Membe atoa tamko juu ya kutekwa kwa Kibanda

Membe atoa tamko juu ya kutekwa kwa Kibanda

Naomba nitofautiane nawe Ben Saanane...hilo tamko haliko 'professional'. Membe ametuhumiwa/kutajwa kuhusika katika hilo sakata katika 'capacity' ya Membe..na sio 'Waziri wa Mambo ya Nje', yaani kiongozi wa serikali. Sasa kwa nini atoe tamko kama Waziri?

Tuhuma hizo zilikua derived kutoka kwenye mahojiano yake yeye kama waziri wa mambo ya nje kwenye kipindi cha ITV
 
Last edited by a moderator:
Ben nimekushusha sana kama jk. Huwezi kusifia tamko la kipuuzi kama hili na yeye alisema hadharani ana maadui 11 na waandishi wa habari wakiwemo.

Hiyo ni haki yako kidemokrasia mkuu.Hata kama tunatofautiana kiitikadi tusi-compromise principles.
Hapo Membe amejibu kwamba hajawahi kuwa na uhusiano mbaya na Kibanda.Lengo ni kukanusha ile insinuation kwamba Kibanda alikua miongoni mwa maadui.Huwa napinga matumizi mabaya ya matukio ya kibinadamu kwenye masuala ya kisiasa na kujinufaisha kisiasa bila kujali sentiments za victim(Kibanda) na familia yake.Hili halina itikadi
 
mi mnazidi kunichanganya kwa hiyo muhusuka ni Membe au Lwakatare?
 
Labda niwashauri tu wana JF hasa wale verified users.

Mambo haya ya kisiasa yanayohusishwa na umafia, kama hujui details za yanayoendelea nyuma ya pazia ni bora uwe msomaji tu na kujiweka mbali na kushabikia.

Kama una ndugu au rafiki anayejihusisha na siasa mwambie akupe picha ya jinsi mambo ya siasa yanavyofanyika behind the scenes. Hizi taarifa zinazoonekana kwenye magazeti,tv na kusemwa kwenye redio hazifikii hata 1/8 ya yanayoendelea nyuma ya pazia...
 
Kama kawaida yao, Membe leo hii anatuomba Watz tumsaidie kung'amua kiburi wamepata wapi hao waandishi! Hivi hawa viongozi kweli wamewahi kujiridhisha kuwa uwezo wao wa kufikiri ni mdogo?

Wananchi wamekuwa wakililia serikali kutolea majibu matukio yakutisha yanayoitikisa nchi, kwamba serikali ina majibu. Sasa Membe anapata wapi utashi wa kutaka Wananchi wamsaidie na sio serikali?
Ndugu zangu, Udhaifu huu ambao kila mwanaCCM anauonesha ni kiashiria tosha kwamba tumekwisha.
 
Maadui 11 ni:
1. Njaa
2. Maradhi
3. Ujinga
4. Kuinua uchumi wa nchi
5. Kuboresha miundombinu
6. Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama
7. upatikanaji wa umeme wa uhakika
8. Kuondoa ufisadi
9. kuondoa rushwa
10. Koboresha elimu ya juu
11. Economic empowerment

And that's precisely my point. Hakuta jina, so kila mtu yuko huru to kutaja chochote/yeyote!
 
Membe hana ujanja, tukio hili na Dr. Ulimboka yamefanywa na watu wao wa magogoni.

Video imesababisha mtu kukamatwa na kuhojiwa nadhani matamshi ya membe yanatosha kabisa kuhojiwa hili halina ubishi press release haitoshi kuhalalisha kutohusika kwake!
 
Aliposema watakimbilia Kenya niliikosoa hiyo kauli maana ni tusi kidiplomasia kwa nchi ya Kenya na kauli ya Membe kama Top Diplomat wa Nchi it is uncalled for.Inaweza kupeleka wrong gesture kwamba Kenya ni safe haven ya wahalifu maana alitaja kwamba maadui zake hao(Wahalifu)watakimbilia Kenya.Hizi ni reckless utterance kwa waziri wa mambo ya Nje
 
Tetty kumbuka hata Dk.Ulimboka aliwataja waliomteka na kumtesa but no any reaction taken.

Unafanyaje kama serikali yetu pamoja na wale tuliowapa dhamana ya kuliongoza taifa letu wanafanya unyama huu na bado wanatuona watanzania wajinga?Na mbaya zaidi kutumia teknlojia za kisasa ili kumpa mtu hatia asiye na hatia?Ona kwa Dr.Ulimboka kuna Mkenya yupo jela na hajui hatima yake leo Lwakatare siyo haki na wala siyo sahihi ndio maana nasema kwa njia hii shimo la panya wataingia wasiokuwemo na waliokuwemo au waliokuwemo wapone na wasiokuwemo wapate varangati la paka.
 
Labda niwashauri tu wana JF hasa wale verified users.

Mambo haya ya kisiasa yanayohusishwa na umafia, kama hujui details za yanayoendelea nyuma ya pazia ni bora uwe msomaji tu na kujiweka mbali na kushabikia.

Kama una ndugu au rafiki anayejihusisha na siasa mwambie akupe picha ya jinsi mambo ya siasa yanavyofanyika behind the scenes. Hizi taarifa zinazoonekana kwenye magazeti,tv na kusemwa kwenye redio hazifikii hata 1/8 ya yanayoendelea nyuma ya pazia...

Mkuu ndio maana tunafungua thread ati. Hata wewe unaweza kutuanikia wazi, kama unaona kuna sensitive issues private message itakubalika vilevile.
 
Niliwahi sikia wambea wa mjini wanasema Membe ni rafiki mkubwa wa Rama Ighondu wa Ikulu ya Magogoni!!
 
Minister_Mr_Bernard_K_Membe2.jpg
 
taffu69 View Post

Bernard Membe angekuwa ni mcha Mungu wa kweli na anayeheshimu Katiba ya Nchi, asingedhubutu asilani kuutangazia umma wa Watanzania kuwa ana maadui 11 ndani ya Tanzania na kuwa atawashughulikia kwa nguvu na mbaya zaidi kama sijakosea aliongeza kuwa ikifika 2016 watahama nchi ama watakimbilia nchi jirani. Angekuwa kweli mcha Mungu na kama aliona kuwa ana maadui, angetoa taarifa kwenye vyombo vya usalama badala ya kutoa vitisho tena kwa kuutangazia umma.

Kaka, acha chuki na propaganda zisizo na kichwa na wala miguu, atawashukughulikia kivipi wakati yeye si polisi wala si hakimu, kuna vyombo vya kutoa haki kama kuna watu wana makosa. Nakushauri ujitahidi kubadilisha topic, maana kama ni ngoma hiyo umeipiga sana sasa haina hata utamu tena.

Unaposema niache chuki na propaganda sijui una maana gani. Hayo maneno ya kuwashughulikia maadui zake 11 alitamka Membe mwenyewe tarehe 16 Julai 2012 na sio maneno yangu. Labda uwe unaongea jambo usilolijua. Kwa kukusaidia soma hiyo habari kwenye link,

VIJIMAMBO: URAIS WAZIDI KUWATESA WANASIASA
 
Membe tukusaideje mzee? Tulijua utakuja tu humu kupinga kama ilivyokawaida yenu magamba. Lakini mbona hujapinga ulisema una maadaui 11 kati yao 2 waandishi au ulimaanisha mafarisayo?
 
sikutegemea kama angeweza kujibu tuhuma nzito kama hizi krahisi na kifupi hivi. hebu aseme vizuri basi wakati anahojiana na mwandishi wa habari kwenye kipindi cha dakika 45 pale ITV,alimaanisha nini kusema kuna maadui 11 na wawili ni waandishi wa habari na atawashughulikia alikuwa anamaanisha nini? au na hilo ni la uongo kama ndo hivyo basi aanze kukanusha tokea hapo wa tz watamwelewa,lakini vinginevyo anachanganya sana. nakumbuka mwalimu wangu alishawahi kunambia kauli moja tu inaweza kuchafua na kuharibu maana ya ujumbe mzima. one word can spoil the whole story. Je anakumbuka kauli ya chenge ya VIJISENTI, kauli ya mkapa,mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe zilivyoleta tafsiri tofauti kwa watanzania?.haya tusuburi wanasheria wake wamshauri nin cha kufanya
Nashukuru kwa kumkumbusha kwenye hizo nyekundu.Hata mimi nilitarajia Mhe.Bernard Membe atajibu tuhuma hizo.Alitarajia watu wayasema nini kwa kauli zake alizotoa hadharani?Kama si Kibanda, basi ataje waandishi wa habari ambao ni adui zake ili tumtoe kwenye tuhuma hii.
Naomba nikukumbushe Ndg Makinya kuna usemi mwingine wa Kiingereza unaosema "Words like eggs once word is spoken and once eggs is broken,can not be ammended again ",
 
Membe anajua vyema kama mchana unavyofuatiwa na usiku kuwa tusingetegemea aseme anahusika,anapanga kuhusika au ana sababu za kuhusika.Kama diplomat na spy mzoefu na akichanganya na akili ya kuzaliwa angelikaa kimya aone kama BASHE NA TIMU WANGESEMAJE!Bado kitendawili kimoja hajakitatua wale maadui 11 wakiwemo waandishi wa habari 2 ni kina nani ,anawashughulikiaje?Huyu MWAFRIKA vipi?
 
Na waandishi watazid kuuwawa kwa sababu ya upumbavu wao.mwanahalisi limefungiwa wanacheka cheka tu

Haswaa! kuna kipindi muungano wa asasi za kutetea haki za binadamu ulitoa tamko kuhusu kufungiwa kwa mwanahalisi. Cha kustaajabisha kuna muhariri wa jukwaa la wahariri alitokea mbele ya vyombo vya habari na kusema "Tamko lile sio la wanahabari"...
 
Mtaji huu wa kutekwa watu utawalipukia sasa hivi kwa tamaa ya kuutumia kwa kila adui. Mara ni Membe mara Rwakatare, mara chadema.
 
Back
Top Bottom