Mengi yazidi kuibuka kuhusu Nyalandu

Mengi yazidi kuibuka kuhusu Nyalandu

Sasa hivi mnaye kwenu
Unahangaikahangaika sana. Na wakati hata wewe ulikuwa na misimamo ya tofauti dhidi ya mafisadi wa ccm...Sasa sijui ni yaleyale ya ukabila na ukanda ama ni kitu gani? Nakukumbuka sana humu before, lakini umepiga uturn ya kufa mtu. Sasa umepofuka kabisa! Umebaki kwenye ushabiki tu wala sioni pointi yoyote unapochangia nowdays!
 
Katika hatua nyingine, mambo mapya yameibuka kuhusu kampuni ya Kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo majangili walidungua helikopta yake mwezi uliopita na kusababisha kifo cha rubani raia wa Uingereza, Roger Gower.
FCF inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) Ltd na Wengert Windrose Safaris.

Wakati helikopta hiyo ikidunguliwa kwa kile kinachoelezwa kwamba ilikuwa kwenye doria dhidi ya majangili, kumbukumbu zilizopo Wizara ya Maliasili na Utalii zinaonesha kuwa kampuni ya Mwiba Holdings Ltd ni miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa na nyara za Serikali.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.

Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge. Helikopta iliyodunguliwa na majangili ndiyo aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge

Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.
Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.

Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.
Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).

Pamoja na kutoa Leseni ya Rais, Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.
FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama (Makao Ranch).

Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makoa kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama.
Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.

Source:Jamhuri

Uongo mtupu nyarandu kawa Waziri 2014 mpaka 2015, Waziri waligawa vitalu ni kagasheki na maige. Tathimini ya vitalu ilikamilika 2012 ikifanywa na tawiri.
 
Business as usual! Tukio la 2011 linakuja kutolewa hadharani 2017 baada ya mtu kumwaga manyanga! Inamana asingejitoa chamani hizi kashifa zisingefichuliwa. Poor my country
 
Yaan hii nchi bwana mtu akienda upinzani ndio utasikia mambo elfu 10 mabaya ameyatenda! Lakn akiwa ccm aa yeye msafi 100%
 
Swali moja tu
Mtoa mada unataka kusema kuna kulindana ndani systm kama sio hii hoja ilikuwa wapi siku zote?
Najaribu kuwaza kwa maandishi!!!
Kwani hii hoja unajua ni ya lini
 
Kuna ndugu waliwahi kusema huyu jamaa hafai ila alivohama chama wataanza kusema anafaa na makosa aliyofanya ni kwasababu alikuwa anaagizwa kutoka juu au kwa vimemo hahahahaha hii Tanzania yetu raha sana.
Ni bora upige kura kwa kusikiliza hoja za mtu bila kujali chama ila ukijali zaidi chama hicho chama kuna siku kitafanya mambo ambayo utashindwa kujitetea hata mbele ya chama kingine unachokiona hakifai.
 
WanaJF,

Heri ya Mwaka mpya.

Manyerere Jackton na Balile pamoja na timu nzima ya jamhuri mnafanya kazi yenu vizuri.Hii ndio inaitwa investigative journalism(Uandishi wa Kiuchunguzi) sio wale wambea wengine wanajiitawaandishi wa habari za kiuchunguzi

BTW: Sasa inabidi Nyalandu atoke hadharani aeleze ukweli.Serikali nayo ichukue hatua za kisheria baada ya uchunguzi

Hivi kweli mtu anaweza kuwa waziri wa jamhuri ya muungano na kufanya mambo yasiyo ya kizaelendo tena ambayo ni ya kuhujumu uchumi na pia kuhatarisha usalama wa taifa kiasi hiki bila Idara ya usalama kujua na kuchukua hatua muafaka?
Toka huko mafichoni uje uokoe nyumbu jangili papa kavamia mbuga ya ufipa nyumbu wote wamechachawa
 
WanaJF,

Heri ya Mwaka mpya.

Manyerere Jackton na Balile pamoja na timu nzima ya jamhuri mnafanya kazi yenu vizuri.Hii ndio inaitwa investigative journalism(Uandishi wa Kiuchunguzi) sio wale wambea wengine wanajiitawaandishi wa habari za kiuchunguzi

BTW: Sasa inabidi Nyalandu atoke hadharani aeleze ukweli.Serikali nayo ichukue hatua za kisheria baada ya uchunguzi

Hivi kweli mtu anaweza kuwa waziri wa jamhuri ya muungano na kufanya mambo yasiyo ya kizaelendo tena ambayo ni ya kuhujumu uchumi na pia kuhatarisha usalama wa taifa kiasi hiki bila Idara ya usalama kujua na kuchukua hatua muafaka?
Dah!
Please come back!
 
Jamuhuri limekuwa gazeti la habari za kiuchunguzi hongera sana balile na manyerere najua katika waandishi wanaoipigania Tanzania mpya mnaongoza
JERRY MURO NAYE NI INVESTIGATIVE JOURNALIST MZURI TU SHIDA NJAA
 
Unahangaikahangaika sana. Na wakati hata wewe ulikuwa na misimamo ya tofauti dhidi ya mafisadi wa ccm...Sasa sijui ni yaleyale ya ukabila na ukanda ama ni kitu gani? Nakukumbuka sana humu before, lakini umepiga uturn ya kufa mtu. Sasa umepofuka kabisa! Umebaki kwenye ushabiki tu wala sioni pointi yoyote unapochangia nowdays!
Endeleen kumpangusa nyalandu
 
Business as usual! Tukio la 2011 linakuja kutolewa hadharani 2017 baada ya mtu kumwaga manyanga! Inamana asingejitoa chamani hizi kashifa zisingefichuliwa. Poor my country
We kweli nyumbu.. Soma tarehe ya huu uzi ndio urudi tena
 
Back
Top Bottom