Fursa Pesa
JF-Expert Member
- May 30, 2012
- 4,437
- 3,261
Anayeijua kweli hakika ni Mwenyezi Mungu tu,sisi wanadamu bado tunahitaji msaada mkubwa juu ya kweli kutoka kwa binadamu wenzetu kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
Binafsi sijui chochote kuhusu hili sakata na hivyo sina haja yoyote ya kutaka kujua chochote kuhusu hili.
Ni bora mara mia saba kwa Mh.Membe kutokuzumgumza chochote kuhusu hiki ambacho yeye hakijui kwa kuwa kukizumgumzia kunaweza;
1.Kuendeleza migogoro isiyo ya lazima na vyombo vya habari.
2.Kumshushia hadhi yake yeye kama waziri kiasi cha kumfanya kutumia title ya uwaziri kwa masuala binafsi kitu ambacho si kizuri kwa kiongozi wa umma.
Ni busara kwa mambo mazito kama haya yakatatuliwa mahakamani,kwa kuwa haiwezekani eti gazeti linaandika juu ya uhusika wa fulani kwenye kitu fulani bila ya ushaidi wa kutosha.Hapa napata shaka juu ya taaluma za watu hawa.
Labda nitoe rai kwa vyombo vya habari hususani magazeti ya kuwa wasipende kuandika habari ambazo bado ni mbichi/tetesi ama kwa kufuata hisia ya mtu/kundi fulani la watu ili eti baadae iwe kitu fulani na wao wenye vyombo hivyo waonekane wana mchango mkubwa kwa kundi fulani/mtu fulani kwa manufaa yao binafsi.
Palipo na haki pana wajibu,sote tutimize wajibu wetu kwa nafasi zetu na tusisahau ya kuwa cheo ni dhamana na wakati huohuo tusitumie cheo/vyeo vyetu kwa manufaa binafsi hakika hatutafika.