Meremeta 00:00:00. EXTRA

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji iwapo taarifa zimefahamika kwa nini watu tununue hizo taarifa na tusipewe bure?

Je Watanzania wasioweza kuchangia hizo dola 30 lakini wanataka kufahamu huo uozo wa meremeta wafanyeje? ilhali kuna watanzania wanaufahamu huo uozo lakini wanauza hata taarifa?.

Mimi ninapinga kwa nguvu zote, hatua hii ya mwanakijiji kuuza hizi taarifa muhimu, taarifa za kuwakomboa watanzania lakini zinageuzwa kuwa za kuuzwa instead.

Kwa jinsi hizi taarifa zilivyo muhimu, thamani yake ni kubwa sana kiasi kwamba hizi dola 30 zitakwamisha lengo la kumkomboa Mtanzania aliye masikini ajabu (dola 30 kwake ni mshahara wa mwezi).

sana sana kinachofanyika kwa hizi dola 30 ni kutugawa Watanzania katika kundi la walionacho na wasionacho linapokuja suala muhimu la kukomboana sisi kwa sisi, kwa sababu hakuna ushahidi kwamba mwenye hizo dola 30 ndo mwenye brain muscle, au patriotism kubwa, au uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli katika ile nchi kuliko mlalahoi, mshinda njaa, ambaye hana kitu lakini anaumia kweli kweli kutokana na madudu haya yaliyomo kwenye MereMeta.

Mwanakijiji fikiria mara mbili kabla hujatuuzia hizi taarifa.

Mkuu mimi naamini kwanza hata gharama aliyoitoa kama kweli wewe ni mzalendo ni ndogo sana kumbuka amepata taarifa ameziweka kwenye kitabu/kijarida vyote hivyo vinagharama zake sasa kuchangia gharama hizi kwa manufaa ya taifa wewe unaona siyo sahihi.MKJJ amejitoa mhanga kwa ajili ya nchi yetu hilo pekee lilitakiwa tumpongeze.
 
hii inaitwa hekima.
 
....Mods kutokana na uzito wa habari hii naelekea kufikiri kikosi cha 'usalama' humu jamvini wamo Alert kwa lolote litakalotokea,kwa kipindi cha siku2hizi tutatembelewa sana humu ndani!!
**Ni mawazo binafsi tu!
 
you have no idea mambo yaliyotokea siku hizi chache..mengine yanachekesha na kuudhi kwa wakati mmoja.
 
Buuu...haya wajameni this is all what I have....:(
 
Attachments

  • Meremeta.jpg
    Meremeta.jpg
    55.1 KB · Views: 109
Mkuu mwanakijiji, Mungu wa rehema akulinde na kukubariki kwa kazi nzuri unayolifanyia taifa letu, nasema asante sana.
 
Mkuu mwanakijiji, Mungu wa rehema akulinde na kukubariki kwa kazi nzuri unayolifanyia taifa letu, nasema asante sana.

Amen, awasute sute maadui zako, awaangamize kwa motona upepo wa kisuli suli, awagharikishe kama farao na jeshi lake walivogharikishwa kwenye bahari ya shamu!
 
nyinyi mnataka kuwatibua mafisadi sasa!

Na watibuke tu ndo tuwajue..kabla kiboko hajachokozwa unaweza kudhani ni gogo liko kwenye maji ,, lakini tibua kidogo ndo utajua kama ni kiboko au gogo.

FYI, juzi niliangalia tena documentary ya mapanki, ili kuwa na background nzuri ya hii kitu....nakuhakikishia safari hii nimeielewa zaidi kuliko mwanzoni!
 
Napenda watu wanaopenda kuwiden their horizon.. sasa ukiipata ripoti yenyewe... utashika mikono yako kichwani huku ukijiondokea zako; na kama mfalme aliyenyang'anywa taji lake utatembea kichwa chini huku upanga wako unauburuta!
 
Wanaotaka hiyo kopi waifanyie kazi wathibitishe kuwa nia yao ni njema kwa kukupatia kwanza yao waliyoandaa ili mbadilishane. Ili uone kwanza kama inamuelekeo?? Kama hawajafanya kitu mpaka leo meaning hata draft basi ina maana hawaihitaji hiyo kopi.
 
Babu yangu mwanakijiji, uchanguzi unakaribia, je hauoni ni haki ya kila mtanzania kujua nini serikari iliyokuwepo zaidi ya miaka 30 imekilea? watu tuchangie kwa kujitolea kwa kazi yako nzuri uliyoifanya ila wape haki kila mtanzania kujua nini kinaendelea. Maana kila mmoja wetu tunauwezo wa kubadilisha kainchi ketu cha Tanzania, iwe kwa njia ya kuchagua raisi na chama tawala au kujitoa muhanga wa ajili ya maendeleo ya kila mtu na watu masikini.

Naelewa unaitaji kurecover cost ila pia watanzania wangapi hasa wapiga kura wenye uwezo wa kubadirisha raisi wa nje wanaweza kuafford?
 
nadhani sasa imefika t-1, au nyie bado mko jumatatu? "Houston...were a clear for launch." Engine zina moto tayari, launchpad imeshajiweka pembeni...twasubi: 00:00:00
 
Hili swala siyo dogo, ni kubwa, ni aibu kwa mafisadi na kwetu sote. Sasa hivi najisikia aibu sana ninapokutana na wakongo mitaani. Nitabakia mwenye kushangaa kama hakuna hatua zitakazo chukuliwa. Hivi bunge linamalizika lini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom