Jambo moja nina uhakika kuhusu Membe na Urais.
Awali ya yote, wa kwanza kabisa kuzungumzia suala la Member na Urais ni gazeti Rai miaka kadhaa iliyopita pale alipomuumbua Hassy Kitine. Wakati huo Membe alikuwa ni Mbunge tu...enzi za Mkapa. Likewise, wengi wakati huo walikuwa hawamfahamu Membe.
Baada ya Kombora la Membe ambalo lilimwondoa Kitine kwenye nafasi ya Uwaziri, Rai ikafanya mahojiano na Membe na moja ya maswali ambayo ilimuuliza ni kama ana mpango wa kugombea Urais 2005. Membe akasema wazi kwamba hana mpango huo.
Baada ya kuingia JK, Membe alianza unaibu Waziri (if am not mistaken, mambo ya ndani au nishati). Later akateuliwa Waziri Mambo ya Nje! Kama ilivyo mazoea yetu, tunazani kila anayekuwa Mambo ya Nje, ni move towards Urais...hili lilitokana na Mkapa na JK kuwa Mambo ya Nje b4! Hapa sasa, ndipo Wabongo tukaendelea kuitilia nia suala la Membe na Urais. nakumbuka hata yeye mwenyewe aliwahi kujibu kwamba, hadi yeye, kuna Mawaziri 13 ambao walipitia nafasi hiyo, na only 2 ndio wamepata kuwa marais.
So, kama kweli Membe ana nia na Urais, basi nia hiyo ilijengwa na vyombo vya habari pamoja na wananchi. Katika hali ya kawaida, ikiwa watu wanakuzungumzia zungumzia kuhusu post fulani, basi huenda nawe ukajikuta unajihisi labda unastahili kwa nafasi hiyo!! Na as far as nae ni Mtanzania basi anastahili nafasi hiyo....Wapiga kura ndio watakaomua kama anafaa au hafai.
Binafsi, sijaona move yoyote ya Membe kutaka Urais sana sana ninachokiona ni hofu ya wanaotaka urais pamoja na wapambe wao. Hawa watu inaonesha dhahiri kwamba wanamuhofia Membe...!!!