benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Kupitia ukurasa binafsi wa mtandao wa X (Zamani Twitter) wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika. Mashariki, January Makamba ameandika ujumbe kuwa mapema leo amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Eli Cohen
Ujumbe huo umeeleza kuwa Waziri Cohen ameahidi Serikali ya Israel kuboresha juhudi za kuwatafuta
wanafunzi wawili wa Kitanzania ambao hawajulikani walipo tangu Oktoba 7.
Pia Waziri Makamba ameeleza kuwa Waziri Cohen amemfahamisha juu mtazamo wa Israel kuhusu mzozo unaoendelea hivi sasa huku yeye (Makamba) akisisitiza msimamo wa Tanzania kwamba kipaumbele kinapaswa kutolewa kwa:
(a) Kufuata sheria za kimataifa za kibinadamu, hasa ulinzi wa maisha ya raia
(b) Kusitisha operesheni za kijeshi ili kuruhusu juhudi za kibinadamu zisizo na vizuizi
(c) Kuanzisha upya mchakato wa amani ikiwa ndio suluhisho kwa mataifa mawili kama nguzo yake.
Tulikubaliana kuendelea kuwasiliana.