Mengi yazidi kuibuka kuhusu Nyalandu

Mengi yazidi kuibuka kuhusu Nyalandu

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,587
Reaction score
28,749
Katika hatua nyingine, mambo mapya yameibuka kuhusu kampuni ya Kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo majangili walidungua helikopta yake mwezi uliopita na kusababisha kifo cha rubani raia wa Uingereza, Roger Gower.
FCF inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) Ltd na Wengert Windrose Safaris.

Wakati helikopta hiyo ikidunguliwa kwa kile kinachoelezwa kwamba ilikuwa kwenye doria dhidi ya majangili, kumbukumbu zilizopo Wizara ya Maliasili na Utalii zinaonesha kuwa kampuni ya Mwiba Holdings Ltd ni miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa na nyara za Serikali.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.

Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge. Helikopta iliyodunguliwa na majangili ndiyo aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge

Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.
Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.

Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.
Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).

Pamoja na kutoa Leseni ya Rais, Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.
FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama (Makao Ranch).

Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makoa kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama.
Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.

Source:Jamhuri
 
Kama ni kweli kwa hii serikali ya magu huyu naye hatopona mwendo ni mdogo mdogo tutaona mengi kipindi hiki tusubiri wanakwenda kuisoma namba mapema sana
 
Yaani hii nchi sijui ilisha kuwa kichaka gani. Hata shamba la bibi nalo lina mmiliki wake. Kila mtu alikuwa anakwapua to tbe maximum kwa nafasi yake. Sioni shaka na taarifa hii kwa sababu Mh. Nyarandu amekuwa akiishi na kwenda US kwa muda mrefu. This guy should be charged with connection to murder that poor British pilot. Sioni tofauti yake na akina Escobar katika uharamia wao na madawa ya kulevya. It's a shame.
 
Kugusa huyo mmiliki ni timing, ni mmoja wapo wa wafadhili wa serikali ya state, through chama cha D!
Waziri nae ameishi sana state! Tunajua organization nyingi zinavyotengeneza operatives wake direct na indirect kufanikisha deal zao.(mfano EHM's) na nyingine za kijasusi kibiashara lakini nyuma ya kivuli cha usalama!

Jipu hilo likitumbuliwa vibaya, usaha ukiruka unaweza kumtia mtu upofu!
 
Nyalandu aliwahi kuwa hata anasafiri na hao wazungu kwenye kampen zake za urais. Lakini haishangazi ndo ilikuwa style ya awam hiyo manake kama hata unakumbuka hata wachina nao walikuwepo kwenye kampen za CCM. Anyway, sijui mwisho nini lakini bado hali ni mbaya sana bado na sii ajabu hata JPM akamaliza awam ya 5 bila kugusa nusu ya majipu kama haya na mengine ukizingatia kuwa JK kila siku anabisha hodi ikulu sijui alisahau nn mle.
 
WanaJF,

Heri ya Mwaka mpya.

Manyerere Jackton na Balile pamoja na timu nzima ya jamhuri mnafanya kazi yenu vizuri.Hii ndio inaitwa investigative journalism(Uandishi wa Kiuchunguzi) sio wale wambea wengine wanajiitawaandishi wa habari za kiuchunguzi

BTW: Sasa inabidi Nyalandu atoke hadharani aeleze ukweli.Serikali nayo ichukue hatua za kisheria baada ya uchunguzi

Hivi kweli mtu anaweza kuwa waziri wa jamhuri ya muungano na kufanya mambo yasiyo ya kizaelendo tena ambayo ni ya kuhujumu uchumi na pia kuhatarisha usalama wa taifa kiasi hiki bila Idara ya usalama kujua na kuchukua hatua muafaka?
 
Back
Top Bottom