Membe kuwania urais 2015...

Membe kuwania urais 2015...

Baada ya Kambi Mbili zenye Nguvu ndani ya CCM kuangushwa Vibaya na CDM katika chaguzi za Ubunge huko Arumeru Mashariki ( Namzungumzia Lowasa) na Udiwani huko Kirumba na Kiwira ( Namzungumzia Sitta)

Je ni wakati Muafaka sasa kwa CCM kuanza kumuandaa Benard Membe Apeperushe bendera 2015? Wana CCM Mnasemaje?

Unaposema CCM imuandae Membe kwa ajili ya 2015,ina maana lowassa na sitta walikuwa wameandaliwa na Chama?
OTIS
 
Sijui kwa nini watu wanamuona Membe ni predential material? Foreign affairs imemshinda atawezaje nchi nzima? kwa mdimu?

Yaani mkuu tupo pamoja....
Huyu jamaa hamna kitu kabisa, ni aina ya akina JK tu
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Unaposema CCM imuandae Membe kwa ajili ya 2015,ina maana lowassa na sitta walikuwa wameandaliwa na Chama?
OTIS

Sitta na Lowasa wameshachuja hawans mvuto
 
Hii post yako itatusababishia BAN tafadhari ifute!
Join Date : 6th April 2012
Location : Mfereji maringo-Zanzibar
Posts : 186

Tume ya Katiba,
Wewe ni mgeni humu jukwaani. So far una siku kama 4 hivi lakini nimegundua you are Pro Magamba. Hii kazi unayofanya ilishawai kufanywa na wenzako. Wengi wao iliwashinda wakakata tamaa na hawaonekani kabisa jukwaani. Baadhi yao bado wanaendelea ingawa kwa kuchechemea kwa sababu hawana hoja. Nakushauri fanya kazi ya ushabiki wako kwa utaratibu. Ukikurupuka utapotea kama Mwita25 na Malaria Sugu. Hawa walikuwa na spidi kali zaidi yako.
 
Sijui kwa nini watu wanamuona Membe ni predential material? Foreign affairs imemshinda atawezaje nchi nzima? kwa mdimu?

Imemshindaje.
Kipi ameshindwa fanya kama sehemu ya majukumu yake.
OTIS
 
Ustaadhi B.Membe urais hauwezi, huoni hata mambo ya nje imemshinda mkulu ameamua kufanya kazi zake?
 
Imemshindaje.
Kipi ameshindwa fanya kama sehemu ya majukumu yake.
OTIS

Unaweza kuniambia status ya Tanzania kwenye ulingo wa kimataifa ukoje tangu huyu bwana ashike usukani? Unakumbuka 'lying low' ya Libya? Juzi walibya walikuwa wanakunywa juice magogoni, uso wake uliangalia upande gani? Na porojo zake kuwa kuna nchi za magharibi zinafadhili machafuko- aliishia kwa kuwekwa kitako.

Huko tuendako ni vizuri kuwa na waziri wa foreign affairs anayetaka kutumikia nchi zaidi kuliki kujijenga yeye kama rais mtarajiwa. Huyu bwana anatumia muda mwingi kujitangaza yeye kama yeye na sio nchi.
 
Ccm hawana wa kumusimamisha 2015, na ndo maana wanafikiria kumpandisha huyo mchovu, wamruhusu aje amsindikize Dk slaa kuelekea ikulu.
 
Membe peke yake anafaa kuwa Rais 2015. Tumuombee kwa mwenyezi Mungu.
:A S kiss:
 
Jamani hivi mpaka lini tutaendelea kujadili nani atagombea urais kupitia chama cha majambazi (ccm), 2015 hatutathubutu tena kuyapeleka majambazi mengine pale magogoni kwani imetosha kuibiwa tena, alafu hata huyu muimba tarabu wa bagamoyo mlimuweka pale magogoni kimakosa kabisa!
 
Benard Membe=Jakaya Kikwete, So shida zitaendelea kwa ari zaid, nguvu zaidi na kasi zaidi.
 
Jana ni shuhudia ukilaza wa Membe pale Taifa Stadium akiwa na Nape Nnauye katika Tamasha la Pasaka......ametamka four times anasema tumuombe R.I.P Vicent Kanumba badala ya Steven Kanumba. Sasa huyu ndo mtu anafaa?kama nchi ipo kwenye majonzi ya kumpoteza kijana wake na ambaye ametangaza taifa letu nchi za nje ambazo Membe ndo Waziri wa mambo ya nchi za nje na Kimataifa hajui hata jina. Je itakuwaje akipewa nchi si ndo hatajua kwa nini achaguliwe kuwa rais?
 
Join Date : 6th April 2012
Location : Mfereji maringo-Zanzibar
Posts : 186

Tume ya Katiba,
Wewe ni mgeni humu jukwaani. So far una siku kama 4 hivi lakini nimegundua you are Pro Magamba. Hii kazi unayofanya ilishawai kufanywa na wenzako. Wengi wao iliwashinda wakakata tamaa na hawaonekani kabisa jukwaani. Baadhi yao bado wanaendelea ingawa kwa kuchechemea kwa sababu hawana hoja. Nakushauri fanya kazi ya ushabiki wako kwa utaratibu. Ukikurupuka utapotea kama Mwita25 na Malaria Sugu. Hawa walikuwa na spidi kali zaidi yako.

Hongera kaka, umenisaidia sana, nilikuwa nafikiria sana namna ya kumuanza huyu mzenji...naona amevamia humu jukwaani kama vile ana miaka kadhaa.....
Amesahau, Haraka haraka haina baraka, na Simba mwenda pole ndio mla nyama....wao na Magamba yao na Uzanzibar wao wanaota kuja Kuitawala Tanganyika 2015....ngoja tuone, kama watu less than 1.5 milioni wanaweza kutushinda 44 ml. Halafu wanasahau kuwa joto linaongezeka, muda si mrefu Zenj itamezwa na maji...sijui watajivunia nini....? Pigeni tu kelele,na majigambo kuwa tume ya Katiba ni yenu....yananiboa kweli....subiri kuna siku yenu...
 
Ustaadhi B.Membe urais hauwezi, huoni hata mambo ya nje imemshinda mkulu ameamua kufanya kazi zake?
Hebu tufafanulie imemshinda kwa misingi ipi? kuwa analytical kwamba kulitakiwa kifanyike hiki, lakini hakikufanyika au hakikukamilika kwa wakati husika. Siyo kuropoka tu eti imemshinda. Elezea kwa mifano nini kimemshinda?
 
Jana ni shuhudia ukilaza wa Membe pale Taifa Stadium akiwa na Nape Nnauye katika Tamasha la Pasaka......ametamka four times anasema tumuombe R.I.P Vicent Kanumba badala ya Steven Kanumba. Sasa huyu ndo mtu anafaa?kama nchi ipo kwenye majonzi ya kumpoteza kijana wake na ambaye ametangaza taifa letu nchi za nje ambazo Membe ndo Waziri wa mambo ya nchi za nje na Kimataifa hajui hata jina. Je itakuwaje akipewa nchi si ndo hatajua kwa nini achaguliwe kuwa rais?
wewe ndiyo kilaza namba moja kabisaaa. Yaani wewe kigezo ndo umeona jina la mtu?? hebu tutoleeni utumbo humu. Huna akili kabisa wewe
 
Benard Membe=Jakaya Kikwete, So shida zitaendelea kwa ari zaid, nguvu zaidi na kasi zaidi.
Hebu elezea hiyo equality uliyoionesha hapo? wanafanana nini? sura au? kuwa great thinker wewe acha kuandika kizembezembe ebooo! mnaboa sana humu watoto wa mayai ninyi
 
Hivi kweli jamani, kama kusoma hatuwezi hata macho hayaoni? Niambieni, Huyo Membe wao kafanya nini katika nchi hii mpaka tumfikirie. tafadhari tujaribu kutazama kama hata kusoma hatuwezi!! Huyo ni kilaza mwingine tu.
 
Back
Top Bottom