Kandambilimbili
R I P
- Nov 11, 2008
- 782
- 42
Hapa sielewi, kwani Masha alisema atamchukulia hatua ndani ya siku saba au Mangi atoe ushahidi baada ya siku saba? inawezekana anajipanga who knows?Ndugu wanaJF,
Tumesikia mambo mengi kutokana na na saga la Masha VS Mengi. Bila kujali tuhuma Mengi alizoziweka juu ya waziri kijana ambaye hakutajwa jina na Mengi.
Masha kama waziri mwenye dhamana ya usalama wa raia na mali zao, aliahidi kuchukua hatua dhidi ya yule ambaye anataka kumdhuru raia Mengi na mali zake, hivyo kutaka kupata vidhibitisho kutoka kwa mengi. Ili kutimiza azma hiyo Masha alimuomba/mlazimisha Mengi kuwakilisha vielelezo vya ushahidi kwenye ofisi yake, na kama akishindwa vile vile Mengi angechukuliwa hatua kwa kuipaka serikali na vyombo vyake matope ama kafanya uchochezi.
Siku saba zilishakwisha, Mengi hakupeleka vielelezo kama alivyotakiwa, Masha kama waziri na ofisi yake kwa ujumla imekaa kimya bila kusema chochote baada ya siku saba kuisha.
Hivyo Sababu za masha kujiuzulu ni hizi hapa:
Masha ameshindwa kutimiza wajibu wake kama waziri kulinda raia na mali zao, ameshindwa ahadi yake aliyoitoa siku 12 tu zilizopita. Hivyo Masha ni Muongo amaudanganya UMMA.
Inawezekana kabisa 99% ni kweli Masha alihusika kwenye huo mpango wa kutaka kumfilisi Mengi hivyo kauogopa kutimiza yale mamlaka yaliyo chini yake kwa hofu ya kumtokea puani(kumbuka Balali alifanya press akasema yeye ni safi, Mgonja nae hivyo hivyo, Mramba ndio usiseme na wote walitishia kwenda mahakani leo wao ndio wako huko) Kwa mifano hiyo inatosha kusema Masha anahusika kwenye hiyo plan.
Masha angekuwa muungwana, alipoona hiyo ahadi yake haitekelezeki alipaswa kurudi kwenye press na kuomba msamaha kwa kauli yake aliyeitoa na kusema alikuwa mislead hivyo either anaifuta kauli yake ama atuambie wamefikiria kuchukua hatua ingine (maelewano nje ya vyombo vya dola), na kama ni hivyo kwani Mengi anaugomvi gani na Masha kama Masha hausiki kwenye hiyo tuhumaaa???? Leo ni siku ya 5 Kimya chake ni dharau kubwa kwa wananchi wa Tanzania, Hivyo hafai kuongoza umma wa watanzania
Mwisho nitoe wito kwa viongozi wengine kutojiona wao ni miungu kuwa hawakosei, sisi kama binadamu tunakosea na tunapokosea kiungwana tunaomba msamaha, tuache dharau na kujikweza kama Masha.
Masha Tukosa imani na wewe, Maalbino wanauwawa uko kimya kutatua tatizo,
Vikongwe wanauwawa uko kimya, tangu uingie kwenye hiyo wizara ujambazi umeongezeka, Usalama wa raia na hata wa rais umekuwa mashakani (kumbuka yaliyotokea Mbeya), n.k Hufai jiuzulu, Masha jiuzulu
JF pazuri bwana a lot of PERCEPTION and BLA BLA