- Mkuu PM vipi tena Kitine amemuita Membe, mwizi anayeficha hela nje agombee urais nazo, sasa akiitwa kingedu hutaki vipi? Una tatizo na Membe nini mkuu wangu, hafai kwa kosa gani hasa alilofanya kwenye policies zake akiwa Wizara ya nje?
- Kwenye kampeni za siasa kuchafuana ni kawaida, lakini hukalii kukumbatia ya zamani unasahau unaanza upya, I mean wacha chuki na Waziri Membe, kama ana makosa kwenye policies zake ziseme, lakini ya kampeni za siasa yalishapita sasa yupo kwenye kutawala, onyesha mapungufu yake kiutawala,
- Kitine hana u-senoir wowote ni simply muongo sana na ni mwizi, tena yeye na mkewe, ila kwa vile system yetu ni ya kusameheana ndio maana ana ubavu hata wa kuita wengine wezi, nashangaa mtu makini kama wewe kumuita a proven thief wa hela za wananchi kwamba ni senior, senior wa nini hasa? labda wizi wa hela za wananchi, wananchi wanakufa Muhimbili pale kwa kukosa dawa, wengine wanadanganya na kuiba hela za wananchi hao hao na kwenda nje kufanya shopping, wewe unamuita senior pleaseee!
- Waziri Membe na wananchi wote wa nchi hii wana haki ya kugombea anything, hawa kina Kitine ndio tatizo kubwa sana kwa taifa letu, maana ni majungu majungu tu alipokuwa usalama aliwahi kumakamata nani? PM wewe nakuheshimu sana kwani najua ni mtu makini sana lakini huwa una tatizo sana na mtu yoyote anayetaka uongozi CCM, isipokuwa Lowassa tu, huwa sikuelewi!
William.