Membe amshukia KITINE, amfananisha na "Kingwendu"

Hivi Membe anavyotuambia kwamba aligombea ubunge baada ya kusikia minongonezo hizo ni kauli za kutoa kiongozi mkubwa serikalini kama yeye? Tanzania bana ni zaidi ya uijuavyo. Hizo whisper ultras anazosema Membe kama zinamsaidia yeye hilo ni juu yake na maluweluwe yake yanayoendelea kichwani mwake. Lakini aliita waandishi wa habari bila aibu akasema hivo, dah. Anyway ni mwanaccm na hicho ndo chama kinachoongoza serikali. Mungu tunusuru hata kabla ya 2015.

Duh, kumbe wala hujui kwanini aliita waandishi wa habari na bado unanguvu ya ku draw conclusion ya kwanini aliita waandishi! Unanikumbusha mtoto wa rafiki yangu moja, siku moja rafiki yangu akamwambia mtoto wake "vaa vizuri na ingia kwenye gari", mtoto akasema "sawa baba". Akaenda kuvaa vizuri na kurudi nakuingia kwenye gari, wakiwa wanatoka getini mtoto akamuuliza babake "hivi baba tunakwenda wapi?" Babake akasema "eboh! sasa wewe ulifikiaje hatua ya kuvaa, kuingia kwenye gari na kufunga mkanda bila kujuwa unakwenda wapi?"
 
Duh, mkuu yaelekea wewe ni mgeni hapa Duniani. Basi ngoja tukueleze haya juu ya huyu Kingwendu:

1) Alijaribu kusomea PhD miaka 7 Canada, akashindwa na kurudi na PhD ya kujisingizia. hajamaliza PhD wala hana PhD. Ni miongoni mwa wanaodanganya kwamba wana PhD, hiyo ni fact.

2) Kingwendu alitimuliwa madaraka na Nyerere baada ya kuchakachuwa gari 2 kati ya gari 6 zilizookuwa zimekabidhiwa Tz kutoka Sheli Sheli. hiyo nayo ni fact.

3) Kingwendu alimdanganya Mkapa hadi mkapa akaidhinisha dola $63,000 kupitia wizara ya afya (sio dola 50,000 kama wanavyokosea magazetini) kwa matibabu feki ambayo yalitengenezewa risit fake na jamaa wa Nijeria aliyekuwa anajilia uroda kwa mke wa Kingwendu Toronto. Kingwendu alipobanwa, akazirudisha dola $60,000 bila kuwaambia waTz alizipata wapi, kuona ameumbuka Kingwendu akahonga kamati ya bunge. Kamati ikala mkwanja na bado ikamwambia Membe, naye hakufanya ajizi akamwangamiza Kingwendu. Na hiyo ni fact.

Hitimisho: Kingwendu amtaje waziri anayemtuhumu ili ngoma hii inoge, vinginevyo ana kila sifa ya kuitwa Kingwendu, zee la majungu, na ushauri wanggu hasipewe hata sekunde 2 kwenye Tv au magazeti hadi hapo atakapotaja jina la waziri anayemshutumu. Yaani yeye anamjadiri mwizi dk 15 lakini ukimuuliza jina anasema "kafanye uchunguzi". Kingwendu at best.

Nahisi umekurupuka kujibu comment yangu nadhani WJM anajua nini nilikuwa namaanisha, ulichofanya wewe ni kujaladia tuhuma za kitine kwa kuziita facts ambapo sijui proof/details za uhakika nizipate wapi labda waweza kunisaidia,sakata hilo nalikumbuka ila sina kumbukumbu nzuri kuhusu undani wake, anyway let me do my homework!
 
Membe mnatuficha wewe na JK ndugu wa DAMU. Tunaelewa mamake Kikwete ni mama yako pia.
Tukikuchagua tutakuwa tumechagua msanii namba mbili!! HATUKUHITAJI JOKA LA MDIMU.

Kastarehe fanya homework kidogo basi kabla hujatapika. Membe hana chembe ya undugu na JK, au kama Elimu yako haitoshi kiganjani kwako basi uliza huko Rondo, Lindi anakotoka Membe au Msoga, Pwani kwa JK. Adithi za vijiweni vinashusha thamani ya JF na kutufanya tuwe mbali na great thinkers.
 
Membe ana haki ya kumuita mtu aliyetoa tuhuma zile kwa jina la kingwendu ambaye ni mganga wa kienyeji. Ni vizuri tukafika mahali watu wakawa wawazi kama wanataka kisaidia hii nchi mtu unaenda kwenye vyombo vya habari unakaa dakika 45 kupiga umbea. Kama umeamua kusema jambo na unauhakika nalo ni vizuri kuliweka wazi ili watu wakuunge mkono potelea mbali kama utahatarisha uhai wako. Vinginevyo ni ramli hizo. Maana hakuna tofauti na mganga wa kienyeji anayesema mchawi wako ni mtu wako wa karibu mweupe, wakati huo ukijua wako watu wengi wa aina hiyo.

Itakuwa ni ndoto watanzania kupata maendeleo kama tutaendelea kushabikia na kuamini habari za kusadikika kama hizo zilizotolewa na Mzee Kitine. Angejipatia heshima kwa kuwa Jasiri kuwasadia wananchi na serikali kubainisha wazi kuwa fulani amaeiba fedha serikali ambazo alipokea siku fulani na kwa sababu fulani na vielelezo unaweka hadharani. Siyo mzee mzima kwenda kwenye TV kuongea maneno yasiyokuwa na msingi kwa nia ya kupata huruma ya wanyonge wasiojua pia kuwa kauli kama hizo ndiyo chanzo cha umaskini wao.

Ni lazima watu kama hao waepukwe kabisa katika jamii hata hilo jina la kingwendu alilopewa ni afadhali maana watu wanaopiga umbeya ni mashetani wakubwa na maadui wakubwa na chanzo kikuu cha umaskini wa Tanzania.

Mkuu, ni wezi wangapi ambao wametajwa waziwazi na vielelezo kuwekwa bayana (wizi wa EPA), lakini hakuna hatua zilizochukuliwa zaidi ya kusamehewa kabla hata ya kuhukumiwa??!!!!
Au unaizungumzia Tz ya kufikirika?
Wacha watu warushe mawe gizani, litakayempata atatoa kilio cha sauti na ndipo watu watamjua kwamba kumbe fulani naye alikuwemo!!!
 
Duh, mkuu yaelekea wewe ni mgeni hapa Duniani. Basi ngoja tukueleze haya juu ya huyu Kingwendu:

1) Alijaribu kusomea PhD miaka 7 Canada, akashindwa na kurudi na PhD ya kujisingizia. hajamaliza PhD wala hana PhD. Ni miongoni mwa wanaodanganya kwamba wana PhD, hiyo ni fact.

2) Kingwendu alitimuliwa madaraka na Nyerere baada ya kuchakachuwa gari 2 kati ya gari 6 zilizookuwa zimekabidhiwa Tz kutoka Sheli Sheli. hiyo nayo ni fact.

3) Kingwendu alimdanganya Mkapa hadi mkapa akaidhinisha dola $63,000 kupitia wizara ya afya (sio dola 50,000 kama wanavyokosea magazetini) kwa matibabu feki ambayo yalitengenezewa risit fake na jamaa wa Nijeria aliyekuwa anajilia uroda kwa mke wa Kingwendu Toronto. Kingwendu alipobanwa, akazirudisha dola $60,000 bila kuwaambia waTz alizipata wapi, kuona ameumbuka Kingwendu akahonga kamati ya bunge. Kamati ikala mkwanja na bado ikamwambia Membe, naye hakufanya ajizi akamwangamiza Kingwendu. Na hiyo ni fact.

Hitimisho: Kingwendu amtaje waziri anayemtuhumu ili ngoma hii inoge, vinginevyo ana kila sifa ya kuitwa Kingwendu, zee la majungu, na ushauri wanggu hasipewe hata sekunde 2 kwenye Tv au magazeti hadi hapo atakapotaja jina la waziri anayemshutumu. Yaani yeye anamjadiri mwizi dk 15 lakini ukimuuliza jina anasema "kafanye uchunguzi". Kingwendu at best.

Membe amewapa fact alizozipata kwa kukaa Canada...lakini you didn't do your home work properly......re seat!
 
Nahisi umekurupuka kujibu comment yangu nadhani WJM anajua nini nilikuwa namaanisha, ulichofanya wewe ni kujaladia tuhuma za kitine kwa kuziita facts ambapo sijui proof/details za uhakika nizipate wapi labda waweza kunisaidia,sakata hilo nalikumbuka ila sina kumbukumbu nzuri kuhusu undani wake, anyway let me do my homework!

Labda nikusaidie kwenye hiyo homework:

Juu ya PhD ya Kingwendu, hilo sio tatizo search kwenye shule aliyosema kasoma na watakupa facts, njoo zimwage hapa hata kama hazinogi

Juu ya kutimuliwa madarakani, hilo utahitaji msaada wa wanausalama wa taifa ili upate details za deal la magari aliyoiba. Ila facts amabayo iko wazi ni kwamba alifukuzwa kazi na Nyerere.

Juu ya Kingwendu kuiba $63,000 hii unaweza kuanza kumuuliza dokta msingiziwa, Doctor Charles Peter Arizona teaching hospital (ambaye wakati huo alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa udaktari), ukitoka hapo muulize nurse msingiziwa, Stevenson White wa clinic moja huko Seattle jina sasa nimesahau (huyu masikini alikuwa mwaka wa kwanza nurse). Ukimaliza hapo check na Ulimwengu aliyekuwa anavujishiwa kila move za Kingwendu katika kukamilisha wizi huu kutoka kwa marehemu Ng'ittu wa usalama wa taifa (RIP)

Ukishindwa kupata data huko njoo kwangu
 
- Mkuu I like your arguments kwa sababu upo fair kidogo, lakini kama kweli Kitine amelipa the price na ameridhka kwamba alifanya makosa na ni lazima kulipa price, then asingekwua na visasi hivi, maana CAG imeonyesha wazi nani ni nani!

William.

Williama, hata kwenye legal system (including USA) mtuhumiwa/mwizi anaweza kupata huruma (i.e kupunguziwa muda wa kifungo) in exchange na information ambazo zitasadia kukamata wahalifu wengine. Kama Kitine alikamatwa na akalipa price (akapoteza uwaziri) leo hii tukatae taarifa za potential wizi kwa sababu huko nyuma yeye Kitine aliiba?

Ili hoja inayosema kwamba Kitine ni muongo ana analipa visasi basi ni vizuri tukapata evidence kwamba kati ya mawaziri/naibu mawaziri 51 wa Tanzania hakuna hata mmojawao aliyepokea hela toka huko kuliko tajwa! Na inakuwaje kati ya mawaziri/naibu mawaziri 51 Membe aamue kutunga kujibu tuhuma za Mzee Kitine? Membe ni msemaji wa mawaziri wote?

Hata kama waandishi wa habari walimuuliza swali linahusiana na madai ya Mzee Kitine, kama hafamu angesema hafamu, lakini story za king'wendu zinageuza the entire equation na innocence ya Membe inakuwa under the spotlight.

Hii movie wala haijaanza, ndio kwanza tuko kwenye foleni ya kununua popcorn!
 
Hii movie wala haijaanza, ndio kwanza tuko kwenye foleni ya kununua popcorn!

Husipoteze ela kununua popcorn, Kingwendu anakimbia waandishi wa habari, na soma Nipashe ya leo. Starling wa movie hii ametoweka na wala hutamsikia tena. Kwenye movie ukiona starling anajitundika juwa movie imeshafika mwisho na kinachofuata ni majina ya washiriki wa movie tu, kwa mfano utaona wameandika Philemon aikael Mbowe = mshika taa, nk
 
kitine alisema mawaziri wote ni wezi kwa hyo ni pamoja na membe lkn mbona wenzake wote hawajajibu kajibu yeye tuu.
 
Labda nikusaidie kwenye hiyo homework:

Juu ya PhD ya Kingwendu, hilo sio tatizo search kwenye shule aliyosema kasoma na watakupa facts, njoo zimwage hapa hata kama hazinogi

Juu ya kutimuliwa madarakani, hilo utahitaji msaada wa wanausalama wa taifa ili upate details za deal la magari aliyoiba. Ila facts amabayo iko wazi ni kwamba alifukuzwa kazi na Nyerere.

Juu ya Kingwendu kuiba $63,000 hii unaweza kuanza kumuuliza dokta msingiziwa, Doctor Charles Peter Arizona teaching hospital (ambaye wakati huo alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili wa udaktari), ukitoka hapo muulize nurse msingiziwa, Stevenson White wa clinic moja huko Seattle jina sasa nimesahau (huyu masikini alikuwa mwaka wa kwanza nurse). Ukimaliza hapo check na Ulimwengu aliyekuwa anavujishiwa kila move za Kingwendu katika kukamilisha wizi huu kutoka kwa marehemu Ng'ittu wa usalama wa taifa (RIP)

Ukishindwa kupata data huko njoo kwangu

afadhali ya wewe hoja zako seems palatable na sio yule frozen mind WJM!
 
Husipoteze ela kununua popcorn, Kingwendu anakimbia waandishi wa habari, na soma Nipashe ya leo. Starling wa movie hii ametoweka na wala hutamsikia tena. Kwenye movie ukiona starling anajitundika juwa movie imeshafika mwisho na kinachofuata ni majina ya washiriki wa movie tu, kwa mfano utaona wameandika Philemon aikael Mbowe = mshika taa, nk

Sidhani! Keshatoa matangazo na posters ziko kila mahali, movie lazima!
 
Mi nadhani membe alitakiwa ajibu kama anajenga hotel ya mabilioni huko Mtwara au hajengi. Maana hiyo hotel inayojengwa inatisha, amekuwa akiingia usiku huku akitumia gari ambalo ni tinted wakati anakagua. Aseme ukweli kama anasingiziwa.
 
hata wale baadhi waliorudisha fedha za EPA hawakuamriwa na mahakama! waliwasihi wafanye hivyo la sivyo mahakamani!
issue ya Kitine sina uhakika alirudisha fedha kwa kulazimishwa au kwa ridhaa yake so as to cut the long story short, na inavyoelekea it was a clean transaction na ndo maana wabaya wake hawalisemi sana hilo kama wewe mshadadiaji!

- The ishu hapa ni Kitine sio EPA, halafu tizama huna uhakika na inaelekea meaning hujui unachosema, sasa naomba uulize wka wengine kwa nini Mkapa rafiki wa karibu sana wa Kitine, aliyemrudisha toka Canada, akamrundikia mivyeo kushoto na kulia, akafikia hatua ya kumfukuza mivyeo yote kwa ajili ya hii saga?

- Sasa nido utaijua JF, wacha kukurupuka!

William.
 
huyu william anapenda kujipendekeza kwa viongozi kama mwana mkeau anataka hurumaza kuteuliwa na wakuu? haoni hata ubunge wa kuteuliwa kaukosa? au kapewa u dc sijaona list
 
Mkuu wangu tuhuma ulizomshushia willy na wazazi wake ni kubwa sana inabidi uziletee ushahidi.

Kuhusu Anne Kilango na mumewe kupewa fedha za EPA, hayo yalizungumzwa na Sophia Simba kwenye kikao cha chama tawala wakati huo akiwa waziri wa utawala bora!! Kilango alitishia kwenda mahakamani kumshitaki lakini mpaka leo kimyaaa........ Sasa unataka ushahidi gani zaidi ya kauli ya waziri mwenye dhamana ya kusimamamia TISS na Takukuru?
 
..sidhani kama Col.Kitine amezusha tu suala hili.

..nadhani kinachokosekana ni watu wa ku-cooperate kuweka ushahidi hadharani.

..Membe naye anatumia mafumbo kujitetea kwasababu he doesnt know exactly Col.Kitine ana ushahidi gani dhidi yake.

..tatizo lingine la Membe ni kwamba yuko so incoherent. Yaani akielezea kitu chochote kile huzunguka wee mwisho hupotea kabisa na kusahau hata aliulizwa nini.
 
Haihitaji kwenda shule ili kujua kuwa serikali hii tangu mwanzo iliundwa na wezi, mtu yeyote mwadilifu asingekubali kuteuliwa kuwa waziri ktk serikali ya kijambazi kama hii, iliingia madarakani kwa hela za wizi (epa na ndugu zake wote), walipoingia tu kiongozi wao akapiga mchongo wa richmond, hakuna mwadilifu mwenye akili timamu atakubali kuwa waziri ktk serikali inayoundwa na wezi na vibaka watupu. Membe alishashindwa kazi tangu siku ya kwanza, ndo maana mishemishe zote za wizara ya nje zinafanywa na m-kwere. Kama membe angekuwa na ufahamu hata kdg angeshaachia ngazi zamani lkn yuko pale kwa sababu ya posho na michongo wanayopiga. Na kwa wanaong'ang'ania kuwa mzee Kitine amtaje waziri aliyemkusudia.... Wale mafisadi wote ambao mmeshatajiwa mmewafanya nini?!
 
Time well wasted
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom