Serikali Yatoa Tamko Hali Watanzania Nchini Israel

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Serikali imesema inaendelea kufuatilia kuhusu hali za Watanzania waliopo nchini Israel na kwamba taarifa zaidi zitatolewa pale itakapobidi.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 29, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi alipozungumza na wahariri na waandishi wa habari.

Amekiri uwepo wa baadhi ya Watanzania katika Taifa hilo hasa wanaosoma na kwamba taarifa kuhusu hali zao Serikali inaendelea kuzifuatilia.

"Serikali inafuatulia taarifa kwa ukaribu kupitia ubalozi uliopo nchini Israel na itakapobidi tutatoa taarifa, lakini tusiseme Mtanzania amepotea hadi tutakapokuwa na uhakika.

"Kwa sababu kwenye vita kila mtu anatafutia namna ya kujitetea hatuwezi kuwa na uhakika wa mtu kupotea hadi taarifa zitakapothibitishwa," amesema.


 
Back
Top Bottom