Membe: Hatujapata taarifa kuhusu Israel!

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Serikali imesema haijapata taarifa za Waziri wa Ulinzi wa Israeli, Ehud Barak, kutoa matamshi kwamba Tanzania sio nchi muhimu kwake. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu kauli hiyo jana kwa njia ya simu, alisema kwamba hajapata taarifa kamili kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, alitaka apigiwe simu jana mchana, lakini alipopigiwa simu yake ya mkononi ili kueleza msimamo wa serikali, simu yake iliita bila kupokelewa. Kauli hiyo kwamba Tanzania si muhimu kwa Israeli ilitolewa na Waziri Barak alipofanya mahojiano na Radio Israel na kunukuliwa na vyombo vingine vya habari vya nchi hiyo wiki iliyopita. Waziri Barak alitaja nchi muhimu na zenye maslahi kwa Israel kuwa ni Ujerumani, Uingereza na Ufaransa na siyo baadhi ya nchi maskini, ikiwamo Tanzania.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa wa Chadema, John Mnyika, alisema kupitia kauli ya kiongozi huyo wa serikali ya Israel, inaiona Tanzania sio nchi muhimu. "Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa, Bernard Membe kuitaka serikali ya Israel kuomba radhi kufuatia kauli hiyo au kueleza wazi iwapo mazungumzo hayo ya Waziri Barak ni msimamo wa nchi hiyo kuhusu uhusiano wa kidiplomasia wa mataifa yetu," alisema Mnyika.

Chanzo: Nipashe

UPDATE

And the deputy minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Mr Mahadhi Juma Maalim, told The Citizen Tuesday that the government has taken the issue seriously and is holding consultations over recent derogatory remarks.

"We are holding meetings to see how we can respond to Mr Barak's comments. We will let you know when we are ready," he said during a telephone interview. Mr Barak has refused to apologise to Tanzania after branding the country as irrelevant as far as Israel's relations with other nations are concerned.

Source: http://thecitizen.co.tz/news/4-national-news/18379-israels-remarks-raise-concerns.html
 
Tusijali kuhusu Israel, wao ni kunguni wanajali kunyunya kwa rafiki yao yoyote; kitu kinachotakiwa ni tuendelee kuchimba GAS ya kutosha kuuza utaona wanaanza kuleta pua zao kwetu, sababu GAS ya EGYPT is done finito, SYRIA hawana GAS wana PETROLEUM na ina UCHAFU kweli inatakiwa isafishwe haswa nchi zinazoinunua ni za EUROPE only petroli safi sana ni ya LIBYA .

Labda ya kwetu itakuwa safi pia
 
unafikiri hajapata taarifa? aseme tu kuwa anaogopa kuwaudhi mabwana zake.

Hivi taarifa kamili huwa anazipata kwa nani? Lile suala la ushoga alipata taarifa kwa nani?
 
Hata mimi ningekua Israel nisingemtilia maanani Tanzania. Hana faida kwake binafsi atamfaidisha vipi mwingine?
Lizzy, hakuna mtu anawalazimisha waisrael kuwathamini Watanzania. What we need to see ni reaction ya Tanzania kama taifa baada ya Israel kutamka mara mbili kua sio nchi muhimu, na kumaintain good relation na Tanzania sio muhimu.
Watanzania mnasema nini? Tanzania kama taifa inasema nini? Je, itaendelea kua na uhusiano na nchi hiyo? Those are the question Membe needs to address publicly.
 
I know!!
Na kitendo cha wao kukaa kimya kinaweza kikatokana na wao kutafuta namna ya kuipotezea hiyo kauli kwasababu wanajua fika Israel wanamaanisha na maamuzi ya Tanzania hayawezi kuathiri Israel ila yanaweza yakaathiri Tanzania.

Kama tungekua na jeuri taarifa ingeshatolewa kwamba kutokana na dharau ya Israel, hatutaki uhusiano nao.But we don't. . . .
 
Hivi taarifa kamili huwa anazipata kwa nani? Lile suala la ushoga alipata taarifa kwa nani?
Balozi wa heshima alipotoa taarifa hakuitoa tu, ni lazima aliwasiliana na serikali kwasababu iliwasilishwa kwa waziri wa mambo ya nje wa Israel.
Kama taarifa ilikuwa ni ya uongo basi Membe alipaswa kuijibu pia.
Ehud kupitia wasemaji wake amesema hataomba radhi kwa vile msemo huo ameshautumia mara nyingi.

Hoja yangu ni kuwa Waziri membe ni miongoni mwa watu wanafiki sana. Hata ninaposikia anatajwa kuwa mgombea huwa nabaki nikisikitika. Suala la rada lilikuwa hivi hivi hadi BAE walipogoma kulipa ndipo tukamsikia.

Kaingilia kati pesa zirudishwe akiulizwa akina nani wanahusika anasema yeye si msemaji na hajui. Hajui lakini yupo kwenye mazungumzo pesa zirejeshwe!! Pesa zimerejeshwa hawaambi Watanzani ziko wapi.

Huyu Bernard Membe hana sifa ya aina yoyote kuwa kiongozi wa kitaifa. Sehemu kubwa ya kazi zake anazifanya kinafiki kwa kuwafanya watanzania mazuzu. Huyu mumuelewe ni mnafiki, narudia membe hana rekodi ya iana yoyote ya maana zaidi ya unafiki.
 
Membe is basically saying "I don't know what to say". Which is sad given the time this brouhaha has been in the news. Anachosema ni kwamba kila anayekutukana ni lazima aandike barua yenye letterhead , mhuri na sahihi, ikiorodhesha matusi yote. Sad.

Ukisikia kitu kimetangazwa na XINHUA kwa watu wanaoelewa kuwa XINHUA ni mouthpiece ya serikali ya China, halafu zimepita siku kadhaa hakuna mtu aliyewajibishwa XINHUA, na aliyesema kapewa nafasi ya kuomba radhi kakataa, hajachukuliwa hatua yotote, na serikali ya China haijakanusha, mwenye akili unajua kwamba kuuliza kwamba "Huu ni msimamo wa serikali ya China au?" ni swali la kizushi.

So goes for Reshet Klitat HaAliya/ Radio Israel.

Obviously hii either ni rookie gaffe or Wa Israel hawajali diplomacy na hawaogopi kusema ukweli ulio undiplomatic, obviously serikali ya Israel pamoja na Barak hawataki kukubali kuomba msamaha, obviously kwa kukataa kukubali wanaifanya hii rookie mistake iwe position ya serikali kwa sababu kwao ku apologize kutakuwa embarassing zaidi ya kukubali kwamba hii ni rookie mistake.

Kwanza wanaona Tanzania hatuna hata uhusiano wa kibalozi nanyi, pili nyie watetezi wa Palestina kila siku, tatu mnamtetea Iran awe na nuclear weapons, kwa hiyo kwa nini tu apologize kwa mtu ambaye hatuna chochote cha ku gain kwake? It's not like we are going to compete realistically for the Tanzanian vote in the UN kwa resolution ya kutaka Palestine iwe a member state.

Kwa msingi huu visiwa vya Kiribati huko South Pacific, vyenye watu takriban 100,000 na zero natural resources apart from tourist attracting beaches vinaweza kuwa muhimu kwa Israel kuliko Tanzania.

Ignorant statements like these makes one want to justify Iddi Amining all Israel nationals out of Tanzania, but you can't punish people for the mistakes of politicians.

This should be an argument against the notion that Israel is "Taifa la Mungu". Kama mungu angekuwa na taifa certainly asingeumba waziri aliye stupid kufanya needless undiplomatic gaffes kama hii.

Hivi anmgesema tu kwamba Uingereza na Ujerumani ni muhimu na si kama nchi zisizoendelea point yake isingeeleweka? Kulikuwa na ulazima gani wa kununua controversy bila sababu?

Humtukani hata ombaomba irrelevant ambaye huna haja ya kumtukana sio tu kwa sababu si sawa na ni ushenzi, lakini pia kwa sababu hujui huyu ombaomba kesho atakuwa nani na anaweza kukusaidiaje.Ndiyo maana naiita hii "rookie mistake". It is a wanton disregard for the most basic principles of civility and diplomacy (especially when nothing is at stake). Generality.
 
Kama tungekua na jeuri taarifa ingeshatolewa kwamba kutokana na dharau ya Israel, hatutaki uhusiano nao.But we don't. . . .

Mbona tulikuwa jeuri kumjibu haraka Cameron na issue yake ya ushoga na misaada?
 
Mbona tulikuwa jeuri kumjibu haraka Cameron na issue yake ya ushoga na misaada?

Just another move on the chessboard. . .
Ile wanajua wataanzisha NGOs kibao kutetea hivyo ufadhili hautakoma. Hili la sasa hivi ni either wajipendekeze au waonyeshe jeuri, inavyoonekana wamechagua kujipendekeza.
 
Lizzy, hakuna mtu anawalazimisha waisrael kuwathamini Watanzania. What we need to see ni reaction ya Tanzania kama taifa baada ya Israel kutamka mara mbili kua sio nchi muhimu, na kumaintain good relation na Tanzania sio muhimu.

Watanzania mnasema nini? Tanzania kama taifa inasema nini? Je, itaendelea kua na uhusiano na nchi hiyo? Those are the question Membe needs to address publicly.

Well, the deputy minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Mr Mahadhi Juma Maalim, told The Citizen Tuesday that the government has taken the issue seriously and is holding consultations over recent derogatory remarks

"We are holding meetings to see how we can respond to Mr Barak's comments. We will let you know when we are ready," he said during a telephone interview. Mr Barak has refused to apologise to Tanzania after branding the country as irrelevant as far as Israel's relations with other nations are concerned.

Source: The Citizen- Israel
 
][/SUB]
Hivi anmgesema tu kwamba Uingereza na Ujerumani ni muhimu na si kama nchi zisizoendelea point yake isingeeleweka? Kulikuwa na ulazima gani wa kununua controversy bila sababu?

Nadhani imetokea tu kwamba, incidentally, the names "Mauritania" and "Tripolitania" just happen to ryhme with "Tanzania" (off the bat at as it presumably were). Lakini, at the same time, looking at the bigger picture, Ehud Barak wasn't exactly deluded at saying what he didespecially given the inferior and virtually obscure status of Tanzania internationally.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Well, the deputy minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Mr Mahadhi Juma Maalim, told The Citizen Tuesday that the government has taken the issue seriously and is holding consultations over recent derogatory remarks

"We are holding meetings to see how we can respond to Mr Barak's comments. We will let you know when we are ready," he said during a telephone interview. Mr Barak has refused to apologise to Tanzania after branding the country as irrelevant as far as Israel's relations with other nations are concerned.

Source: The Citizen- Israel
They are taking too long to respond, as says Kiranga this silence is already a response. And as says Lizzy this tacit response does not make us proud of them.
 
They are taking too long to respond, as says Kiranga this silence is already a response. And as says Lizzy this tacit response does not make us proud of them.

One one hand, Membe anasema serikali hajapata taarifa, lakini naibu wake anasema kuwa the government has taken the issue seriously and is holding consultations. Which is which?
 
Nadhani imetokea tu kwamba, incidentally, the names "Mauritania" and "Tripolitania" just happen to ryhme with "Tanzania" (off the bat at as it presumably were). Lakini, at the same time, looking at the bigger picture, Ehud Barak wasn't exactly deluded given the inferior and virtually obscure status of Tanzania internationally.
On the contrary, nadhani he meant it. Maana alisema mara mbili, sio mara moja! mara ya kwanza alisema sio muhimu, na mara ya pili akasema hawezi kuapologize, he has more important matter to attend to! alafu kumbuka Tanzania has condemned Israel actions in Gaza in the past...
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom