" kwa mazingira ya sasa serikali haiwezi kutusaidia.

Tusimamie wapi kuwabana? hili ndio swali langu, Tuiinmgie mitaani naogopa kutatokea mapanga, watanzania tunajua kudai haki kwa amani kweli? watu waliochoshwa ukiwaambia njoo tufanye mkutano au maandamano ya amani watachukua mawe tu, hawataweza kuvumilia.
 
Duuu! kweli sasa hivi mambo yanakwenda behind the curtain, na kama tusipokuwa makini hata humu JF tutapigwa kizungumkuti maana naona hata namba ya members sasa hivi inaongezeka kwa kasi sana hasa baada ya kutoka ripoti ya Meremeta

Waache waje tuu watakoma wenyewe hapa hatuangalii watu tunachambua mada kwa uhakika na kujenga hoja kwa kutumia vielelezo hatumwogopi mtu hapa.

La muhimu ni kuwa wakiwa humu ndani watajifunza mengi ambayo yatakuwa faida kwao na kwa jamii yote ya Tanzania kwa ujumla.
 
Pia sehemu nzuri ambayo ilikuwa ya kuweka hizi hoja kati ni mahakama, Je mahakama yetu ipo huru kweli? na DPP ndio wa kutusaidia kuendesha mshitaka na PCCB & UWT ndio hao wa kuongoza upelelezi sasa mimi nachanganyikiwa, jamani nipeni moyo tufanye nini haya mambo yafike mwisho na haki na sheria zichukue mkondo wake?
 
Unaendesha mashtaka dhidi ya nani, wakati umeshaambiwa mwacheni mzee wetu APUMZIKE.
 
Wanatupatia Nyonyo halafu tunaanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe...

Nyonyo ni tamu ndugu yangu. We hujaona kasheshe ya kumwachisha mtoto kunyonya na endapo ameachwa hadi kufikia miaka 2; umria ambao anaanza kuita.. Mama nipe nyonyo!! Ukimleta mdogo wake wakati huo hakikisha visu viko mbali. It's the same game!
 
Lakini RAIA MWEMA wao si walishasema kuwa wameipata JF ama?

Sasa hawa THIS DAY waomeona ubaya gani kusema kama source yao ni JF?

Hapa tunapa wider picture kuwa inawezekana wahariri wenyewe inawezekana walipokuwa chuo kikuu walikuwa wana palagarize course works zao na haya ndio matokeo yake wakiwa kazini wanaumbuka

GT

Raiamwema ndio walikuwa newsbreaker. JF walitoa barua hii raiamwema na sio vinginevyo. Original chanzo cha habari hii ni Raiamwema.
 
Kuna watu wamezoea kudanganya na kujitutumua kila kona eti ni watu wa usalama. Sasa zile document zao zimezagaa mitaani wanaanza story, marta ni uandishi mara ni uongo eeh tumechoka. Kweli hatujui kusoma alama za nyakati.Times change.
 
Nadhani ni vema watu wakaanza kuchangia humu baada ya kuisoma ripoti nzima ya Mwanakijiji kuhusu Meremeta badala ya kukurupuka.
 
Tunashukuru sana kwa hii ripoti japokuwa wengine tuko kwenye mazingira hatarishi lakini hayawezi kutukatisha tamaa kujiunga pamoja katika kulipigania taifa letu. Mwenyezi Mungu akubariki na kukulinda
 
Back
Top Bottom