Membe atoa tamko juu ya kutekwa kwa Kibanda

Anayeijua kweli hakika ni Mwenyezi Mungu tu,sisi wanadamu bado tunahitaji msaada mkubwa juu ya kweli kutoka kwa binadamu wenzetu kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu.

Binafsi sijui chochote kuhusu hili sakata na hivyo sina haja yoyote ya kutaka kujua chochote kuhusu hili.

Ni bora mara mia saba kwa Mh.Membe kutokuzumgumza chochote kuhusu hiki ambacho yeye hakijui kwa kuwa kukizumgumzia kunaweza;

1.Kuendeleza migogoro isiyo ya lazima na vyombo vya habari.

2.Kumshushia hadhi yake yeye kama waziri kiasi cha kumfanya kutumia title ya uwaziri kwa masuala binafsi kitu ambacho si kizuri kwa kiongozi wa umma.

Ni busara kwa mambo mazito kama haya yakatatuliwa mahakamani,kwa kuwa haiwezekani eti gazeti linaandika juu ya uhusika wa fulani kwenye kitu fulani bila ya ushaidi wa kutosha.Hapa napata shaka juu ya taaluma za watu hawa.

Labda nitoe rai kwa vyombo vya habari hususani magazeti ya kuwa wasipende kuandika habari ambazo bado ni mbichi/tetesi ama kwa kufuata hisia ya mtu/kundi fulani la watu ili eti baadae iwe kitu fulani na wao wenye vyombo hivyo waonekane wana mchango mkubwa kwa kundi fulani/mtu fulani kwa manufaa yao binafsi.

Palipo na haki pana wajibu,sote tutimize wajibu wetu kwa nafasi zetu na tusisahau ya kuwa cheo ni dhamana na wakati huohuo tusitumie cheo/vyeo vyetu kwa manufaa binafsi hakika hatutafika.
 
Ukifikiri kuwa binadamu huishi na kufa,
Na kuwa hakuna ajuaye siku yake ya mwisho,
Utashindwa kuuelewa moyo wa atakayeingia ikulu akiwa na furaha baada ya vitendo katili namna hii..
We'd rather not have politics if politics cant get better than these acts of mediocrity.

Watawala wa Tanzania kwa sasa wamekuwa wajeuri na wakatili zaidi ya ukatili wa mkoloni wa Kijerumani na Mreno tuliowasoma kwenye historia na kuhadidhiwa na wazee wetu.
 
Nilisema sana humu ndani na thread nyingine kuwa closed bila hata kuchangiwa.nilieleza ugumu wa kuishi na kuitumia devided ccm.ccm kwa ndani kuna movement za kidini ,uraisi ukakabila,matabaka ya kiasia ,makundi ya urais, etc,Ni ngumu kwa mwenye akili timamu kuweza hata kuwappease huku ukiwa salama.Kipanda na wanafiki wengine hawajasoma upepo na kuona usalama uliopo kambi ya ushindi ktk cdm
Kwa walionsikia bashe ktk maazimio ya wadau wa habasi ni ataona Mkanganyiko..kijana alikuwa anaongea km anajua aliyehusika ila si waliokuwa wa wakimaanisha wadau wengine.mbaya alikuwa anaonekana kupika majungu huku akiweka hisia za uongo. Kwa ufahamu mdogo wa wanaccm na desperation zao kwa kiasi cha kuona bora nchi iangamie kuliko kuachia nchi,hawazi ona kuwa matafia yanaona na yanakua sana hizi footprints ni za nani..
Sesikali haijui watu kuwa armed ni issue ya siku 3.watu wanatishiwa na kujeruhiwa tanzania polisi wapo kimya tuu.watu wanauwawa kova yupo busy kusema ni wahuni na cdm.soon atapwaya hata kazi aliyopewa ktk hiyo nafasi ya kimkakati.before 2014 patakuwa na media zenye malengo na nguvu na ccm hawakuwa na control na watakuwa wamekula hasara kununua na kuua watu
.
nafisi.
 
Maadui 11 ni:
1. Njaa
2. Maradhi
3. Ujinga
4. Kuinua uchumi wa nchi
5. Kuboresha miundombinu
6. Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama
7. upatikanaji wa umeme wa uhakika
8. Kuondoa ufisadi
9. kuondoa rushwa
10. Koboresha elimu ya juu
11. Economic empowerment

makelemo mtu haitaji degree kutambua upande wako.inshort unajaribu kufanya kitu ambacho ni kama kupaka rangi upepo huyo unayeye mtetea na utetezi unaoutoa ni mwepesi sana.hayo yanayosemwa huyo bosi wako membe aliyasema kwa mdomo wake kwenye tv na ikaandikwa kwenye vyombo vingine vya habari na hakuwahi kupinga.hao maadui uliyowataja hapo juu ni wako siyo wa membe.......mwambie membe alishaingia choo cha kike long time pamoja na support ya shemeji yake na dada yake. Mkumbushe tu kuwa watu wanalikumbuka suala la oic pia.
 
Waziri Membe akanusha kuhusika tukio la kumdhuru Mhariri Kibanda.

membe+px.jpg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe

KWA UFUPI


Usiku wa kuamkia Machi 6, mwaka huu, Kibanda akiwa anarejea nyumbani kutoka kazini alivamiwa na watu wasiojulikana na kushambuliwa kiasi cha kuharibiwa jicho, kukatwa kichwa, kung’olewa meno na ukucha.


Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amekanusha madai ya kuhusika na vitendo vya kikatili alivyofanyiwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.


Juzi gazeti la Mtanzania linalochapishwa na Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, lilitoa habari inayomtuhumu Waziri Membe kuhusika na uhalifu huo, huku ikinukuu kauli zake alizotoa katika kipindi cha televisheni moja Julai mwaka jana, aliposema ana maadui kumi na moja kati yao wamo waandishi wa habari wawili.


Usiku wa kuamkia Machi 6, mwaka huu, Kibanda akiwa anarejea nyumbani kutoka kazini alivamiwa na watu wasiojulikana na kushambuliwa kiasi cha kuharibiwa jicho, kukatwa kichwa, kung’olewa meno na ukucha.


Hata hivyo akizungumza kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Membe alisema ameshangazwa na taarifa hizo na kusisitiza kuwa hahusiki.


“Nimeshangazwa na kusikitishwa na habari hizo, napenda niwahakikishie Watanzania wenzangu kwamba sijahusika, sikuhusika na sina sababu ya kuhusika kwa nanma yoyote ile,” alisema Membe na kuongeza:


“Sina nia, genge wala fedha za kufanya shughuli kama hiyo. Katika maisha yangu yote, sijawahi kugombana naye (Kibanda) na hajawahi kunifanyia ubaya wowote. Kwa kifupi sina uhasama na Kibanda.”


Membe anayetajwa kuwa mmoja wa watakaowania urais mwaka 2015 kupitia CCM, alisema habari hiyo ina malengo ya kisiasa.


“Huu ni mwendelezo wa mkakati wa kisiasa wa kunichafua ambao umekuwa ukiendelezwa na wale wasionitakia mema,” alisema.
Hata hivyo, Waziri Membe ambaye hivi karibuni alisema hatagombea tena ubunge, aliwashukuru watu waliomtumia salamu za kumtia moyo huku akihoji ujasiri wa watu wengine kusema uongo hadharani.


“Jeuri na kiburi cha namna hii hakiwezi kutokana na sheria za nchi, haki ya kikatiba wala hofu ya Mwenyezi Mungu. Naomba Watanzania wenzangu mnisaidie kutegua kitendawili hiki,” alisema Waziri Membe na kuongeza:


“Naamini ukweli kuhusu suala hili utajulikana na yeyote mwenye ushahidi aonyeshe uzalendo wake kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.”
Naye Ofisa Mkuu Mtendaji wa New Habari, Hussein Bashe alisema wao wanachotaka ni Waziri Membe ahojiwe kutokana na matamshi yake.


Bashe alidai kuwa, Waziri Membe analalamikiwa kwa mazungumzo yake kwenye kipindi katika kituo cha televisheni moja kudai ana maadui kumi na moja.
“Huyu bwana alitangaza ana maadui kumi na moja na kati ya hao wawili ni waandishi wa habari,” alisema Bashe.


Bashe aliongeza kuwa Waziri Membe alikwenda mbali zaidi na kudai angewashughulikia maadui zake.
“Sasa tayari kuna mwandishi ameumia na yeye (Membe) ana maadui waandishi ndiyo maana tunataka ahojiwe,” alisema Bashe.
Pia, aliongeza kuwa suala hilo lilijadiliwa kwenye kikao cha Wadau wa Vyombo vya Habari hivi karibuni.

Alisema Waziri Membe anatakiwa kukanusha matamshi hayo siyo suala la kuhusika kumteka Kibanda. Bashe alisema wanaamini vyombo vya dola ndiyo vyenye uwezo wa kumsafisha Waziri Membe, kwa sababu wao wana ushahidi wa kanda wakati anatoa matamshi hayo lakini siyo kwamba wanamhusisha moja kwa moja na tukio hilo la kumdhuru Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri.
Waziri Membe akanusha kuhusika tukio la kumdhuru Mhariri Kibanda - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
kitalolo, Lokissa
mimi simpendi kabisa huyo aliyetoa tamko
kwa kweli namwona wa baridi mno namfananisha tu na yule wa elimu hata matamko yake
yaone yalivyokaa kiswahili swahili, eti ndiye ajaye,
hasemi kuhusu aliyeumizwa anajitahidi kujitetea, kwani nani asiyemjua alivyo na visa na visasi.
kitalolo sipendi siasa kwa kuwa inanifanya nione uchungu kutokana na mambo yanayotendeka.

loh,
Mamndenyi na huyu naye ansema tumelogwa
 
Kuna mahali anajichanganya sana. Bado anayo maswali ya kujibu. Yuko kwenye corner. Na alichangia mwenyewe kujiweka huko.
 
kitalolo, Lokissa
mimi simpendi kabisa huyo aliyetoa tamko
kwa kweli namwona wa baridi mno namfananisha tu na yule wa elimu hata matamko yake
yaone yalivyokaa kiswahili swahili, eti ndiye ajaye,
hasemi kuhusu aliyeumizwa anajitahidi kujitetea, kwani nani asiyemjua alivyo na visa na visasi.
kitalolo sipendi siasa kwa kuwa inanifanya nione uchungu kutokana na mambo yanayotendeka.

loh,

Hata mimi sipendi siasa kama siasa ila nafwatilia tu jinsi mambo yanavyoenda Tanzania na Duniani kwa ujumla si unajua hawa wanasiasa na siasa ndio zinadrive kila kitu hata uchumi maana mkiwa na sera mbovu zilizotokana na wanasiasa kama wabunge tunavyowachagua wanaaenda kukaa bungueni kutunga sera ambazo zitatekelezwa na serekali na wanaposhinda kuisimamia serekali katika kutekeleza majukumu basi kila kitu kinakuwa worse. si elimu, afya, usalama, nk
 
yote uliyoeleza ni sawa lakini pale uliposema tutulie tusubiri vyombo vya ulinzi vifanye kazi yao,ndipo kwenye mashaka,maana ya Arusha,Ulimboka,Mwangozi mpaka sasa haijulikani
 
Maadui 11 ni:
1. Njaa
2. Maradhi
3. Ujinga
4. Kuinua uchumi wa nchi
5. Kuboresha miundombinu
6. Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama
7. upatikanaji wa umeme wa uhakika
8. Kuondoa ufisadi
9. kuondoa rushwa
10. Koboresha elimu ya juu
11. Economic empowerment

ungekuwa mgombea ningekupa kura....chezea politics ww
 
Kibanda alidi ktk maelezo yake hawajui watesi wake, ingawaje membe anatuhumiwa tusubiri atoe majibu yake ndipo tumhukumu
 
Mbona Membe hazungumzia kilichoandikwa na mwandishi. Mwandishi alifanya reference ya matamshi yake yeye Membe kuhusu maadui aliowasema japo hajatutajia majina. Atufafanulie maadui wake ni wapi hao ambao ni waandishi wawili??

Asibwabwaje tu bila kujibu hoja ya alichokiandika mwandishi. Akitaka kujisafisha atueleze hao maadui zake ni akina nani na je aliposema ata-deal nao alikuwa na maana gani ???
maneno ya Membe ni ya hatari zaidi kuliko ya Lwakatare kama polisi wetu wangekuwa makini
 
kitalolo, bunge? ni makomedian
siku moja niko likizo kijana wangu anasema naangalia komedi,
nikavutiwa ni komedi gani, kuangalia ni bunge letu,
nilisikitika niliona aibu tena nikajisikia vibaya
kama watunga sheria wamefikia hali hii tena eti ni muhimili wa tatu wa nchi/serikali, aibu hii tutaenda nayo wapi.

Hata mimi sipendi siasa kama siasa ila nafwatilia tu jinsi mambo yanavyoenda Tanzania na Duniani kwa ujumla si unajua hawa wanasiasa na siasa ndio zinadrive kila kitu hata uchumi maana mkiwa na sera mbovu zilizotokana na wanasiasa kama wabunge tunavyowachagua wanaaenda kukaa bungueni kutunga sera ambazo zitatekelezwa na serekali na wanaposhinda kuisimamia serekali katika kutekeleza majukumu basi kila kitu kinakuwa worse. si elimu, afya, usalama, nk
 
Last edited by a moderator:
kitalolo, bunge? ni makomedian
siku moja niko likizo kijana wangu anasema naangalia komedi,
nikavutiwa ni komedi gani, kuangalia ni bunge letu,
nilisikitika niliona aibu tena nikajisikia vibaya
kama watunga sheria wamefikia hali hii tena eti ni muhimili wa tatu wa nchi/serikali, aibu hii tutaenda nayo wapi.

sometimes its better you watch the comedy show because you will add something to your health than watching our bunge show
 
Last edited by a moderator:
Naipenda sana hii battle huku kambi ya lowassa inafanya kazi ya kumchafua Membe na kambi ya Membe inafanya kazi ya kuichafua CDM, hawa jamaa wamegawanyika vibaya napenda sana huu mnyukano uendelee at the highest level tuujue ukweli
 
WanaJF naomba mnijuze kuhusu uandishi wa barua. Kama Bw Membe amesaini na "ku-declare" kuwa yeye ni "Waziri wa mambo ya nje na....." si alitakiwa atumie "official headed paper"?
 
Ben, kuhusika au kutohusika kwa Membe ni yeye atakayetengua kitendawili hiki. Alianzisha mwenyewe hilo sakata. Nafikiri anachotakiwa kufanya Membe ni kuwataja maadui zake 11 miongoni mwao waliwemo waandishi wawili kama alivyonukuliwa na ITV mahojiano ya Dk 45. Awataje na aseme wanahusikaje kumharibia au uadui wao na yeye ni upi. Pili, atoe ufafanuzi wa kauli yake kwamba akioteshwa, 2016 kuna watu watahama nchi wakaishi mombasa na kwa nini mombasa? Mimi naamini Membe anaweza akawa hajui wala hahusiki na kuteswa kwa Kibanda lakini, ajue kuwa malalamiko yake ya kuwa na maadui atakuwa ameyaweka wazi kwa angalau rafiki yake mmoja au wawili na hivyo bila yeye kufahamu na kwa kufikiri kuwa kwa Membe kupata nafasi kubwa serikalini nao pia watafaidi, basi yawezekana wao ndo wanamsaidia rafiki kujibu mapigo bila kumhusisha Membe. Yote yanawezekana. Ajibu hayo na kuyaweka wazi, la sivyo kila mwandishi atakayepatwa na janga bado yuko kwenye seti ya maadui wawili wa Membe mpaka tutakapowafahamu ni wepi. Lets be serious when it comes to National issues and its political future. I assure you, this is taken lightly today, but it has a very big political impact to Membe and his alliances in future, shouls somebody else raise to power. Asijaribu kukwepa, alianzisha jambo alimalize maana polisi hawataki kumhoji kwa kuwa hawana tabia ya kuhoji vigogo. Muda utaamua....................
Very Good,Professional,short and clear......

Kwenye ile thread iliyomhusu Membe nilishauri kwamba kuna haja ya Membe kufanya press juu ya uhusika au kutohusika kwake mapema.
 
Hii statement ya Membe yakusema "Sina nia wala fedha zakufanya hivyo" Ina utata mkubwa sana. Kwani zile fedha za Ghaddafi yeye na kundi lake walishazimaliza? Zilitolewa kwa kazi nyingine nyie mnazitumia kuumiza wengine ili mbaki madarakani.
Huu mpango mzima Membe anaufahamu vizuri sana; ndio maana amechukua muda mrefu kutengeneza tamko. Nafikiri ingekuwa ngumu sana kwayeye kuongea na vyombo vya habari directly, kwani dhamira yake inamtesa na ndio maana amekuwa akitafutwa kwa simu kwa muda sasa bila kujibu.
Haya makundi JK anawachanganya sana. Kwa kila kundi anaonyesha support yake behind the scene; hivyo kila mmoja anaamini ana support ya mzee. Sijui ni kwanini hawajamjua mwenzao anavyong'ata na kupuliza na hivyo anaweza kuwageuka yeyote kati yao wakati wowote. Au kwavile the first son alisema raisi hawezi kutoka kaskazini basi Membe anajua ni yeye mwenye support kubwa ya mzee. Membe anaamini ushindi wake utaletwa na JK na TISS na si kura za watanzania. Na hivi ameshaaga kwenye jimbo mbona kutakuwepo kivumbi come that 2015.
 
Very Good,Professional,short and clear......

Kwenye ile thread iliyomhusu Membe nilishauri kwamba kuna haja ya Membe kufanya press juu ya uhusika au kutohusika kwake mapema.

Mdogo wangu Ben, kidogo rudia kusoma alicho kiandika Bernard Membe and then rudia alicho kisema Bashe (hapa tuondoe mapenzi ya nani anampenda nani au nani yupo kambi ipi) Bashe kama Mwanahabari alinukuu matamshi ya Membe akiwa hewani ndani ya dakika 45, alisikika akisema anao maadui 11, 2 kati yao ni waandishi wa habari, mara kuna waandishi tayari yamewakuta ya kuwakuta, kumbuka pia familia ya Raisi (mama na mwanae) wameonesha pasipo shaka kuwa upande wa Membe kwenye mbio za kwenda Ikulu though hatuna uhakakia na upande wa rais mwenyewe kwenye hili, kwa akili ya haraka haraka, Membe kwa mfano kama ana nia mbaya na mtu yeyote, je atashindwa kutumia vyombo vya dola kufanya unyama wowote? Kwa nafasi aliyonayo na uhusiano alionao na mkuu wa kaya? Wanapo sema watu wamwogope Mungu, hvi kweli kuna kiongozi ndani za ccm mwenye ujasiri wa kuwaambia wengine wamwogope Mungu? Mh, sijui, bado sijaona hiyo professionalism kwa Membe, alipaswa aidha kukataa kwamba hakutamka yale maneno ya vitisho au kuwataja hao maadui zake ili tujiridhishe kuwa Kibanda sio miongoni mwao.
 
Back
Top Bottom