Allien
JF-Expert Member
- Jul 6, 2008
- 5,546
- 1,861
sorry to burst your bubble.. suala hili limefikia tamati ya kiutuzima. Nadhani na sisi tuliache liishie hivyo hivyo na turudi kwenye Kagoda yetu, EpA, Meremeta na wenzake. Kama wangekuwa na la kufanya wangefanya na habari toka ndani sana, kijana wetu alikosea tu kidogo na ninaamini atakuwa amejifunza.
Kiongozi Mwamakijiji,
With due respect napenda nitofautiane na wewe kwa hili. Kwa Watanzania haijalishi kama hili suala wamefikia tamati kiutu uzima au la. Hili swali kwa sasa ni public issue. Mengi alianza in public na Waziri kijana akalisemea in public. Watanzania wanayo haki ya kujua majibu ya maswali yote.
Na kama humu JF unadhani kama eti kwa sasa tuliache na kurudi on other issues, I am afraid tutakua tunaingia katika ufisadi upya. Ni lazima tupressurize ili kupata facts zote kama:
Ni nani aliyemtishia Mengi kifo na ikiwezekana afikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
Ni waziri yupi kijana aliyetaka kumujumu Mengi? Tunapenda kuona pia sheria inachukua mkondo wake.
Na baada ya hayo serikali itoe maelezo ya kuridhisha kwa Wananchi kama vikao hivyo kweli vilikuwapo vinginevyo ijisafishe kabisa kwa kuchukua hatua kwa wote waliuohusika na njama hizi. Ikigundulika ni kweli, Wanaharakati wachukue hatua kulipigia kelele hili na kama kuna namna sheria pia ichukue mkondo wake.
Mwishoni, naomba wewe Mwanakijiji, utoe makala katika CHECHE, Watanzania wapate kujua based on information na facts zilozopatikana mpaka sasa. Usipofanya hivyo, nitakuwa na maswali Mengi sana ya kujiuliza juu yako.
Mwanakijiji, hizi ni zama mpya na mambo ya kishikaji hayapo tena. Mwizi aitwe mwizi, Mhujumu aitwe mhujumu, nk na kwa wote hao sheria zichukue mkondo wake.
Usitukatishe tamaa, wengi tumekuwa tukikuona kama mmoja wa viongozi wetu hapa JF. Au wameanza kukununua?
Nimesema tulitoa kiingilio kwenye Movie Hii, Trailler imekwisha tunasubiri Movie. Kama Movie hakuna, turudishiwe pesa na turudi home tuwaaambie Wadau ni nani waliochemsha na kwa vipi.