Mengi yazidi kuibuka kuhusu Nyalandu

Mengi yazidi kuibuka kuhusu Nyalandu

Katika hatua nyingine, mambo mapya yameibuka kuhusu kampuni ya Kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo majangili walidungua helikopta yake mwezi uliopita na kusababisha kifo cha rubani raia wa Uingereza, Roger Gower.
FCF inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) Ltd na Wengert Windrose Safaris.

Wakati helikopta hiyo ikidunguliwa kwa kile kinachoelezwa kwamba ilikuwa kwenye doria dhidi ya majangili, kumbukumbu zilizopo Wizara ya Maliasili na Utalii zinaonesha kuwa kampuni ya Mwiba Holdings Ltd ni miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa na nyara za Serikali.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.

Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge. Helikopta iliyodunguliwa na majangili ndiyo aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge

Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.
Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.

Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.
Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).

Pamoja na kutoa Leseni ya Rais, Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.
FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama (Makao Ranch).

Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makoa kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama.
Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.

Source:Jamhuri
am sure gazeti la jamhuri huwa lina siri nzito sana kuhusu ujangili...
kuna habari moja walitoaga connection nzima ya ujangili jinsi inavyoratibiwa na nyarandu...
ila serikali chini ya jk ikawa kimya.......ila walitoa had hotel wanazokusanyia had yanavyouzwa
serikali ikae na jenerali ulimwengu wapate feedback vizuri bila hivyo drama ya wizi itaendelea
 
Kugusa huyo mmiliki ni timing, ni mmoja wapo wa wafadhili wa serikali ya state, through chama cha D!
Waziri nae ameishi sana state! Tunajua organization nyingi zinavyotengeneza operatives wake direct na indirect kufanikisha deal zao.(mfano EHM's) na nyingine za kijasusi kibiashara lakini nyuma ya kivuli cha usalama!

Jipu hilo likitumbuliwa vibaya, usaha ukiruka unaweza kumtia mtu upofu!
mkuu kwahiyo huyo jamaa wa FCF ni mfadhili wa democratic????????
daahh nchi yao inafadhiliwa kwa rasilimali zetu............
alafu baadae wanakuja tena kwetu na kutufadhili kwa njia nyingine kumbe ni fedha zetu......
dahh hii iangaliwe vizuri hii
 
hawa jama wanasema wapo kutusaidia kulinda wanyama wetu safely......it means sis tumeshindwa kulinda alaf tunawalipa high amount ya kulinda wanyama wetu...wakat wao ndo majangali........
GO HII LINK....
Home

FCF proactively assists the Tanzanian Wildlife Division/protection by providing anti-poaching teams that consist of highly motivated and professionally trained rangers
hapo kwenye red...
tz hamna wataalamu na watu morali kulinda wanyama wetu....ngoja wathungu waje wenye morali na huruma na rasilimali na wanyama wetu walinde.....................
 
Nyalandu aliwahi kuwa hata anasafiri na hao wazungu kwenye kampen zake za urais. Lakini haishangazi ndo ilikuwa style ya awam hiyo manake kama hata unakumbuka hata wachina nao walikuwepo kwenye kampen za CCM. Anyway, sijui mwisho nini lakini bado hali ni mbaya sana bado na sii ajabu hata JPM akamaliza awam ya 5 bila kugusa nusu ya majipu kama haya na mengine ukizingatia kuwa JK kila siku anabisha hodi ikulu sijui alisahau nn mle.
na jana beni mkapa kaenda ikulu..............tareh 25/2
 
WanaJF,

Heri ya Mwaka mpya.

Manyerere Jackton na Balile pamoja na timu nzima ya jamhuri mnafanya kazi yenu vizuri.Hii ndio inaitwa investigative journalism(Uandishi wa Kiuchunguzi) sio wale wambea wengine wanajiitawaandishi wa habari za kiuchunguzi

BTW: Sasa inabidi Nyalandu atoke hadharani aeleze ukweli.Serikali nayo ichukue hatua za kisheria baada ya uchunguzi

Hivi kweli mtu anaweza kuwa waziri wa jamhuri ya muungano na kufanya mambo yasiyo ya kizaelendo tena ambayo ni ya kuhujumu uchumi na pia kuhatarisha usalama wa taifa kiasi hiki bila Idara ya usalama kujua na kuchukua hatua muafaka?
usalama??????
sitaki kuongea kitu mkuu...nsije nkawa naimiss JF...
ila vyombo vya dola minaona havina nguvu kwa viongoz serikalini polis.....
tutasakwa mi nawewe besigye na akina mbowe+lissu sio akina nyarandu..........mfano besigye uganda
 
Kuna uzi humu alidai wamarekani wanataka niwe rais wa tanzania
ndo tujue wamarekani hawanaga urafiki na mwafrika zaid ya kutaka kunyonya2 rasilimali.....
waza hivi....angepita urais ingekuaje?????????????
 
Huo ndo ukweli na ndipo tutamwelewa. zaidi ya jipu hilo tunahitaji arejee majipu ya ESCROW na saga la Zenji!
MSITEGEMEE HAYA MAJIPU KUGUSWA...
hivi simnajua escrow muhongo yumo..leo ni wazr wa nishati na madini..sector nyeti kabisa nchini..sasa atashikiwa vipi na sakata la escrow....
zanzbar rais kasema hatoingilia kati ila fujo zikitokea atapeleka jeshi........
so hayo mambo sahau mkuuu...
 
Tena Rais wa UKWATA Taifa! Binafsi nilitegemea angekuja kuwa askofu kwa unyenyekevu ule aliokuwa nao. Kumbe ilikuwa gia ya kuruka Marekani. State ikamloga mazima. Aliporudi akawa anakimbizana na totoz na ufisadi.
kumbe nyarandu aliokoka?????
hizi fedha hizi........
 
Jamuhuri limekuwa gazeti la habari za kiuchunguzi hongera sana balile na manyerere najua katika waandishi wanaoipigania Tanzania mpya mnaongoza
mkuu somtimes habari zao ni kupongeza CCM hawa jamhuri lkn huwa nashindwa kuwaelewa...
huwa nahs walipata % flani ili kusfia serikali..........
 
Hivi Na Wale WALIOHUSIKA Na KUSAFIRISHA Wanyama Walio Hai Kwenda Ughaibuni, Wameshakamatwa Tayari!!! MAANA Twiga Wetu Kukamatwa Mbugani, Kupelekwa Airport Na Kupandishwa Ndege Na Kusafirishwa Kwenda Ughaibuni!!! KAMA Bado, TUNAHITAJI Wakamatwe, Wahojiwe, Washitakiwe, Wafungwe Na Wafilisiwe MALI ZAO Zoote!!!! NDIO Majipu Tunayoyahitaji Yatumbuliwe Haraka Saanaa!!!
hapo utagusa wengi vasco,nyarandu,kinana nk...
ndomana jpm yupo kimya.........hapawez apo si saiz yake,,...yeye anatumbua saiz yake2
,makubwa kumshinda anayaacha.........
 
Kweli kwa upuuzi uliokuwa ukifanywa na maswahiba wa Kikwete hii nchi almanusura ingetoweka. Ila Mungu ni mkubwa, kamleta Magufuli kwa wakati muafaka. Rai yangu kwa watanzania, tuzidi kumwombea rais wetu na kumuunga mkono ili hawa waliotufikisha hapa walipe dearly for the shit they cost our country. God bless Magufuli, God bless Tanzania
 
hii kali sana, nyalandu inabidi ajibu shutma
 
Nyalandu aliwahi kuwa hata anasafiri na hao wazungu kwenye kampen zake za urais. Lakini haishangazi ndo ilikuwa style ya awam hiyo manake kama hata unakumbuka hata wachina nao walikuwepo kwenye kampen za CCM. Anyway, sijui mwisho nini lakini bado hali ni mbaya sana bado na sii ajabu hata JPM akamaliza awam ya 5 bila kugusa nusu ya majipu kama haya na mengine ukizingatia kuwa JK kila siku anabisha hodi ikulu sijui alisahau nn mle.
ha ha ha LOL labda kuna kitu kasahau huwezi jua.....na JPM kesha kikalia ndio hapo sasa
 
Nyalandu hajawahi kuwa mzalendo, nilishangaa sana kutaka kuwania urais.
Elewa tu kitu kimoja mkuu, kwamba kuna kuwa mzalendo kwa macho ya kiTanzania na kwa macho ya wawekezaji wa nje.
 
Back
Top Bottom